Elections 2010 Mgombea wa CCM adai ameleta televisheni Mbeya

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Thursday, 30 September 2010 19:57 0diggsdigg

Brandy Nelson, Mbeya
MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbeya mjini kupitia CCM, Benson Mpesya amewasihi wakazi wa jimbo hilo wamchague kwa mara nyingine kwani ndiye aliyeleta Telesheni ya TBC1 na Star TV katika uongozi wake wa kipindi kilichopita.

Akizungumza katika moja mikutano yake ya kampeni juzi katika eneo la Uhindini jijini Mbeya alisema anashangazwa na watu wanaosema kuwa katika kipindi cha uongozi wake hakuna alichokifanya huku kukiwa na mambo mengi ambayo ameyafanya.

“Nataka niwaeleze mambo niliyoyafanya katika kipindi cha miaka 10 kwamba ni mengi, lakini kikubwa nimeweza kuwaletea televisheni ya TBC na Star TV kwani huko nyuma hivi vitu havikuwepo,”alisema.

Mpesya alisema pamoja na kuleta televisheni hizo ameweza kujenga ukumbi wa kisasa wa Benjamini Mkapa ambapo mmiliki wa ukumbi huo ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Mbunge huyo alisema mambo ambayo amefanya katika kipindi hicho,ni pamoja na kubadilisha Chuo cha Ufundi Mbeya (MTC) na kuwa Taasisi ya Sayansi na Tekonolojia (MIST) na kujenga Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo tayari amemuomba Mgombea urais Jakaya Kikwete kujenga wodi tatu katika hospitali hiyo.

Aidha mgombea huyo alionyesha kumbeza mgombea wa ubunge kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu.

Alisema kuwa atawashangaa wakazi wa Jimbo la Mbeya kama watamchagua mtoto ambaye ni mwanafunzi wake na anavaa ‘kata kei na heleni’ wakati yeye ameweza kuwafanyia mambo mengi na kielimu amemzidi kwani mpaka sasa ana shahada mbili.

source: Mwananchi

Mpesya, uwe unaangalia maneno ya kuwaambia wapiga kura wako, unakili kuwa joseph mbilinyi ni mwanafunzi wako na anavaa kata kei na heleni!! nani alimfundisha? Wewe si ndiyo mwalimu wake? Kama mwanafunzi anavaa heleni na kata kei si mwalimu wake itakuwa zaidi maana mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu.

hana jipya kabisa huyo choka Mbaya wanambeya fanyeni mabadiliko.
 
Thursday, 30 September 2010 19:57 0diggsdigg

"Nataka niwaeleze mambo niliyoyafanya katika kipindi cha miaka 10 kwamba ni mengi, lakini kikubwa nimeweza kuwaletea televisheni ya TBC na Star TV kwani huko nyuma hivi vitu havikuwepo,"alisema.

Hilo ndo kubwa..? sasa hayo madogo sijui ni kitu gani..
Tuna muda mrefu wa kufikia maendeleo tukiendelea na wabunge kama huyu..!
 
Ha ha ha, ati ukumbi umejengwa na Halmashauri, kisha anasema yy ndo kajenga, so kila diwani wa manispaa husika naye anaweza akajipa shavu kuwa arudishwe kisa amekuwapo kwny hatamu wakati ukumbi ukijengwa. Jipange vyema SUGU umng'oe MFA MAJI huyo maana naona anatapa tapa tu, hoja kwishnei, teh teh!
 
Thursday, 30 September 2010 19:57 0diggsdigg

Brandy Nelson, Mbeya
MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbeya mjini kupitia CCM, Benson Mpesya amewasihi wakazi wa jimbo hilo wamchague kwa mara nyingine kwani ndiye aliyeleta Telesheni ya TBC1 na Star TV katika uongozi wake wa kipindi kilichopita.

Akizungumza katika moja mikutano yake ya kampeni juzi katika eneo la Uhindini jijini Mbeya alisema anashangazwa na watu wanaosema kuwa katika kipindi cha uongozi wake hakuna alichokifanya huku kukiwa na mambo mengi ambayo ameyafanya.

"Nataka niwaeleze mambo niliyoyafanya katika kipindi cha miaka 10 kwamba ni mengi, lakini kikubwa nimeweza kuwaletea televisheni ya TBC na Star TV kwani huko nyuma hivi vitu havikuwepo,"alisema.

Mpesya alisema pamoja na kuleta televisheni hizo ameweza kujenga ukumbi wa kisasa wa Benjamini Mkapa ambapo mmiliki wa ukumbi huo ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Mbunge huyo alisema mambo ambayo amefanya katika kipindi hicho,ni pamoja na kubadilisha Chuo cha Ufundi Mbeya (MTC) na kuwa Taasisi ya Sayansi na Tekonolojia (MIST) na kujenga Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo tayari amemuomba Mgombea urais Jakaya Kikwete kujenga wodi tatu katika hospitali hiyo.

Aidha mgombea huyo alionyesha kumbeza mgombea wa ubunge kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu.

Alisema kuwa atawashangaa wakazi wa Jimbo la Mbeya kama watamchagua mtoto ambaye ni mwanafunzi wake na anavaa ‘kata kei na heleni' wakati yeye ameweza kuwafanyia mambo mengi na kielimu amemzidi kwani mpaka sasa ana shahada mbili.

source: Mwananchi

Mpesya, uwe unaangalia maneno ya kuwaambia wapiga kura wako, unakili kuwa joseph mbilinyi ni mwanafunzi wako na anavaa kata kei na heleni!! nani alimfundisha? Wewe si ndiyo mwalimu wake? Kama mwanafunzi anavaa heleni na kata kei si mwalimu wake itakuwa zaidi maana mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu.

Kama maneno haya ya kuwaletea wananchi TBC na STAR TV imetoka kinywani mwake, basi nimeanza kutilia shaka hizo shahada zake mbili. Maana sioni tofauti ya mvaa kata kei na msomi hapo!
 
Back
Top Bottom