Elections 2010 Mgombea ubunge huyu wa CCM alitokea wapi?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233


Jamani hii nimeipata live kutoka kwa swahiba wangu aliye Shinyanga. Anasema mgombea ubunge wa CCM jimbo la Shinyanga mjini aliyemtaja jina la Steven Masele hatakiwi na wana_CCM kwa sababu siyo mtu wa pale.

Swahiba yangu huyo anasema wana-CCM Shinyanga wanashangaa katokea wapi huyu kwani hana makazi pale na anaishi gesti. Kila siku anabadilisha gesti kwani watu humfuata na kumpigia kelele aonyeshe makazi yake.

Inasemekana mtu huyu alikuwa anafanya kazi TIGO, kanda ya Ziwa na hadi sasa haijulikani kwao ni wapi, kwani hata hilo jina la Masele ingawa ni la Kisukuma kuna wasiwasi alijipachika tu kwani hajui hata Kisukuma vizuri!

Wadau, nashindwa kuzithibitisha hizi habari kutoka kwa mtu mwingine lakini naomba mwenye habari zaidi kuhusu huyu bwana atuwekee hapa.
 
Bora ni mtanzania kigezo cha anaishi wapi sio chenzo cha kuwa kiongozi bora
 
Bora ni mtanzania kigezo cha anaishi wapi sio chenzo cha kuwa kiongozi bora

Hii nikweli.
Kuulizana kwenu wapi ni ubaguzi ... na sisi tunaamini kila mtanzania ana haki ya kuishi popote pale TZ mradi havunji sheria.
kama hawamtaki kwa sababu wanaona hafai nivyema .... hizo kura zao wampe mgombea wa chama cha upinzani.
 
naona tatizo ni kule kutokuwa na makazi ya kuduma, sasa kiongozi gani mwenye kukaa gesti? sasa matokeo yake ndio huko kuzidisha maswali, mbona kuna mbunge Muarabu na walimpigia kura?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom