Mgogoro wa uongozi na wakufunzi chuo cha Ustawi utaisha lini?

Mike 1234

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
1,633
154
jamani kuna mgogoro wa uongozi na wakufunzi wa chuo cha ustawi wa jamii kijitonyama,mgogoro ulianza siku nyingi mpaka pro Rwegoshora akaondolewa,sasa nauliza wahusika mgogoro huu utaisha lini? maana una adhari kubwa sana kwa wanafunzi na taifa kwa ujumla,chuo kilisogeza muda wa kufungua muhula wa pili hivyo wale wote walikuwa wamalize mwezi wa 7 ikawa watamaliza mwezi wa 9, hivi hizo nyongeza za kodi za vyumba na chakula wanafunzi watazitoa wapi? wako wapi viongozi wasaidie hili?
 
tatizo CCM watakuwa wameshawekeza hapo, maana hizi wizara zetu ndio chanzo cha matatizo mengi sana, kuna watendaji waliowekwa kwa fadhila na hawajui kufanya kazi isipokuwa kulinda maslahi ya jamaa zao waliwaweka
 
tatizo CCM watakuwa wameshawekeza hapo, maana hizi wizara zetu ndio chanzo cha matatizo mengi sana, kuna watendaji waliowekwa kwa fadhila na hawajui kufanya kazi isipokuwa kulinda maslahi ya jamaa zao waliwaweka
nikweli kabisa pale wameweza,wamepandikiza watu wao ambao hawana sifa za uongozi,sijui nchi hii tunaenda wapi
 
Na wanafunzi wapya wanasajiliwa lini?maana selections hawajatoa bado na nimeshachoka kuingia kila cku kwny website yao jaman hawatuambii hata 2po njia panda tokea mgomo ulivyotokea hadi sasa
 
pale ccm na viongozi wao watakapoacha kuteua watu kwa itikadi za vyama ama imani zao za makanisa au misikiti, elimu yetu na mambo mengine yatasonga mbele.
wateule wanawaza kukuza imani za dini zao kwenye taasisi za umma kwa kodi za watz wote au itikadi ya chama fulani kana kwamba vingine ni dhambi
Poleni sana ustawi wa jamii na watz wote lakini tujifunze kupitia wao nasi tusijefanya hayo maofsini mwetu
 
Back
Top Bottom