Elections 2010 Mgombea wa Chadema ahongwa milioni 60

Mkuu hiyo namba milioni 60 sijui ina nini kwa CCM. Nimeiona na kuisikia sana kwenye siasa za mwaka huu tokea primaries. Watu wa hesabu hapa wanisaidie, ni nini kinatoa hesabu ya milioni 60 kama rushwa wa wagombea ubunge wa mwaka huu?

Ni Mshahara na marupurupu ya miezi mitano kama angeshinda ubunge. Huu ni ulofa kweli kweli kwani kama angeshinda ubunge ndani ya miaka mitano angeingiza 720 million kwa uchache.
 
Good riddance, maana asingewafaa wananchi wa Singida huyu! Sasa CCM si lazima washitakiwe kwa kutoa rushwa na huyu naye, au Takukuru watasubiri Mtikila ashitaki! Maskini hivi Mtikila yuko Huru au anakula dona jela!

Yuko huru nadhani hana media support ndio maana hasikiki
 
Ubunge aliutaka mwenyewe na amejiondoa mwenyewe basi. Wala hakuwa mwanachama wa CHADEMA!
 
CHADEMA wajitahidi kutumia Intelligency yao au PCCB kuangalia accounts zake kama atakuwa ana cash kubwa ya ghafla na pia kufuatilia baada ya uchaguzi..

Kama kuna ushahidi wa namna yoyote, waende mbele ya vyombo vya sheria

Kazi imeshaanza na tutasikia taarifa muda si mrefu,watu wako makini katika kazi yao bana,usicheze na takukuru bana,safari hii wameamua kufanya kazi kwa nia moja.kujisafisha na kujiridhisha kwa wananchi
ili waaminike zaidi.
 
Kazi imeshaanza na tutasikia taarifa muda si mrefu,watu wako makini katika kazi yao bana,usicheze na takukuru bana,safari hii wameamua kufanya kazi kwa nia moja.kujisafisha na kujiridhisha kwa wananchi
ili waaminike zaidi.

Ukizingatia alishinda kura za maoni CCM akaondolewa ina maana hatakiwi na sasa ni muda wa kummaliza kabisa asahai siasa za Tanzania
 
Kwani alitangaza mwenyewe kuwa ameachia jimbo au Makamba amemzungumzia,
 
Yanaposemwa maneno yenye kuchoma moyo kuhusu Chadema na wanachama wapya watu huwa wakali coz hatupendi kuambiana ukweli..sasa imeanza kudhihirika kwani tulishawahi kuonya humu kwamba hawa wanaenda upinzani na kuomba kugombea wana ajeda za siri tukaonekana ni wapinga mabadiliko na sasa inajidhihirisha rangi yao ni ipi...kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu ila interest za kudumu ambazo ni pamoja n akupata madaraka.
 
Watu kama hao unachukua burdizo unaminya ili ageuke kuwa bwabwa kabisa
 
Hii ndo aina ya wagombea ..interest zao mbele..za taifa mwisho au hazipo kabisa..!!
Maendeleo tutayaangalia kwenye TV tusipobadili tabia za aina hii katika uchaguzi huu..!
 
Duh, ningemwona huyu jamaa ningemrushia hata mawe kupunguza hasira zangu.

Mkuu usipate shida bure ya kujitakia murder case. Siasa ni biashara kama ilivyo biashara nyiginezo.!!!! Jina la kampuni ni chama alicho mtu!!!
 
Ndio, hio ndio siasa bwana, wanasiasa wengi wako kifedha zaidi na kama ikigundulika na ushahidi upo kuwa kweli jamaa kama m60, takukuru wafanye kazi yao na chadema nao wamshitaki huyo mgombea wao.
 
katika mazingira ya namna hii, demokrasia ya kweli Tanzania itapatikana baada ya vijana walioelimika kujitoa ili kupambana. Nchi inakwenda kubaya, wagombea, wapiga kura wana-nunuliwa, ufisadi utakomeshwaje? Vijana inabidi tujitoe tukapambane majimboni!
 
Kazi imeshaanza na tutasikia taarifa muda si mrefu,watu wako makini katika kazi yao bana,usicheze na takukuru bana,safari hii wameamua kufanya kazi kwa nia moja.kujisafisha na kujiridhisha kwa wananchi
ili waaminike zaidi.
Ni kweli ila penye haki ni pale penye mkono mrefu....Nataka kufanya mawasiliano na uongozi wa JF kabla ya upload baadhi ya clip kaadha hivi za maongezi ya hao wakuu wa CCM, kuhusu ili sakata na huyu bw kuhongwa million 60 na kuahidiwa u-DC...
 
Kazi imeshaanza na tutasikia taarifa muda si mrefu,watu wako makini katika kazi yao bana,usicheze na takukuru bana,safari hii wameamua kufanya kazi kwa nia moja.kujisafisha na kujiridhisha kwa wananchi
ili waaminike zaidi.

Aaa wapi bwana; Tabora Mtu alikamatwa na shs 1m live lakini hatuoni kitu. Elia amepiga chenga ya mwili basi tuache yaishe.
 
Good riddance, maana asingewafaa wananchi wa Singida huyu! Sasa CCM si lazima washitakiwe kwa kutoa rushwa na huyu naye, au Takukuru watasubiri Mtikila ashitaki! Maskini hivi Mtikila yuko Huru au anakula dona jela!

Yupo amejaa tele, hata leo nimemuona pale Benjamin Mkapa Tower! Kama kawaida yake ndani ya suti!!
 
Tfadhalini tuache kukimbilia kuwahukumu watu kutokana na shutuma zinazotoka kwa watu wanaotumia majina ya vivuli. Hivi mna uhakika gani kuwa sababu pekee iliyomyfanya aitoe ni kuhongwa hizo milioni sitini. Kunajengeka utamaduni kuwa kila anayebadili maamuzi ama kuondoka upinzani basi ni lazima amehongwa. Nawaua wengi tu ambao wameondoka upinzani kutokana kushindwa kuvumilia mafyongo yaliyoko huko kama ambavyo wapo wanaoondoka CCM kwa sababu kama hizo.

Jamani kama kweli tunataka mbadala makini na wa kuaminika ni lazima tujiepushe na hizi siasa hovyohovyo za kukimbilia kutuhumu watu mambo ya ajabu hata bila ya kuwa na ushahidi.

Kama kuna mtua ana ushahidi wa dhahiri kuwa mtu huyu amejitoa kugombea ama kurudi CCM kutokana na kuhongwa atoe vielelezo vyako lakisi sio hizi hadithi za eti reliable source....

Inasikitisha kuona jinsi gani baadhi ya wanaJF wanaotilia mkazo umakini wanakimbilia kuconclude tuhuma bila hata kufuatilia ukweli wala undani wake....

omarilyas
 
Afadhali huyo ameonyesha rangi yake mapema kabla hatujampa dhamana ya kwenda kututumikia.
Hata hivyo, ni kwa faida gani hawa CCM wanafanya hayo?
Je, uongozi unauzwa nchi hii?

Naomba kauli za kukemea rushwa zipigwe marufuku kwa viongozi wa CCM kwa kuwa wanaishi kwa kutegemea rushwa.
 
Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, kwa tiketi ya Chadema Elisha Nkhambaku amerudi tena CCM baada ya kufatwa na uongozi wa juu wa CCM ukimsihi arudi CCM ambako alijiengua baada ya kushinda kwenye kura za maoni na NEC kumuengua kwenye kinyanganyiro hicho.Elisha ambaye alikuwa amejiunga na Chadema ili kugombea kwenye Jimbo hilo la Singida Magharibi amejitoa Chadema baada ya kupewa million 60 na kuahidiwa u-DC kwenye jimbo jipya...

Source: Zimetoka kwa mtu wakaribu sana ambaye alikuwa ni mmoja ya watu waliomfuata Elisha.


source wako ni mtu aliyefuata Elisha na kumpa kiasi hicho cha fedha kisha akatoa siri kwako..... imekaa kama propaganda ya kisiasa vile
 
duh, ndio maana naziogopa siasa za bongo, kwani kule pemba mmoja tu aliwahi kununuliwa Msabah tangu mfumo huu wa vyama vingi uanze
.

Wanaotoka CHADEMA kwenda CCM wamenunuliwa!!!!!!!! je, Wanaotoka CCM kwenda CHADEMA nao wananunuliwa au? Siasa sio hasa hata kidogo.
 
Alafu mnawaonea dada zetu kwa kuwaita CHANGUDOA. Kuna tofauti gani hapa?
 
Back
Top Bottom