Tuyuku
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 3,292
- 1,919
Taasisi ya Ustawi wa Jamii ipo katika hali mbaya sana kutokana na menejimenti mbovu na uongozi mbovu wa serikali ya wanafunzi.
Wahadhiri wa Taasisi hiyo wapo katika mgomo toka Jumatatu wakishinikiza kukutana na waziri mkuu Pinda kutokana na mamlaka zingine kushindwa kutatua matatizo yao sugu.
Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko juu ya uongozi mbovu wa chuo hicho chini ya mapacha watatu. Mapacha hao ni kaimu mkuu wa chuo bwana Madihi, mkurugenzi wa mafunzo bwana Mchovu na mkuu wa utawala na fedha mama Mbonimipango. Mapacha hao watatu wanakiendesha chuo kama taasisi yao binafsi kwa kukithiri kwa ufisadi. Jambo linalohuzunisha zaidi ni kuwa mapacha hao watatu wote kwa pamoja hawana sifa za kuiongoza taasisi hiyo. Wote hawana PhD kama inavyotakiwa kwa taasisi inayotoa shahada. Jamambo linalosikitisha zaidi wanafanya kila jitihada ili shahada iondolewe hapo chuoni ili wao waendelee kuwepo hapo kwa maslahi binafsi.
Taasisi imevurugika kiasi cha kuwa kama chuo cha watu watatu. Wanajivunia kubebwa na katibu mkuu wa wizara ya afya Blandina Nyoni na mwenyekiti wa tume ya mipango ya rais ambaye ni mume wa huyo mama. Huyo mama ni mharibifu sana kwani alishaharibu sana TBC kabla ya kwenda Ustawi wa Jamii.
Tatizo jingine hao mapacha watatu wamemnunua rais wa serikali ya wanafunzi Gelard Simbaya. Rais huyo amehongwa kiwanja akaahidiwa kujengewa na nyumba, alihongwa kwenda kufanya field Ulaya, na ameahidiwa gari ilimradi atetee maslahi yao. Hali hiyo imepelekea uchaguzi wa serikali mpya ya wanafunzi hadi sasa haujafanyika miezi miwili zaidi ya tarehe iliyopaswa kufanyika kwani uongozi wa taasisi unahofu anaweza kuja rais ambaye hatokubaliana nao.
Ubazazi huo wa mapacha watatu umekuwa ukitimua timua ovyo wahadhiri jambo lililowafanya wahadhiri waliobaki kuamua kugoma wakishinikiza kuletwa kwa menejimenti yenye sifa inayozingatia uadilifu na utawala wa sheria.
Kiujumla hali ni mbaya sana ndani ya taasisi hiyo. Wito kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za makusudi ili kuwaokoa wanafunzi ambao ni sehemu ya wapiga kura wao.