Mgombea ubunge Arumeru mashariki ametoboa sikio

Naona mmekosa hoja mmeingia kwenye masikio . Kwani ubunge unaongozwa na masikio ? Acheni kuongea ujinga kama mnakunywa komoni . Alaah !!!

Kwani hiyo nayo ni shida? Atakayefanyakazi na wananchi jimboni ni mbunge na sio sikio lake. Watu mnapenda kujadili mambo ya k.i.j.i.n.g.a!
Uongozi ni pamoja na kuwa na maadili mema hasa yanayoendana na jamii unayoiongoza. Huwezi kuwa imamu au mchungaji ukapanda kwenye kibweta na bukta kwa kisingizio cha kwani bukta ndio imamu au mchungaji.

Kwa Tanzania mwanamme kutoboa sikio ni kitu cha ajabu si maadili yetu kwa hilo hata mtetee vipi. Yeye katoboa sikio moja kwa ajili ya kuweka hereni, si kama utamaduni wa kimasai unaojulikana. Nasikia kaishi Uingereza, tunajua utamaduni wa huko, vijana wengi wanaotoboa kwa ajili ya ubishoo, lakini nilisikia wengine wana maana zao nyingi mbaya, wanapotoboa say sikio la kushoto wanajitambulisha kuwa wao ni watu wanaotumia kitu fulani, kwa hiyo inakuwa rahisi kujua huyu ni mwenzetu wanapokutana. Tusitake kuhalalisha utamaduni hata kama ni mbovu kwa ajili ya mtu mmoja.
 
Makupa siku hizi unabusara sana, au ni kipindi hichi cha joto, usije badilika tabia mvua zikianza

Mkuu LAT siku zote huwa nina busara na nashukuru kuwa wote mmeanza kunielewa sasa, hata kisu kizuri ni kile chenye makali pande zote
 
Uongozi ni pamoja na kuwa na maadili mema hasa yanayoendana na jamii unayoiongoza. Huwezi kuwa imamu au mchungaji ukapanda kwenye kibweta na bukta kwa kisingizio cha kwani bukta ndio imamu.

Kwa Tanzania mwanamme kutoboa sikio ni kitu cha ajabu si maadili yetu hata mtetee vipi. Yeye katoboa sikio moja kwa ajili ya kuweka hereni, si kama utamaduni wa kimasai unaojulikana. Nasikia kaishi Uingereza, tunajua utamaduni wa huko, vijana wengi wanaotoboa kwa ajili ya ubishoo, lakini nilisikia wengine wana maana zao nyingi mbaya, wanapotoboa say sikio la kushoto wanajitambulisha kuwa wao ni watu wanaotumia kitu fulani, kwa hiyo inakuwa rahisi kujua huyu ni mwenzetu wanapokutana.

mbona msimwambie kinega mwenzenu sugu ? Au yeye haimuhusu ?
 
usingeandika hereni ningekushangaa. Jamaa anatembea barabarani mwendo mdundo huku anarusha mikono, mara anashika flaiz utadhani kama ana rap vile, na hereni imening'inia sikioni yaana raha burudani mustarehe!

Ana umri gani huyo mtu?
 
Makupa siku hizi unabusara sana, au ni kipindi hichi cha joto, usije badilika tabia mvua zikianza

Mgombea aliyepita hayupo katika kundi lake ndo mana unaona anarusha mawe.
Ila uwezo wake wa kufikiri upo palepale.
 
Nani kakuambia sugu katoboa sikio wewe?mbona unakua mdandiaji na mpayukaji bila ushahi?

wadandiaji siku zote wanadandia nyuma . Samahani kama nimekudandia nyuma mkuu vumilia.
 
acha kutoboa sikiao...hata kama anatobolewa hayo yangekua ni mambo yake.tunachotaka watanzania ni mtu wakutuondoa kwenye hili janga la wezi,dhulumati,,fisadiz na wapumbavu wote wa sisiemu.tunahitaji kiongozi wa kutuletea maendeleo sio wakututawala nakutufanya misukule,tunahitaji mtu wakusimamia haki na miradi kuiendeleza na kuisimamia
 
Back
Top Bottom