Mgomo mkubwa wa wenye vituo vya mafuta 2011!

Hata Arusha kuna kamgomo ka wauza mafuta, kuanzia phillips mpaka sakina ni kituo kimoja tu kimefunguliwa Bp karibu na triple A
 
HTML:
Depot zote za kuuza mafuta ya jumla Dar es salaam zimegoma

Kama wana mafuta, halafu wanagoma kuyauza watakuwa wametenda kosa la uhujumu uchumi. kama Ewura wako serious wapitie vituoni wakague kama kweli hakuna mafuta kwenye visima husika.
 
kaaazi kweli kweli si wamuache huyu Jeykey wa watu sasa?? yaani maamuzi mengine tena ya CC hayo yanaishia heani....kuna gazeti limeandika eti mafuta yashuka bei, yaani ninachoona hapa tunachonganishwa tuzipie wenyewe kwa wenyewe maaana ukifika kwa huyu anasema hivi huyu anasema vile.....hatuna serikali kabisa tuna genge la majambazi.....
 
hahahaaaaa wametenda kosa gani bhana veve wakati wali-play the biggest role kuchangia gharama za uchaguzi? si ndio tunalipa sasa?? kwao hawalijui hilo ati
Kama wana mafuta, halafu wanagoma kuyauza watakuwa wametenda kosa la uhujumu uchumi. kama Ewura wako serious wapitie vituoni wakague kama kweli hakuna mafuta kwenye visima husika.
 
Hivi tunazo sheria madhubuti ya kushughulika na 'migomo' kama hii.
 
Ni kweli mkuu hali ni tete huko Dar yaani Oil Com nyingi zimegoma mpaka muda huu eg Oil Com segerea
 
Wagome! walau tuone nguvu na busara za serikali zitakavyo fanya kazi....!!!!! maana vitisho vya wafanya biashara vimekuwa vingi kwa serikali yetu embu wakati huu serikali ionyeshe nguvu ilizo nazo, na sio kila mtua heti kwakua anatoa huduma basi anajitutumua, Noooo!!!!!! sio sawa, ikibidi ijipange kurudisha huduma ambazo imeziachia mno kwa mawakala ambao nao wanaelekea kupoteza uzalendo na uwezo wa kuziongoza kama ilivyo kwa EWURA, kwani ni lazima kila kitu kkiwe na wakala??? itafika wakati hata uraisi nao utatafutiwa wakala, maana day after day we keep on prooving failure, kwanini, na ikibidi pawepo na sheria ya kutenganisha utumishi wa umma na biashara kwani biashara pia kushikwa na wanasiasa imekuwa ni kasoro kubwa.
 
Habari nilizo zipata sasa hivi kutoka kwa wadau wa mafuta, inaelekea makampuni ya mafuta yakagoma kesho kuuza mafuta kutoka na kupunguziwa bei ya kuuza mafuta iliyotokana na kuondolewa baadhi ya kodi.

nchi inaelekea pabaya , kama zimbabwe, tujiadhali

Sijui watapiga mabomu kwenye vituo vya mafuta?
 
Habari nilizo zipata sasa hivi kutoka kwa wadau wa mafuta, inaelekea makampuni ya mafuta yakagoma kesho kuuza mafuta kutoka na kupunguziwa bei ya kuuza mafuta iliyotokana na kuondolewa baadhi ya kodi.

nchi inaelekea pabaya , kama zimbabwe, tujiadhali

Ina maana wamesema sababu za kugoma ninni haswa?
Je ni kwamba kwa bei mpya hawatapata faida au kwa sababu tu hapa Tz hakuna neno kushuka kwa bei bali kupanda tu. Watoe Tangazo lao mapema ili serikali ijiandae kuwashughulikia. Ila ninaamini katika hili wananchi watashirikiana kwa karibu na serikali kuwashughulikia hawa wenye vituo vya mafuta kwani mtanzania wa hali ya chini ndiye victim mkubwa wa kupanda kwa bei.
 
hapa tunachezewa akili tu baada ya miezi 3 bei itarudi pale pale na kuzidi kupaa!kwani bei ya kikomo ya juma hili ni Tsh 2004!sasa kila wiki bei muongozo itakuwa inapanda kidogokidogo mapaka pale tutakapofikia ile ya awali na kuipita!
 
Hii kasumba yote waliyoileta ni serikali ya CCM, Hawa jamaa ndio kwanjia moja au nyingine wanahaki ya kugoma kutokana na muda wa serikali hii kushusha bei ya mafuta kwa muda wa siku moja tu haiingii akilini! Naomba msininukuu vibaya hata mimi napenda sana mafuta yashuke bei lakini hawa jamaa wenye vituo vya mafuta wakati bajeti ilishapitishwa nao pia walishanunua mafuta kwa bei iliyokuwepo ambayo ni ya juu kulingana na utaratibu wa serikali kushusha bei lazima wenye vituo ile kwao! kwa wazo langu ni kua hawa jamaa wangepewa muda kama wa wiki moja wawe wameuza mafuta kwa bei iliyokua inaendelea and then baada ya muda huo kuisha ndipo waanze kuuza mafuta kwa bei pungufu tuliyoisikia hapo jana! unazani wenye vituo wanapenda kuingia hasara???...!
 
hapa tunachezewa akili tu baada ya miezi 3 bei itarudi pale pale na kuzidi kupaa!kwani bei ya kikomo ya juma hili ni Tsh 2004!sasa kila wiki bei muongozo itakuwa inapanda kidogokidogo mapaka pale tutakapofikia ile ya awali na kuipita!

Ukweli ndio huo. Ukizingatia hali ya kisiasa mashariki ya kati na nchi zingine za OPEC bado si tulivu, shilingi kusuasua na hata dola ya mmarekani kutokueleweka mwenendo wake, bei za mafuta zina uwezekano mkubwa wa kupanda mara dufu ndani ya kipindi kifupi.

Leo hii bei ya kilo ya sukari imerudi kuwa shillingi 2000, lile agizo la serikali limeishia wapi?

Kitu kingine pia, punguzo hili la bei ya mafuta ni dogo sana kuweza kuleta ahueni yoyote kwa watumiaji wa kawaida ambao tunanunua kwa reja reja na katika viwango vidogo
 
Mimi sihitaji takwimu zozote,ninachosubilia ni mafuta kushuka bei.waziri alikwisha tangaza na pia ewura wamekutana na haowamiliki wamekubaliana ndiyo maana wamesema watatangaza bei mpya.
 
Back
Top Bottom