lucious_lyon
JF-Expert Member
- Jul 20, 2015
- 246
- 290
Lowassa anatumia usafiri wa daladala kufikia Wananchi wa hali ya chini sehemu mbali mbali kupata maoni yao.
Mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa Edward Lowassa akiwa kwenye daladala leo Agosti 24, 2015 asubuhi kuangalia kero za wananchi.
Hapa ni maeneo ya Gongolamboto kuelekea Chanika ‪wakati akijaribu kuzungumza na wananchi moja kwa moja kwa njia ya kuwaweka karibu ili kujua matatizo yanayowasumbua.
Mgombea mwenza wa Urais kupitia CHADEMA,Juma Duni Haji amesema kuwa ziara ya leo ya kushtukiza ya Lowassa na yeye huko Mbagala ni ya kuwasalimu tu malofa wenzao. Duni ameyasema hayo Mbagala alipokuwa akiutuliza umati wa watu uliotamani uhutubiwe.
Duni aliwataka wananchi kuwa wastahamilivu hadi Jumamosi juma hili utakapofanyika mkutano wa kampeni kwakuwa leo hakukuwa na ratiba ya mkutano wa kampeni.