Mgomo wa daladala ulivyopambana na polisi arusha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Adhayadaladala2.JPG


Mamia ya wanafunzi na wananchi katika Barabara ya Uhuru wakiwa hawajui la kufanya baada ya magari ya daladala kugoma.

daladala3.JPG

Madereva wa dala dala na wapiga debe wakilizonga gari aina ya Hiace lililokaidi amri ya kugoma.
HALI si shwari katika jiji la Arusha baada ya jeshi la polisi kuingilia kati na kuzima maandamano ya madereva na makondakta wa daladala kwa mabomu ya machozi walipokuwa wakielekea katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha jana.

Madereva hao wametangaza mgomo usio na kikomo hadi pale madereva wenzao zaidi ya 50 walio mahabusu na gerezani waachiwe bila masharti yoyote.


daladala4.JPG



Wapiga debe na madereva wakiwa na mabango yenye kupinga kunyanyaswa na askari wa usalama barabarani kutokana na adhabu za mara kwa mara ikiwa ni pamoja na vifungo gerezani.

HABARI/PICHA NA JOSEPH NGILISHO, ARUSHA /GPL
 
Ngoja waendelee kulichochea, wakati moto utakapolipuka watajikuta hawauwezi tena hata kwa maguruneti.
 
Haya maandamano ya vikundi mbali mbali kwa sababu mbali mbali ni dalili mbaya sana. Tuombe Mungu...
 
Back
Top Bottom