Mgombea akamatwa kwa rushwa ya Sh500

bora takukuru ingefutwa sababu

haina lolote jipya watuambie kwanza

wale wa ccm waliowakamata wakitoa

rushwa kwenye kura za maoni wamewafanya nini?
 
Gazeti la Mwananchi,

Tuesday, 06 March 2012 20:51

MBIO za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki zimefikia patamu, baada ya mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Democratic (DP),Mohamed Abdalah Mohamed kukamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), akituhumiwa kutoa rushwa ya Sh500.

Kukamatwa kwa mgombea huyo kumekuja wakati mchakato wa uchukuaji fomu za kuwania jimbo hilo ukiwa unaendelea baada ya mgombea wa sita ambaye ni Siyoi Sumari wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kujitokea kuchukua fomu hizo. Wakati uchukuaji fomu ukiendelea jana,habari zilizolifikia gazeti hili zilisema mgombea huyo wa DP na Katibu wa Uenezi na Mipango Taifa wa chama hicho Abdul Mluya walikamatwa eneo la Maji ya Chai wakati akitafuta watu wa kumdhamini.

Vyanzo hivyo vilifafanua kwamba mgombea huyo alikamatwa jana mchana wakati akimpa kiasi cha fedha mmoja wa wapambe wake, ili akachukue kitambulisho nyumbani kwa ajili ya kumdhamini.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, tukio hilo lilitokea saa 7:00 mchana baada ya maofisa hao wa Takukuru waliokuwa wamevalia nguo za kiraia kufika eneo hilo, kuwakamata na kupeleka katika Kituo cha Polisi cha Wilaya kilichopo Usa River kwa mahojiano zaidi.
Mtuhumiwa akisimulia mkasa huo Mohammed alisema, Tukio hilo liliwaathiri kisaikolojia kwa kiwango kikubwa kwani litagharimu hata harakati zao kuendelea kuwatafuta wadhamini katika mchakato huo wa uchaguzi.

Hata hivyo, alisema baada ya mahojiano ya saa kadhaa kituoni hapo na kujieleza kuwa alikuwa katika harakati za kutafuta wadhamini.

Mkuu Polisi wa wilaya hiyo, aliwaruhusu kuendelea na mchakato huo wa kutafuta wadhamini baada ya kuchukua maelezo yao. “Nikiwa kituoni wakiwa wameshikilia nyaraka zetu tulizokuwa tunazitumia kutafutia wadhamini, OCD aliwasiliana na
Msimamizi wa Uchaguzi, Trasias Kagenzi kuthibitisha kama kweli mimi ni mgombea, ndipo niliporuhusiwa kuendelea kutafuta wadhamini,” alisema Mohamed.

Msimamizi huyo wa uchaguzi alithibitisha kukamatwa kwa mgombea huyo na kueleza sababu zake kuwa ni taarifa za raia wema waliopiga simu Takukuru baada ya kuona mtu akipewa fedha. "Baada ya kuongea na mgombea,aliniambia kuwa baada ya kumpata mtu wa kumdhamini katika eneo hilo,alimwambia kadi yake ya kupigia kura iko nyumbani, hivyo mgombea alitoa Sh500 ya Bodaboda ili aifuate ndipo alipokamatwa na Takukuru,” alisema Kagenzi.

Hata hivyo, kwa upande wake Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Arumeru,Zawadi Ngailo alisema hakuwa amepata taarifa za kukamatwa kwa mgombea huyo hadi tunaenda mitamboni.

Ovyo sana, miatano ndo hela gani haya ni masihara
 
Baada ya ku-digest hizo technical terms na huo mfano nimeipata perspective yako. Nafikiri kuna umuhimu wa kuingalia vizuri Anti-corruptio policy ya Tanzania kwa sababu naona kama inakosa uwiano wa moja kwa moja na Global Anti-corruption Policies ambazo ziko makini zaidi.
Kwa mfano katika pekuapekua yangu nimekutana na kipengele cha 'Bribe Payers Index' ambayo inabainisha kitakwimu makampuni,wanasiasa na watu binafsi wanaotoa rushwa kwenye baadhi ya nchi kama vile Pakistan,India,France,Nigeria etc.
Kuna global shift ya kubaini watoaji rushwa kwa sababu wao ndio chanzo halisi cha kuenea kwa janga la rushwa.Sisi bado tuko kwenye kuitegemea sheria yenye mapungufu ifanye kazi ya kuwakamata wapokea rushwa huku ikishindwa kuwafikia vizuri watoa rushwa.
Halafu vile vimetego vya TAKUKURU hukamata samaki wadogo tu wale wazee wa wizi na rushwa ya kalamu kama ulivyoeleza mwanzoni wameteka system yote kuanzia Anti corruption agencies mpaka Judicial system.
Hapa corruption na theft of public finance ni 'political corruption'. Yani wanao unda sheria na regulations wanaziunda in a way that their power, their offices, the facilities they use in their function and their budget zinatumikia private interest hata bila wenyewe kuhusika in the implementation. Vitu kama seating allowance, au kutumia msafara wa Raisi, ikulu etc ni aina ya political corruption. Na mara nyingi ndio corruption with theft inavo tumika. Yani public officer do things that appear be 'legal' but for private interest kabisaaaa.
halafu una cases pale watekelezaji wanachakachua good policies kwa faida zao binafsi na faida ya vyama/ndugu zao. Ndio unakuta a well aproved budget, that should benefit all Tanzanians, ila procurement tenders zinachakachuliwa na watu hula ma 20% etc.
Zote ni aina ya corruption with theft.
Hii ya kuprosecute 'honga' (corruption with no theft), tena ya tsh 500 mi naiona kama ni danganya toto tu. the bulk part is to be tackled elsewhere.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom