Mgombea wa CHADEMA ashinda (Bulifani - Kyaka) wilaya ya Missenyi

Kasi hii imeanza mapema, nahisi kabla ya 2015 kitakuwa kimeshaeleweka
 
Du! Hadi Kyaka Bulifani kumekucha? Huko kwa mbunge mama Mshana wa magamba aliyepita bila kupingwa wananchi wake wameanza kuona mwanga! Rwakatare ukiwa na mbunge wa viti maalum wa CDM Rwamulaza piga kambi huko hadi mpakani bubare kwenye mgogoro mkubwa wa ardhi watu waamshwe na kuona mwanga wa matumaini.
 
Hongera wananchi wa Bulfani, mmeonyesha ukomavu wa hali ya juu, ni one step foward kuelekea magogoni
 
matokeo halisi cdm 401 ccm 129 tlp 2!
Kumbe TLP bado ipo, hii indicator inatosha kabisa kuionyesha CCM kule tunakoelekea, lakini ndugu zangu kina Nape na Mukama ndio kwanza wanasema CCM inaimarika, anyway ngoja tusubiri maajabu labda kwa vile wao ni wanamazingaombwe kama Mwanakijiji anavyosema.
 
Hongera sana wana-Bulifani. Kila hatua moja mbele inatupeleka karibu na ukombozi wa nchi hii. Hongera CDM!

Mh: Kahwa kumbuka cheo ni dhamana. Watumikie wananchi wako kwa upendo, uadilifu na maono.
 
Mwanzo wa Ngoma ni LELE......Safari ya ukombozi imeanza tukishawatoka kwenye level ya kata,kijiji,kitongoji basi hawana chao
 
Hii safi inabidi kuongeza nguvu vijijini ambapo huwa CCM inapita tu. Hongera Mr Kahwa
 
Mgombea wa chama cha chadema amemshinda mgombea wa magamba katika uchaguzi wa mwkt wa kijiji cha bulifani wilaya ya misenyi mshindi anaitwa deo kahwa.

HODI WENYEWE?
Mimi mgeni lakini wakati nasubiri kukaribishwa napenda kumpongeza bwana Kahwa
 
Back
Top Bottom