Mgogoro wa Muungano: Katika Historia

Aloysius

Member
Mar 1, 2011
80
9
MGOGORO WA MUUGANO: KATIKA HISTORIA
Moja ya mambo yanayotikisa hali ya hatima ya taifa letu ambalo kwa muda limepatiwa jina la kisiwa cha amani hivi sasa ni swala la “Muungano”. Nimekuwa nikikereketwa sana kama Mwananchi wa kawaida wanchi hii kupata fursa ya kutia neno katika mkasa mzima wa mvutano huu juu ya muungano.
Ninapo sema ‘Muungano’ nina maana ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar uliyofanyika mwaka 1964 kwa hiari, mapenzi na mtizamo uliokadiriwa kuwa ni wa manufaa sana na waasisi wa mataifa haya Bwn. Hayati Abeid Amani Karume na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Niwazi kuwa manun’guniko ya muungano yanazidi kurindima kwa kasi, kiasi cha kutathminiwa kuwa pengine tukilegea muungano unaweza ukawa ni historia. Baadhi ya wazungumzaji wakisiasa wakati mwingine tumewaona wakionyesha utayari wakumomonyosha muungano, wakiufananisha na ndoa ambayo inaweza ikavunjwa muda wowote, hilihali kwa wengine muungano ni tendo lakitawa na la mwiko lisilo pasa kubezwa au kuzungumziwa kwa kiwango cha kuonyesha nia au wazo la kuuvunja. Binafsi nimekusudia kuuzungumzia muungano kwa kuunasibisha na historia ya Muungano ya nchi ya Marekani ambayo bila shaka ni muungano mkubwa na mkongwe zaidi unaoishi leo duniani. Nimemega kipande cha historia hio ambayo nina imani itatusaidia kupima kuwa tunaupeleka muungano wetu wapi? Je linalotukabili ni tatizo geni? Tatizo linaweza kuwa nini zaidi ya yale tunayoyataja au kuyafikiri?
Kabla hatujaigeukia historia, nieleze tu kuwa sidhani kama tumechungua na kubaini tatizo hasa la muungano liko wapi mpaka sasa, ni utamaduni wa kawaida kitaaluma kwamba hili kutatua tatizo lolote awali ya yote ni lazima kulitambua tatizo vema, kisha kubashiri nini inaweza ikawa chanzo cha tatizo, halafu kuchunguza ubashiri. Hali ilivo sasa nafkiri wanasiasa wanajichanganya ya nini ni tatizo na mbaya zaidi wanachanganya ubashiri (hypothesis) wao au wanauzungumzia kama ndio ukweli uliobanishwa(fact). Serikali tatu je ndio suluhu, Kutengana au serikali moja? Wakubariki majibu haya ni wananchi tena walioelimishwa juu ya athari ya maamuzi yao. hivyo basi nimeazimia kupanua uwanda wa bashiri ya nini ni tatizo hili tuchungue na kujionya juu ya matendo yetu yote ili kunusuru mustakabali wa muungano wetu.
Mwaka 1812 wananchi wa Marekani walimchagua Andrew Jackson kwa mapenzi makubwa sana kua rais wao baada yakuishinda Uingereza katika vita vya kijeshi mara kadhaa. Makamu wa rais wa Andrew aliitwa bwana John C. Calhoun
Bwana Calhoun historia inamwandika kuwa alikuwa ni ‘pandikizi la mataifa makubwa ya Ulaya katika serikali ya Marekani aliye penyezwa ili kuigawanya Marekani vipande vipande, kuidhoofisha na kuifanya itawalike na mataifa hayo’ Secret Terrorists naye Bills Hughes uk. 18-19. Sasa tugeuke kutizama mbinu alizozitumia Calhoun kisha tuzifananishe na matendo ya baadhi ya viongozi tunayo yaona hivi sasa hapa nchini.
Inasemwa kuwa kwa kusaidiwa na mataifa ya Ulaya Calhoun aliasisi shirika la gazeti nchini Marekani lililoitwa ‘United States Telegraph’ na katika gazeti alieneza nadharia aliyoiita ‘States Rights’ (haki ya mataifa) nadhria yake ilikuwa na maudhui kuwa mataifa yote yanayounda Marekani yana haki yakujienguwa toka kwenye muuungano kama wakiamua, hivo basi Coulhon, alitumia chombo cha habari kutimiza azima yake na wale anaowatumikia, pia alitumia jina la ‘haki’ akijitambulisha kama mpigania haki kwania yakutaka kuvuruga muungano.
Mbinu nyingine aliyoitumia ni kodi, KatikaMarekani ya kusini kodi kubwa ya bidhaa ilitozwa, Calhoun aliwaeleza wamerekani wa kusini kuwa hii ilikuwa sababu tosha ya wao kujimega kwakuwa walikuwa wakinyonywa. Kitabu cha John Smith Dye, The Adder’s Den Uk 22 kina haya yakusema kuhusu propaganda za Calhoun:
The South, being an agricultural region, was easily convinced that a high tariff… was injurious to them.
Kwa lugha nyingine Calhoun aliyapika mazingira huku akimsaliti Rais wake Bwana Andrew yatakayo fanya muungano uonekana mchungu mithiri ya aloevera, hili Bwana Andrew aliliona katika kitabu hicho hicho cha John Smith Dye, The Adder’s Den Uk. Wa 19, katika afra ya kumuenzi Thomas Jafferson, alipoulizwa Bwn. Andrew kuzungumza alisema; “Our Federal Union. It must be preserved.” Yaani “muungano wetu. ni lazima hudumu.” Kisha akaketi. Aliposimama Calhoun alizungumza maneno yafuatayo:
The Union next to our Liberties most dear. May we all remember that it can only be preserved by respecting the rights of the states, and distributing equally the benefits and burdens of the union.
Wadadisi waliona kwa kauli hii Calhoun aliupatia muungano nafasi ya pili baada ya uhuru, akipuuza ukweli kuwa pasina muungano kusingekuwa na uhuru, kungekuwa hata na hatari yakuwepo vita dhidi ya mataifa hayo ya Marekani wenyewe kwa wenyewe.
Hebu sasa tujihoji ipasavyo, hatuna ma-Calhoun leo katika Tanzania yetu, wanao tamka haki na hata kumnukuu Baba wa taifa Hayati Julius Nyerere, lakini ndani yao wakiwa na makusudi ya kuua muungano. Tuna uhakika kweli kuwa hatuna watumishi vibaraka wanaotaka kuuzika muungano kwa makusudi yao fulani; nilimskia mbunge mmoja akilalamika kuwa shirika la kodi nchini (TRA) linatoza kodi kwa wafanyabiashara wa Tanzania Visiwani kinyume na makubaliano ya serikali. Je tumechungua uwezekano wakuwepo watendaji ambao wanafanya mambo ya makusudi ili kuufanya muungano uwe mzigo, nakuangalia wanamtumikia nani kama hawaitii serikali yao?
Dhana ya uwezekano wakuwepo watu wanaofanya mambo kwa kuitikia mwito wa mataifa makubwa lazima itizamwe, tuchukue tahadhari, turudi tuangalie nini historia inatuambia. Haijalishi maneno matamu kama ya Calhoun ambayo mtu ataya nena tumkatae mtu anayeteka kututendesha dhambi ya utengano, ambayo Mwl. Nyerere aliifananisha na kula nyama ya mtu. Andrew Jackson katika kitabu cha John Smith hapo juu Uk. Wa 25 alilimbia bunge la Marekani mwaka 1832;
The right of the people of the single state to absolve themselves at will, and without the consent of other states from their most solemn obligations and hazard the liberties and happiness of millions comprising this nation, cannot be acknowledged. That authority is believed to be totally repugnant, both to the principles upon which the General Government is constituted, and the object which is expressly formed to obtain.
Kwa maneno hayo hapo juu Andrew alilalamikia haki eti yakujitenga bila yakutaka hiari ya mataifa mengine ya muungano, utengano ambao utaathiri furaha ya mamilioni ya watu ya wamarekani, alisema dhana ya utengano ni ubatili.
Katika vita hivi vya kutaka kuigawanya Marekani, alipoingia bwana Taylor ambaye pia alikua ni rais wan chi hiyo alikua na haya yakusema ambayo nagfkiri huku tukitafakari ni namna gai tushgulikie matatizo ya muungano tuyaenzi haya;
Attachment to the union of States should be fostered in every America heart. For more than half a century during which kingdoms and empires have fallen, this union has stood unshaken… In my judgment its dissolution was greatest of calamities and to avert that should be the steady aim of every America. -The Adder’s Den ibd pp. 51, 52.
Taylor analeza muungano wao ulidumu kwa miaka ni sharti upiganiwe na kila mzalendo. Kabla hata wananchi hawaja ongea, viongozi wetu wanatuambia nini?
Nimatumaini yangu kuwa historia ya changamoto zilizo ukabili muungano wa mataifa ya Marekani inatufundisha mengi katika kuweza kupata mkondo halisi wa maadui wa muungano, binafsi dhana ya upandikizi inapokuwepo najifunza kuwa adui hatumbulishwi na chama cha siasa, anaweza akawa hapa au pale, au hata pote. Hebu tutumie historia hii kujichunguza. Tujiulize kwanini maadui wa Marekani na baadhi ya watu wasio wazalendo waliupinga muungano? Je hatuna watu hao leo na pi tuna uonaje muungano? Historia ujirudia!

Rugazia Aloys R
Mwanafunzi Chuo Kikuu
S.T Augustine Mwanza
aloysrugazia@yahoo.com.



 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom