Elections 2010 Mgombea wa Chadema ahongwa milioni 60

Uncle Rukus

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
2,415
398
Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, kwa tiketi ya Chadema Elisha Nkhambaku amerudi tena CCM baada ya kufatwa na uongozi wa juu wa CCM ukimsihi arudi CCM ambako alijiengua baada ya kushinda kwenye kura za maoni na NEC kumuengua kwenye kinyanganyiro hicho.Elisha ambaye alikuwa amejiunga na Chadema ili kugombea kwenye Jimbo hilo la Singida Magharibi amejitoa Chadema baada ya kupewa million 60 na kuahidiwa u-DC kwenye jimbo jipya...

Source: Zimetoka kwa mtu wakaribu sana ambaye alikuwa ni mmoja ya watu waliomfuata Elisha.
 
Namfahamu sana Elisha, atakuwa amejimaliza kwa kufanya hivyo. Alikuwa na mtaji mzuri wa kushinda baada ya NGO yake kufanya vizuri katika masuala ya maendeleo jimboni humo. Kukosa msimamo ni hatari.
 
Mkuu hiyo namba milioni 60 sijui ina nini kwa CCM. Nimeiona na kuisikia sana kwenye siasa za mwaka huu tokea primaries. Watu wa hesabu hapa wanisaidie, ni nini kinatoa hesabu ya milioni 60 kama rushwa wa wagombea ubunge wa mwaka huu?
 
Nilisema hapa CHADEMA wasichukue makapi ya CCM, yatawatokea puani. Watu wakasema ooooh, aaaah.

Sasa mnayaona. Na bora hata huyu karudi CCM kabla ya uchaguzi, kuna wengine watabaki upinzani na kuuhujumu upinzani huu huu bungeni.
 
Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, kwa tiketi ya Chadema Elisha Nkhambaku amerudi tena CCM baada ya kufatwa na uongozi wa juu wa CCM ukimsihi arudi CCM ambako alijiengua baada ya kushinda kwenye kura za maoni na NEC kumuengua kwenye kinyanganyiro hicho.Elisha ambaye alikuwa amejiunga na Chadema ili kugombea kwenye Jimbo hilo la Singida Magharibi amejitoa Chadema baada ya kupewa million 60 na kuahidiwa u-DC kwenye jimbo jipya...

Source: Zimetoka kwa mtu wakaribu sana ambaye alikuwa ni mmoja ya watu waliomfuata Elisha.
Kapata alichokuwa anatafuta,hapa TZ wanaogombea ubunge wanatafuta ngawira na sio kwa ajili ya kuwatumikia wananchi,ndio maana kwa sisi wengine siasa ni "taaluma ya kihuni''abadani siwezi nikawa mwanasiasa hasa wa pande hii ya TZ
 
Tanzania tuna safari ndefu sana hasa ukizingatia tunaongozwa na serikali ya CCM ambayo imejaza wezi wa rasilimali zetu, hivyo wanakuwa makini sana ili upinzani usijepata nafasi ya kuingia Ubungeni kwa wingi ili waweze kuendela kula kiulaini.
 
=======

Lakini Mganyizi una uhakika na chanzo chako hicho? Peleleza vema maana Elisha alikataa kata kata alipofuatwa hata kabla ya kuchukua fomu, na walidiriki hata kumpa 100 Mil akawatishia kuwaitia Takukuru.
 
Ndio nina uhakika na chanzo hicho na hili siyo jambo la kujificha.. Kwa maelezo zaidi soma Gazeti la mwananchi la leo limeandika kuhusu Elisha kurudi CCM.
 
Haaaa sasa Uongozi wa CHADEMA KAMA UNAWEZA UTEUE MWINGINE Alaaa haya makapi sasa yanatutokea puani:confused2:
 
Nilisema hapa CHADEMA wasichukue makapi ya CCM, yatawatokea puani. Watu wakasema ooooh, aaaah.

Sasa mnayaona. Na bora hata huyu karudi CCM kabla ya uchaguzi, kuna wengine watabaki upinzani na kuuhujumu upinzani huu huu bungeni.

watu kama hao wanastahili kupigwa Risasi kwa usaliti,
 
Duh, ningemwona huyu jamaa ningemrushia hata mawe kupunguza hasira zangu.
 
CHADEMA wajitahidi kutumia Intelligency yao au PCCB kuangalia accounts zake kama atakuwa ana cash kubwa ya ghafla na pia kufuatilia baada ya uchaguzi..

Kama kuna ushahidi wa namna yoyote, waende mbele ya vyombo vya sheria
 
Mpaka Kikwete na mtandao wake waondoke madarakani watakuwa wameshaitumbukiza Tz kwenye 'coma'.... na kuja kuizindua tena huko itachukua miaka mingi sana. Yaani wao sasa baada ya kuona hali ni mbaya kwao wanatumia kila mbinu ili kubakia madarakani... fedha za wizi, mahakama kuu, media na kila aina ya uhuni. Kinachotia hofu ni madhara ya siasa za aina hii....
Nashangaa na watu wasomi na wenye uelewa wa 'ku-forecast' mambo kama jaji mkuu na viongozi wa kidini wanatumika kuitumbukiza Tanzania kwenye hii hali.. hawaoni madhara yake kwa miaka ijayo??
 
CHADEMA si chama cha siasa bali NGO ya Ndesamburo,Mtei & Co.Hawana umakini wako tayari kupokea makapi
 
CHADEMA wajitahidi kutumia Intelligency yao au PCCB kuangalia accounts zake kama atakuwa ana cash kubwa ya ghafla na pia kufuatilia baada ya uchaguzi..

Kama kuna ushahidi wa namna yoyote, waende mbele ya vyombo vya sheria

naona mkuu unamwaga mchele kwenye kuku wengi.
 
Niliwahi kusema hapa kwamba KOSA ambalo chadema wanalifanya ni kuwaamini wanaojiunga na chama hicho ktk kipindi cha lala salama ya uchaguzi. Walipaswa kumpokea na kuanza kummezesha maji yenye sabuni za chadema awe msafi kisha apewe jimbo.
Tusikimbilie madaraka tukidhani ndo suluhisho la mwisho.
Dawa ni kujipanga na kuamini timu uliyo nayo haitakuangusha.
Poleni chadema
 
Back
Top Bottom