Elections 2010 Mgombea wa CCM Nzega ashindwa kuanza kampeni

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
kutokana na wananchi wa nzega kutokubaliana na kuenguliwa kwa mgombea wao aliyeongoza kura za maoni. mgombea waliompitisha Dr Hamisi Kigwangala ameshindwa kuanza kampeni hadi sasa kutokana na upinzani ndani ya chama chake. hadi sasa anahakiangaika kuwahamisha makatibu wa ccm wa chama na wa vijana akisema ndio wanampiga vita
 
Si Makamba aende kumfanyia kampeni, Bashe kachaguliwa na wananchi Kigwangala kachaguliwa na NEC CCM wapi na wapi.
 
kutokana na wananchi wa nzega kutokubaliana na kuenguliwa kwa mgombea wao aliyeongoza kura za maoni. mgombea waliompitisha Dr Hamisi Kigwangala ameshindwa kuanza kampeni hadi sasa kutokana na upinzani ndani ya chama chake. hadi sasa anahakiangaika kuwahamisha makatibu wa ccm wa chama na wa vijana akisema ndio wanampiga vita

Mwaka wa Nyani Kufa....
Wilaya nyingi zinateleza....
 
Mwaka huu atakiona, huyu jamaa kiburi sana kaka, Mwaka huu ni heri akose hilo jimbo n CCM wajue kuwa watu wametuchoka.
 
Mwaka huu atakiona, huyu jamaa kiburi sana kaka, Mwaka huu ni heri akose hilo jimbo n CCM wajue kuwa watu wametuchoka.

Wapinzani wamo ndio maana mgombea wa CCM anatakiwa kuanza kampeni
 
... akisema ndio wanampiga vita






ukiua kwa upanga nawe utakufa kwa upanga. bashe aliletwa na mafisadi; WAMA wakawazidi kete mafisadi. hiyo ni vicious cycle.

mafisadi walimwua selelii kisiasa; ikulu ikawamaliza mafisadi/bashe. sasa laana ya 'kula nyama ya mtu' imemrudia huyo mteule wa ikulu.


ukweli ni selelii tu ndiye aliyetakiwa kuwa chaguo la wana nzega kwani alishika ,japo, nafasi ya pili kwenye kura za maoni akapewa wa tatu.
 
Hehehehe hehehe
CCM nambari wani chama dume. wana akili kushinda watanzania wooote.
na ni wahuni na wapuuzi kuliko watanzania wooote
 
wapinzani wameweka wagombea hao wawili na anayeuzika sana ni Meza isipokua i dought kama atakuwa na uwezo wa kiuchumi wa kuhimili mikiki mikiki ya kampeni maana as I said Chadema makao makuu wamekariri majimbo ya uchaguzi hivyo hawapo bize sana kwenye majimbo mengine japo kwa NZega wangewekeza nguvu kidogo mno jimbo ni lao!
 
Mgombea wa CHADEMA Nzega ni mtaji tosha kwa mgogoro wa wanaCCM, kimsingi mgombea wa CCM amesusiwa na wanachama wake na kinachotokea ni kuwa wapenzi wote wa Bashe wameamua kujindaa kumchagua mgombea wa CHADEMA ili kukikomoa Chama kwa kushindwa kuwapatia mgombea waliyompenda.
Na hasa inatoka na hali halisi kuwa baada ya BASHE kuenguliwa ndiyo WAKUU wakarudi na kudai hana tatizo la URAI lakini hawakuweza tena kumrudisha kwenye ushindi wake. Wanachama wanaona kuwa ilikuwa njama ya makusudi na dawa yake ni kikichapa viboko CHAMA kwa Kutompa ushirikiano mgombea MTEULE wa VIONGOZI na kumpa ushindi mgombea wa upinzani
 
Wakuu;

Mimi natokea Nzega japo sipo huko kwa muda mrefu sasa, Meza aligombea mwaka 95 kupitia NCCR na ilisemekana kwamba alishinda ila kura zake ndio hivyo tena zilichakachuliwa...; Jamaa ni mfanya Biashara maarufu sana pale Nzega na naweza sema pasipo shaka ATAPITA na atakuwa Mbunge wa Nzega baada ya Selelii.

Habari ndio hiyo!
 
Back
Top Bottom