Hatua yoyote ile ya kugoma kutoa huduma kwa WATANZANIA wasio na hatia haitakubalika. Kwa sasa watanzania tutalaani na kupinga action yoyote kwa madaktari wanayokusudia kuchukua. Hatua hiyo ni kama uhaini kwa kukusudia kuua raia wema wanaokamuliwa kodi kwa kusomesha na kuwalipa mishahara wataalamu. Tunaamini bado kuna nafasi ya kukaa na kupata muhafaka kupitia meza ya majadiriano bila kuilazimisha, kuisulutisha na kuiwekea mashariti ya kuidhalilisha serikali eti kwa kwa kigezo ni kada muhimu. Serikali ina utaratibu wake ambao inapaswa uheshimiwe na watu wote kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Pia tunatoa mwito kwa serikali kuheshimu taaluma za wataalamu wetu kwa kuwapatia vitendea kazi na maslahi yanayokidhi taaluma husika. Suala la kada ya afya lishughulikiwe kwa ujumla wake kwa kuzingatia wataalamu wote waliopo katika kada hiyo bila kuwabagua maana wanategemeana bila kusema Daktari ni bora zaidi, kinyume na hapo ni kuzalisha Crisis nyingine ndani ya kada ya Afya kwa kusababisha chuki kati yao na mgomo baridi utakaoleteleza kuzorotesha huduma ya Afya. Hatua kwa hatua na kwa kasi, Serikali iboreshe maslahi kwa watumishi wake, maana tukisema Sekta ya Afya ni muhimu zaidi, je Walimu wanaopigana kuondoa ujinga na kuzalisha hao wataalamu wa Afya wao si ni bora zaidi? SERIKALI ISIJIINGIZE KATIKA MTEGO WA KUONA KADA NYINGINE NI BORA ZAIDI KWA MAANA KADA ZOTE ZINATEGEMEANA! Mfanyakazi wa TRA si bora zaidi, kuliko mtaalamu wa Afya za Mazingira, Mkemia au mhandisi, Mwanajeshi si bora zaidi Kuliko Daktari, na wala Daktari si bora zaidi kuliko Mwalimu, na Wala WABUNGE si bora kuliko watu wengine. Na kinyume chake ni hivyo hivyo. Tofauti inayoweza kujitokeza, madharani ni kwa kuhamasisha wanafunzi wengi wapende masomo ya Sayansi, hivyo ili linaweza kufanyika kwa wataalamu wa sayansi kupewa motisha na hata ikibidi nje ya mishahara yao. lakini suala la mishahara lazima liwe na kanuni ya uwiano.
Changamoto ninayoitoa kwa serikali kwa siku za mbeleni na kwa hatua za haraka zaidi, pelekeni kwa wingi wataalamu wa kada ambazo zina impacts za moja kwa moja kwenye maisha ya binadamu katika vyombo vya usalama kama vile jeshini, usalama wa Taifa, police na vinginevyo kwa ajili ya emergency wakati wa dharula. Lakini pia maslahi ya wataalamu wetu lazima yaboreshwe.
Nasilisha kwa maslahi ya Taifa
nyinyi mshambulieni huyo kibindi left and right, lakini mimi nauliza hivi hawa madaktari si wamesomeshwa kwa fedha zetu sisi walipa kodi wa nchi hii?
Nyinyi munaoshangiria mgomo nyote ndiyo munaokwenda hospitali za binafsi kwa hivyo hamuathiriki na huo mgomo hata ukiendelea kwa mwaka mzima.
Ila musiwasahau wale waliokufa kwa kukosa huduma.
je aliyosema pinda tarehe tisa february yametekelezwa?mbona kama umetoka usingizini??
mtaandika mtachoka! lakini watu wenye akili hawatasupport mgomo wenu! sikatai mudai maslahi yenu, lakini si kwa kutoa uhai wa Watanzania wasio na hatia na kujiona bora kuliko wengine! nyie mna vyama vyenu TMA na TUGHE ina maana vyote vimeshindwa kuzungumza na Serikali? basi anzieni hapo mviwajibishe kama havifai viondoeni! tunapashwa kuheshimu binadamu wenzetu wasiyo na uwezo wa kutibiwa Hosp za binafsi na kuepuka kuwafanya chambo. Haya ni mawazo yangu na wala sitoi mawazo kwa kufuata mkumbo hata kama nitapingwa na wachangiaji wote lakini lazima nisimamie kile ninachofikiri ni sahihi.MGOMO HAPANA NA HAPANA! TUTAWAPINGA KWA NGUVU ZOTE!
Hv Mponda na Nkya wamefanya nn hadi wajiuzuru?
nimechoshwa na hizi kauli ma dr wamesomeshwa na walipa kodi!!?hivi hujui hata madactari wanalipa kodi!
Nyinyi mshambulieni huyo Kibindi left and right, lakini mimi nauliza hivi hawa madaktari si wamesomeshwa kwa fedha zetu sisi walipa kodi wa nchi hii?
Nyinyi munaoshangiria mgomo nyote ndiyo munaokwenda hospitali za binafsi kwa hivyo hamuathiriki na huo mgomo hata ukiendelea kwa mwaka mzima.
Ila musiwasahau wale waliokufa kwa kukosa huduma.
Wewe choka lakini ndiyo ukweli ulivyo. Kwanza nyinyi munapewa misamaha kibao ya kodi. Pili hiyo kodi yenu munayolipa inaweza kusomesha wangapi wengine bila ya kuchanganywa kwa asilimia kubwa na ya kwetu munaotunyanyada?
Ndiyo hasara ya 'bure' hiyo lazima usumbuliwe. Ingekuwa sote tunalipia elimu tusingewasema kwa hilo
kwanza,niliamini pengine unaongea hivyo kwa kuwa hukua unajua ukweli,lakini sasa nimejua pamoja na kutokujua au kwa makusudi umeamua kupotosha ukweli!una kila dalili za mtu mbinafsi mwenye wivu na kufikilia kwa mafupi na kuzungumza vitu kwa kulukia bila kujua undani wake.hivi kweli unaweza thubutu kusema dactari anakunyonya!!??wewe choka lakini ndiyo ukweli ulivyo. Kwanza nyinyi munapewa misamaha kibao ya kodi. Pili hiyo kodi yenu munayolipa inaweza kusomesha wangapi wengine bila ya kuchanganywa kwa asilimia kubwa na ya kwetu munaotunyanyada?
Ndiyo hasara ya 'bure' hiyo lazima usumbuliwe. Ingekuwa sote tunalipia elimu tusingewasema kwa hilo
Huu ni uvivu wa kufikiri,madaktari wana hoja ya msingi mkuu!