Mgomo na maandamano vyanukia UDOM

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Kuna kila dalili ya mgomo kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma hasa kolege ya education hapo kesho kutokana na kutokupewa fedha zao za kujikimu hadi hivi sasa.Ni takribani wiki mbili hivi sasa tangu chuo kilipofunguliwa lakini hawajapewa fedha zao za kujikimu hadi hivi sasa.

HATA HIVYO PAMETOKEA KUTOKUELEWANA KATI YA WANAFUNZI WALIOTOKA MAKAZINI NA WANAFUNZI WENGINE KWANI WALIOTOKA MAKAZINI WANAUPINGA VIKALI MGOMO HUO.


Source mimi mdau udom.
 
haya umeweka jina lako lakini uwe tayari wakikufuatilia si unajua mambo ya hapo UDOM yalivyo ya kijinga sana kule tu kutoa hizi taarifa unaweza kufauatiliwa
 
Mi mwenyewe siungi mkono huo mgomo, kwani wanafunzi wa hapa bongo tunatanguliza sana maslahi yetu, lakini maslahi ya taifa mnayapakisogo, tumeshuhudia madudu mengi yanayofanywa na serikali legelege kama vile dowans, rada, ndege, kiwila, meremeta, mikataba feki, wizi wa wanyama na nk, Kwanini msifanye maandamano kupinga haya? Kwani hamjui kuwa haya ndio yamepelekea taifa kuwa maskini na kukosa fedha? HIVYO MUWE MNAFIKIRIA,HABARI ZA WASOMI WAJINGA WA SIO NA REASONING TUMEWACHOKA. Anzeni na mzizi wa matatizo ambao ni ufisadi
 
Kuna kila dalili ya mgomo kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma hasa kolege ya education hapo kesho kutokana na kutokupewa fedha zao za kujikimu hadi hivi sasa.Ni takribani wiki mbili hivi sasa tangu chuo kilipofunguliwa lakini hawajapewa fedha zao za kujikimu hadi hivi sasa.HATA HIVYO PAMETOKEA KUTOKUELEWANA KATI YA WANAFUNZI WALIOTOKA MAKAZINI NA WANAFUNZI WENGINE KWANI WALIOTOKA MAKAZINI WANAUPINGA VIKALI MGOMO HUO.


Source mimi mdau udom.
hao wazee ndo magamba yenyewe hayo,,wanaringa na vimishahara vyao vya diploma vya lakilaki wanajiona wana hela sana,,,hata wakiwa makazini migomo ya ualimu ambayo mkoba kila cku anawatangazia hawashiriki,,,wezi wa kesho wakipata nafasi kwani hawatafikiria wanyonge,,,
 
Kuna kila dalili ya mgomo kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma hasa kolege ya education hapo kesho kutokana na kutokupewa fedha zao za kujikimu hadi hivi sasa.Ni takribani wiki mbili hivi sasa tangu chuo kilipofunguliwa lakini hawajapewa fedha zao za kujikimu hadi hivi sasa.

HATA HIVYO PAMETOKEA KUTOKUELEWANA KATI YA WANAFUNZI WALIOTOKA MAKAZINI NA WANAFUNZI WENGINE KWANI WALIOTOKA MAKAZINI WANAUPINGA VIKALI MGOMO HUO. Source mimi mdau udom.
Safi kabisa! Tesekeni hadi mtakapopata akili na kuacha ushabiki wa Yanga na Simba katika siasa! Mnapiga kura kama vipofu, halafu mnalalama kama kama vichaa!
 
muulizeni shemeji yenu mama rizimoja
kama na yeye hajapewa hiyo pesa ya kujikimu
tena asikosekane kwenye maandamano
 
Kama Serikali imeshindwa kuwalipa watumishi wake ndio watawalipa wanafunzi!
 
Back
Top Bottom