Mgomo wa daladala morogoro mjini leo umeingia siku ya tatu mfululizo.

kituro

Senior Member
Dec 25, 2010
176
15
leo ni siku ya tatu tokea mgomo wa daladala uanze mjini morogoro. watu wamekuwa wakitumia usafiri wa tax na pikipiki zijulikanazo kama bodaboda kama njia mbadala kutatua tatizo hilo ambalo kwa ujumla imekuwa ghali sana hasa kwa wafanyakazi wa kima cha chini pamoja na wanafunzi. ingawa baadhi ya maeneo mbunge wa morogoro pamoja na wafanyabiashara wengine wawili wamejitolea mabasi yao kusafirisha watu bure, wafanyabiashara hao ni mbunge wa morogoro mjini (ccm) Abood, Hood na watatu simkumbiki jina lake. pamoja na msaada huo lakini tatizo ni kubwa kwasababu mabasi hayo yakienda kule yanakokuwa yamepangiwa, huchukua zaidi ya masaa mawili kurudi tena, hivyo watu wanapanda mabasi hayo kama ikitokea ukilikuta ndiyo unapanda lakini kulisubiri inakuwa vigumu. ndugu zangu hiyo ndiyo hali halisi inayowakumba wananchi wa morogoro!
 
Back
Top Bottom