Nono
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 1,536
- 643
Jambo la msingi ni kukaa mezani tu kama wadau wa mto nile. Nchi zote zenye vyanzo vya mto huu na wanaonufaika nao hadi mkiani washirikiane na waweke mipango shirikishi ya matumizi ya mto huu muhimu kwa masiha ya mamilioni ya watu. Sio uchaguzi wa Tanzania kuwa chanzo cha mto huu na wala sio wa misri kuwa mkiani mwa mto huu. Lakini pia sio haki ya misri kujimilikisha mto huu kwa mkataba wa kikoloni. Kulikuwa na umuhimu wa kudai uhuru ili tujipangie mambo yetu, ikiwa ni pamoja na maji. Ni wajibu wa nchi zotekushiriki katika kijipangia matumizi ya maji haya zote zikiwa kama mataifa huru.
Kwa vita hakuna atakayeshinda ila misri itajutia uamuzi wake kwa miaka mingi ijayo kama wakihamua kuingia vitani. By the way, watu wote wanaopigana mwishon huishia kwenye meza ya majadiliano, why not start with meza ya majadiliano?