Mgombea ubunge Arumeru Mashariki afukuzwa kazi

Huyu kwanza nani angempa ubunge?? Ukuu wa shule umemshinda na shule inaelekea kufa
 
Huyu kwanza nani angempa ubunge?? Ukuu wa shule umemshinda na shule inaelekea kufa

Shule zote za jumuiya ya wazazi magamba ni hoi bin taaban,wale usitupe lawama kwa walimu wakuu
 
Hizi shule zilishule zilozosajiliwa kama jumuia ya wazazi Tanzania.Mamlaka husika hazioni kua baada ya mfumo wa vyama vyingi visingekua na itikadi za chama kimoja?

Jumuia ya wazazi Tanzania haipaswi kua na itikadi ya kichama cha siasa.Ushauri
 
Ni kawaida kwenye ccm kufanya hivyo, ni kutokana na uchafu wao wa ndani. Lakini kuna siku inakuja watalia na kusaga meno Mungu yupo nawe mh. Utamfukuza kazi lakini huwezi kufuta taaluma yake! Chuki binafsi na roho mbaya za watu wa ccm.
 
kwangu mimi namwona kama ni mtu mwenye tamaa sana,kama yupo serious na mapambano chadema itafanya naye kazi

hapa na mimi nna wasiwasi napo,huyu jamaa inaonekana shida yake ilikuwa ni ubunge tu,anyway tuendelee kumsoma ili tumjue kiundani..
 
tumtie moyo inaonekana nikiongozi mzuri, atapata ajira bado upungufu ni mwingi wa taaluma yake
 
Hapo napata taabu sana na watu waina hii inamaana hakujua matokeo yatakuwa nini kabla ya kufanya maamuzi?

Nilimshangaa sana pale aliposema anaomba kura kwasababu amefukuzwa kazi na muajiri wake hapo natapata mashaka sana hata kama angeshinda angeweza kumatch na kasi na itikadi ya CDM.
 
Kama amefukuzwa kazi sababu aligombea chadema,Mbona atavuna maTsh yakutosha tu,maana hakuna kitu kama hicho katika Labor law it is unfair termination!
 
kila jambo lina gharama zake,kwa hiyo kwake hii ndio gharama ya siasa za kitanzania.lakini pia hata kama asingefukuzwa kazi ni lazima angeacha kazi, kwa kuzingatia kuwa shule hiyo ni mali ya moja ya asasi za ccm.
Asikate Tamaa hiyo ndio safari ya kisiasa ndivyo inavyokuwa mara zoie ina machungu yake na nina imani alijiandaa kwa hilo.
 
Kama ana nia ya dhati ya kupambana na ujinga wa Watanzania ndiyo wamempa nafasi nzuri kutoa elimu ya uraia kwa wengi tofauti na ilivyokuwa katika shule moja tu. Cha msingi wamlipe haki zake zote na huyu bwana ana mchango mkubwa sana kwa Chadema hasa ktk kipindi hiki. Hata hivyo walimu wengi tumeona ni vema kupambana ujinga wa watu wazima wanaowachagua viongozi wabovu walioifikisha hapa ilipo.
 
Back
Top Bottom