Elections 2010 Mgombea wa CUF aomba kura apewe mgombea wa Chadema

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Habari zilizonifikia toka jimbo la Bukoba mjini zinasema mgombea Udiwani kwa tiketi ya chama cha CUF kata ya Hamugembe aliyejulikana kwa jina moja kama "Kenyanya" na ambaye amekuwa katika kiti hicho kwa miaka kumi na sasa ameomba kupitia chama chake kutetea tena kiti chake, jana alihudhuria mkutano wa Kampeini wa Chama cha Chadema uliokuwa ukifanyika katika eneo la Omukishenye Hamugembe, na kukaribishwa meza kuu kama mgeni.

Alipopewa nafasi ya kusalimia wahudhuriaji wa mkutano huo wa kampeini, kwa mshangao, diwani huyo aliomba huku akinadi wananchi wa kata hiyo wamchague kwa kura zao zote mgombea wa Chadema Ndugu Peter Rugemarila. Akionyesha kuwa anasema kile alichokusudia, alibainisha kuwa mgombea huyo wa Chadema ni mgombea anayekubalika katika kata yao na hata yeye atampatia kura yake na kura zote ambazo wananchi wa kata hiyo wanakusudia kumpatia yeye badala yake wampe mgombea huyo wa Chadema pamoja na mbunge wa Chadema ndugu Lwakatare.


Habari ndiyo hiyo.

Dr Slaa suppoter i.jpg
shabiki wa chadema Bukoba mjini akiwa katika vazi alilojitengenezea.
 
Habari zilizonifikia toka jimbo la Bukoba mjini zinasema mgombea Udiwani kwa tiketi ya chama cha CUF kata ya Hamugembe aliyejulikana kwa jina moja kama "Kenyanya" aliomba wananchi wa kata hiyo wamchague kwa kura zao zote mgombea wa Chadema Ndugu Peter Rugemarila kuwa ni mgombea anayekubalika katika kata yao na hata yeye atampatia kura yake na kura zote ambazo wananchi wa kata hiyo wanakusudia kumpatia yeye badala yake wampe mgombea huyo wa Chadema pamoja na mbunge wa Chadema ndugu Lwakatare.

Habari ndiyo hiyo.
Mchukia Fisadi, hiki ndicho anachotakiwa kukifanya Prof. Lipumba na wale wagombea wengine wote wa urais, japo ni maskapi tuu, ili ligi ibaki kwa Dr wa ukweli, Wilbroad Slaa, na Dr. (Kilemba cha Ukoka) Jakaya Kikwete.

Ila pia Chadema ikibali kuicampenia CUF kwenye maeneo inayoyaona CUF ina nguvu.

Huu ubinafsi wa wapinzani kutoshirikiana, unanitia kichefu chefu, kwani kuna maeneo wataishia kugawana kura nyingi kati yao, huku CCM ikiibuka kidedea!
 
CUF ishawekwa mfukoni na CCM, hasa baada ya makubaliano ya kitapeli huko Zenj. Hilo ni bao safi la CCM. Profesa mzima kichwa hakifanyi kazi. Inatia kinyaa.
 
JAMANI tuweke ushabiki pembeni
TUFANYE kazi ya kuhakikisha Slaa anapata ushindi PEVU ndipo tusherehekee
 
cuf na ccm wanaajenda sawa kuichafua chadema.........hata mimi ningekwa cuf na nina lengo la kweli la kuikomboa nchi ningeamua kuhamia chadema ambao wanakubalika na wana sera kabambe za kuikomboa.
 
Back
Top Bottom