Elections 2010 Mgombea CHADEMA Nkenge ajiondoa kugombea Ubunge

Sikonge leo nilikuwa sijacheka lakini hii video imenifanya nicheke sana, mama uvumilivu umemshinda.
hahaha hahaha waziiiimu mtupu.
nadhani hata mwenyewe akiiona atapasuka mbavu na kudondoka tena
 
Kama kajitoa mimi sioni shida , the ball is rolling already chadema wateue kada aende akaendeleze vuguvugu la wanaharakati walioitikia wito wa Dr.Slaa kwa kumpigia debe Dr. NA PIA KURA ZA ubunge ziende CUF na za madiwani ziende chadema just a simple linear equation to be solved.
Napendekeza zitto na shibuda waende just for three consecutive days, mambo yakuwa sawa tu.Tumewashika hao SISIEMUUU
 
njoo CCM kimbilio la kweli la wanyonge
Ni bora nikishindwa kabisa kuvumilia kukaa Chadema nitarudi kijiweni kuishi bila chama kama nilivyowahi kuwa huko nyuma, maana siamini kama kuna chama makini na cha hakika ingawa bado kichanga kama Chadema.
 
what is said is correct we are not looking for what is done in the past but what can be done better in the future dk slaa is it
 
Ameshakula vya watu na sasa amekubali na yeye aliwe kidogo.

Maadamu mwaka huu Dr. Slaa anashinda, jamaa ndiyo wiiiii (ile ya JKT).



Kuna watu wana vituko!!!!, Sikonge, umenichekesha sana.
 
Last edited by a moderator:
kuwajua mamluki ndani ya vyama ni vigumu sana lakini huenda ni wengi sana. hasa hawa waliojiunga wakati huu wa uchaguzi kama akina Marando huwa napata hofu sana nikisikia huyu bwana ndiye anayemshauri Dr. Slaa
 
Kama kajitoa mimi sioni shida , the ball is rolling already chadema wateue kada aende akaendeleze vuguvugu la wanaharakati walioitikia wito wa Dr.Slaa kwa kumpigia debe Dr. NA PIA KURA ZA ubunge ziende CUF na za madiwani ziende chadema just a simple linear equation to be solved.
Napendekeza zitto na shibuda waende just for three consecutive days, mambo yakuwa sawa tu.Tumewashika hao SISIEMUUU

Mzee nakubaliana na wewe 100 %.

Taratibu tutawapata wanampinduzi wa kweli. Hawa waganga njaa ni bora tukawjua mapema.
 
Nadhani huyo mpiga mziki amekosa sababu ya kushawishi umma kwa kujiondoa kwake.kwani alivyoingia kwenye kinyang'anyiro aliambiwa atapewa ela?au aliingia kutafuta ela za CCM Wanazotoa kwa wagombea wa vyama vya upinzani ili wajitoe na kuwaacha wakiwa hawana wapinzani.Hata ccm wagombea hawajapewa ela pamoja na kuchangisha 50 bn.njaa itatumaliza

Ukweli ni kwamba wagombea wengi waliongia katika kampeni, hawajui gharama za kuwa mgombea.

Licha ya fedha, inahitaji mambo mengi ya kuwa tayari.

Mtu wa kweli anayejitoa kwa ukweli kufanikisha azma iwayo yoyote ile, huwa yu tayari kugharimika yeye mwenyewe kwa mambo mengi ikiwamo pesa.

Basi ukisikia mgombea amejitoa kwenye kinyang'anyiro kwa vile hajapata msaada toka makao makuu, basi ujue huyo hakufaa tangu mwanzo, huyo ni mfano wa nahodha anapoona mawimbi makali anaruka na kukiacha chombo.

Watanzania tusikatishwe tamaa na watu wa namna hiyo, bado watu wapo ni suala la muda tu.
 
Ninaendelea kusisitiza kuwa vita ya ukombozi si lelemama, Vita ya ukombozi yahitaji wanamapinduzi wa ukweli na wanaharakati wanao kubali kujitoa muhanga. Hiv Wagombea wa APPT ,SAU, CHAUSTA, NCCR MAGEUZI, NRA, JAHAZI ASILI na vyama vingine visivyo na wabunge hivyo havipati RUZUKU toka SERIKALINI wagombea hao wanapata fedha toka wapi? Gharama zao za kampeni zinagharimiwa na nani? Hivyo ni wazi wagombea wengi ktk kampeni hizi wanajitegemea kwa gharama. NDIO MAANA NASISITIZA SANA WANANCHI na WAPENDA MABADILIKO tuwachangie wagombea tunao waona ni tumaini jema kwa Taifa letu bila kujali anatoka chama gani.

Ni vyema Bwana FOCUS akawa mbunifu na mkweli wakati wa kampeni zake, kwa kuwaeleza wanaomuunga mkono kuwa kampeni zinz kwama sababu ya ukata na kuomba michango kwa wenye mapenzi mema kwake na CHAMA chake, TBC jana wameonyesha mgombea wa CHADEMA huko Njombe Bw NYAGAWA na mwisho tuliona bakuli likipitishwa ili wenye mapenzi mema na CHADEMA wachangie. Pia alionyeshwa babu mmoja akikataa katakata kuchangia kwakuwa wao CHADEMA wanaitaji kura yeye atawapa lakini sio fedha. Nimetoa ushaidi huo kuonyesha kuwa fedha ni tatizo la wagombea wengi.Ushuhuda mwingine ni wa Marehemu MB PHARES KABUYE ambaye alikuwa mwalimu mstaafu na alikuwa mbunge pekee wa TLP na katika shuhuda zake alisema alitumia usafiri wa Baiskeli na wakati mwingine kwenda kwa miguu ili kuwafikia wapiga kura na kuwaomba ridhaa yao, Bw. MREMA aliwahi kukiri kuwa Marehemu KABUYE alipambana hadi kushinda bila msaada wa Fedha toka TLP Makao Makuu.(Japo kuwa ushindi wake ulitenguliwa na mahakama) na rufaa ya Bw KABUYE ilikuwa aijasikilizwa na mahakama umauti ukamfika kwa kupata ajali mkoa wa morogoro akiwa safarini kwenda Dar) Ninachotaka kuonyesha hapa kuwa si FOCUS pekee anaye tumia gharama zake, ni wajibu wake , chama chake ngazi ya wilaya mkoa na jimbo kutafuta suluhisho na si kukimbia mapambano. KUmbuken mgombea ubunge wa CHADEMA jimbo la mbeya mjini ameandaa CONCERT ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni zake na za DK SLAA huyo ni mpiganaji SUGU ajakata tamaa na anaendeleza mapambano bila kuchoka sababu yeye ni SUGU.

JE, matatizo utatuliwa kwa kuyakimbia?NA SUMU ujalribiwa kwa KUIONJA? FOCUS kujitoa ni kukimbia tatizo hivyo ujatafuta suluhu maana CCM wapo na ulivyojitoa umewapa nafasi ya kuendelea kuwapo hivyo WEWE ndie tatizo kwa kujitoa na kusababisha wananchi wakose nafasi ya kuliondoa tatizo CCM jimboni mwao. Na kwa kuwa sumu haijalibiwi kwa kuionja wewe umeonja Mlungula wa CCM (SUMU) sasa ujue dhambi ya usaliti itakuandama kizazi hata kizazi maana Umetenda usaliti kwa kuthubutu kuwaonjesha SUMU wana NKENGE kwa kuiachia nafasi CCM iongoze tena kwa miaka mitano mingine. FOCUS huo ni usaliti maana ilibidi ujadiliane na chama chako na kufikia muafaka nasi kujiamulia wewe kumbuka uwamuzi wako unawanyima wana NKENGE haki ya kuchagua, usingegombea ili chadema wasimamishe mgombea mwingine na wananchi wapate haki ya kuchagua.

Wana JF na watanzania wenzangu ni vyema tukumbuke mwaka huu yatupasa kuchagua mtu na si chama hivyo huyu bwana FOCUS hatakama ni mgombea wa CHADEMA na wengi mnaamini kuwa chadema ni chama mbadala lakini ukweli ni kuwa hafai na kama angeshinda ilikuwa hatari kwa waTZ wote Kumbukeni CUF wanamgombe huko NKENGE mpimeni kama ni mzalendo na mwanamageuzi wa dhati achaguliwe bila kuangalia itikadi yake. Tunachoitaji mabadiliko CHANYA na lengo ni kuitoa CCM katika uongozi wa nchi, na lengo si CCM waondoke tu bali tunaowaingiza madarakani ni viongozi wa dhati na wazalendo kwa nchi yao? kama wagombea wa upinzani ni wababaishaji ni bora kumpa mgombea mzalendo na mpiganaji wa ufisadi na mpenda maendeleo wa CCM kuliko mwizi,fisadi na kibaraka wa CHADEMA au CUF (Wa upinzani).

Pamoja na hayo yote wana JF tukumbuke maoni yetu na kuhamasishana kwetu hakutokuwa na tija kama hatuichangii CHADEMA (VYAMA VYA UPINZANI) ili iweze kushiriki kampeni bila tatizo. Kumbukeni uchaguzi ni gharama na hoja ya FOCUS kuwa kazidiwa na gharama si ya kuibeza sana kw upande mwingine inamantiki. HAYA SHIME KUJITOA KWA FOCUS KUWE CHACHU WA WAPENDA MABADILIKO KUCHANGIA CHADEMA/CUF na WAPINZNI WENGINE ILI MAFISADI WASIPATE UPENYO WA KUJIINGINZA kulaghai wagombea kwa fedha zao kwa madai wagombea hawaletewi fedha za kampeni.
 
Mi nilishasema tangia awali. Chadema hamko serious. Mnabisha. Sasa kweli Chama ambacho kinataka kipewe nchi hawawezi hata kujipanga kuchagua wagombea wa ukweli. Watu wanawasikiliza, wanaingia kundini, baada ya kuona incompetence ya Mbowe jinsi anavyoendesha chama. Tartiibu wanakula kona. Its unfortunate, lakini as of now--hamko serious.
Hivi ninyi watu wa CCM mmesahau mlifikaje hapo mlipo? Mbona leo mnanyea kaburi la muasisi wenu?
 
KAMPENI ENEO LA BANDO LA CCM_.JPG
CHADEMA muwe serious jamani khaaaaaaaa
sasa hapa mnapigia kampeni chama gani? inaonyesha wengi wenu bado wana urafiki na sisem ndiyo maana wananunulika kirahisi
 
Sababu kubwa ya kujitoa ni kuwa Chama makao makuu kimeshindwa kutoa fungu la kumwezesha kufanya kampeini badala yake amekuwa akitumia fedha zake

Sasa kama kisa ni fungu la kampeni kwanini ajitoe? Alishindwa kumalizana na uongozi wake hadi afanye huo uamuzi wa kijinga??? Hapa issue ni kwamba huyu ni mamluki wa CCM na aliitafuta hiyo nafasi ili aje kukichafua chama, najua mbinu za CCM ni nyingi sana! Namlaani kwa jina la bwana, watu kama hawa ni wa kuchoma moto kama vibaka tu. Wana CHADEMA wa nkenge msimcheleweshe huyo msaliti mkubwa. Hata mimi siasa za miafrika zimenishinda kabisaaaa
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Missenyi Bw Isidory Mtaro amekutana na waandishi wa Habnari wilayani humo na kutoa ufafanuzi juu ya focas kujiondoa na hatima yake kisheria.Ni kuwa Focas wa CHADEMA alimkabidhi jana barua ya kujiondoa na kiapo cha Mahakama kikionesha kujitoa hivyo AMEONDOLEWA RASMI kwenye kinyanganyiro.
 
Nadhani huyo mpiga mziki amekosa sababu ya kushawishi umma kwa kujiondoa kwake.kwani alivyoingia kwenye kinyang'anyiro aliambiwa atapewa ela?au aliingia kutafuta ela za CCM Wanazotoa kwa wagombea wa vyama vya upinzani ili wajitoe na kuwaacha wakiwa hawana wapinzani.Hata ccm wagombea hawajapewa ela pamoja na kuchangisha 50 bn.njaa itatumaliza

Ukweli ni kwamba wagombea wengi waliongia katika kampeni, hawajui gharama za kuwa mgombea.

Licha ya fedha, inahitaji mambo mengi ya kuwa tayari.

Mtu wa kweli anayejitoa kwa ukweli kufanikisha azma iwayo yoyote ile, huwa yu tayari kugharimika yeye mwenyewe kwa mambo mengi ikiwamo pesa.

Basi ukisikia mgombea amejitoa kwenye kinyang'anyiro kwa vile hajapata msaada toka makao makuu, basi ujue huyo hakufaa tangu mwanzo, huyo ni mfano wa nahodha anapoona mawimbi makali anaruka na kukiacha chombo.

Watanzania tusikatishwe tamaa na watu wa namna hiyo, bado watu wapo ni suala la muda tu.
 
Nafikiri hata kugombea aliomba mwenyewe hakulazimishwa na mtu hiyo ndiyo demokrasia simlaumu waliobaki wataliendeleza libeneke, hata hivyo toka mwanzo alionyesha hali hiyo.

Ndio hapo sasa, aliomba mwenyewe kugombea na sasa ametoa jina..... btw, muda wa kutoa au kuweka majina si umepita?
 
Fedha za ccm walizoiba epa inzidi kututesa watz kwani bado watz wanakubali kuendelea kununuliwa japo kwa kasi ya kushuka......wengine wanakuja lakini wengi wanasema njaa inawakimbiza lakini hata wao wanawashauri watoto wao na ndugu zao kuichagua chadema..............msifadhaike mioyoni mwenu kwa kuwa mnamwamini mungu basi muaminini na dr.slaa
 
Mi nilishasema tangia awali. Chadema hamko serious. Mnabisha. Sasa kweli Chama ambacho kinataka kipewe nchi hawawezi hata kujipanga kuchagua wagombea wa ukweli. Watu wanawasikiliza, wanaingia kundini, baada ya kuona incompetence ya Mbowe jinsi anavyoendesha chama. Tartiibu wanakula kona. Its unfortunate, lakini as of now--hamko serious.
wangeapata japo theluthi ya hela za EPA ili tatizo lisingekuwa tatizo hata kidpgo kwa CHADEMA, wangejiachia na kuwapa ruzuku za kutosha wagombea wake bila kusita.
 
Binafsi namfahamu huyu bwana Focus,kwanza ninashangaa ni lini huyu bwana ameanza siasa.Ni mpiga muziki maarufu pale Bukoba mjini.Chonde Chadema watu wa namna hii liwe fundisho kwenye chaguzi zingine.Tujipange tafadhali,saa ya ukombozi ndo inakaribia.
 
Back
Top Bottom