Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,723
- 2,255
Lole Gwasika,
Duh Mazee, hapa kidogo umenitisha..Kumbe sheria ni hivyo eeeh! au jamaa ni shoga anasherehekea kivyake!
Mkuu Mkandara, Ass huyu ni yule punda!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lole Gwasika,
Duh Mazee, hapa kidogo umenitisha..Kumbe sheria ni hivyo eeeh! au jamaa ni shoga anasherehekea kivyake!
hii sheria inajielezaje waziwazi kwamba haruhusiwi? Katika statement hii wewe mwenyewe hujatoa interpretation yako tayari?Mkandara said:Huwezi kuondoa sheria (restriction) zinazomzuia mgombea binafsi ukasema ni interpret ya sheria ya mgombea yupi anayeruhusiwa wakati sheria inajieleza waziwazi kwamba haruhusiwi!.
Mimi nadhani tunachukulia swala hili kwa ushabiki na sii kufuata sheria.. hata mimi ningependa kuona wagombea binafsi lakini swali linarudi palepale..
Ikiwa leo tunashindwa kuvichagua vyama kama CUF na Chadema kwa sababu havina team tosha ya uongozi huyu mtu mmoja atakuwa amebadilisha kitu gani?
Je, akishinda ataweza vipi kuunda serikali!.. maanake inabidi tubadilishe pia sheria za bunge na Mawaziri..Hao mawaziri watatoka chama gani?.
wateule hawatapewa nafasi wateule wachague njia mbadala ya kusaidia matatizo ya wananchi. usihofu si lazima uwe mbunge kuokoa wananchi wako. sii lazima uende dodoma. hawa jamaa piga uwa hawawezi kukubali hilo.Jamani Mimi nataka kugombea Ubunge katika Jimbo moja Kanda ya Ziwa kama Mgombea binafsi kutokana na kukerwa na misimamo ya kukengeuka ya vyama vya siasa na kuwa mtumwa wa M/kiti wa Chama.Sasa Serikali imekata rufaa kupinga kuruhusiwa.Tatizo ni nini hasa?Wana JF mnaofahamu mtuelimishe.
.......Je ni kweli Jaji ali-alter constitution badala ya Kuitafsiri....
Na, jaji Masati, akiandika kwa niaba ya jopo wala hakuficha kwamba, naam, sasa tunatengua katiba:KATIBA YA JAMHURI
39. (1) (c) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama: ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
67. ( 1) ( b) Mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
21. (1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 39 ya 47 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na nanchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Vipengele vilivyotenguliwa na mahakama vilichomekwa kinazi kwenye Katiba katikati ya kesi ya kwanza, mwaka 1993, wiki moja kabla ya hukumu ya hayati jaji Lukakingira alipokubali pingamizi la Mtikila dhidi ya sheria inayotakataza ugombea binafsi. Hivyo, hukumu dhidi ya serikali, kwamba sheria ya uchaguzi ni kinyume cha Katiba, ikawa haina nguvu kwa vile serikali ilishajiwahi kuburuza muswada wa kubadili Katiba ili hiyo sheria ya uchaguzi ikubalike.MAHAKAMA KUU, 2006
``The issue therefore is whether the amendments to Articles 21(1) and Articles 39 and 67 of the Constitution is ConstitutionalIt may of course sound odd to the ordinary mind to imagine that the provisions of a constitution may be challenged for being unconstitutional
So this Court may indeed declare some provisions of the Constitution, unconstitutional.
We thus proceed to declare that the said amendments to Articles 21(1), 39(1)(c) and 67(10)(b) are unconstitutional.``
Mahakama Kuu ikakubaliana nae kwamba serikali haina nguvu kuchomeka mabadiliko ya Katiba yanayoondoa haki za msingi zilizokuwepo awali. Hivyo mwaka 2006 majaji wakafuta vipengele vipya vilivyochomekwa kwenye Katiba, kwamba ni unconstitutional. Mtikila akawa two for two, kashitaki mara mbili kashinda mara mbili.KATIBA YA JAMHURI
20 (2)ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote.
20(4) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au shirika lolote au kwa chama chochote cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa ya chama hicho.
21(1) Kila raia wa Jamhuri wa Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja, au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wanacnhi kwa hiari yao kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Swali ni, jee, Mahakama ina nguvu kutengua katiba? Kama inayo, serikali inasema mwishowe majaji wanaweza kukadilisha Katiba nzima. (Kumbuka hawabishani kama ilitengua au haikutengua.)KATIBA YA JAMHURI
98. (1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata kanuni [ifuatayo]: itaungwa mkono kwa kura za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote;
(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya 98 (1) kubadilisha masharti ya Katiba hii au masharti ya sheria maana yake ifahamike kuwa ni pamoja na kurekebisha au kusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka masharti mengine badala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya masharti hayo.
Duh! there goes our "Philadelphia Lawyer"....
And he/she did a commandable job. The rest were just trying to give their lay opinions.
....in short from what i read in your post........majaji walifanya kazi yao ipasavyo i.e. kutafsiri.....kwamba yale marekebisho yaliyofanyika yalikuwa "unconstitutional"...........
Mkandara,
hii sheria inajielezaje waziwazi kwamba haruhusiwi? Katika statement hii wewe mwenyewe hujatoa interpretation yako tayari? Kazi ya kutafsiri sheria ni ya mahakama. Na kama sheria iko ambigious huoni mahakama ina uwezo kutoa tafsiri yeyote?
buchanan;474532]Tatizo: Mahakama Kuu ya Tanzania ili-declare baadhi ya Ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kuwa ni "unconstitutional" - i.e. "the provisions of the constitution are unconstitutional!". Ibara hizo zinahusu mgombea binafsi. Msimamo wa Serikali ni kwamba kama hali hiyo ya Mahakama kuondoa Ibara za Katiba ikiachwa then mwishowe tunaweza tusiwe na Katiba kabisa.