Mgogoro wa madaktari ulivyoathiri wanafunzi wa sayansi

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,195
1,417
Wanajamii ma great thinker yangu ni machache. Leo nimewakuta watoto wangu na marafiki zao wakizungumza suala la kusoma PCB combination kubwa wanaochukua madaktari watarajiwa. Hofu imewashika hawaoni kama PCB inalipa baadae. Nawaomba wazazi wenzangu mchunguze athari ya mgogoro huu na hatua stahiki zichukuliwe mapema. Wale wenzetu mnaofanya tafiti liangalieni suala hili mwaka huu iwapo wanafunzi wa PCB wataongezeka au la. Pia athari hii inaweza kuwa kubwa baadae tusipokuwa waangalifu. Kaeni na watoto mjue mawazo yao ukizingatia masomo yenyewe ni ya muda mrefu, post graduate yake pia muda mrefu, shuluba nyingi nk. Mwisho watu wa HAKI ELIMU na wengine wenye mapenzi mema na TZ anzeni kutoa matangazo ya kusafisha hali ya hewa.
 
ndio taifa tunaloliandaa kwa sasa na shule zetu za kata na bado watu wanapiga siasa kila mahali mpaka kwenye suala nyeti kama afya za watu,na hii itachangia sana kupunguza 'motive' kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi(pcb) kwenda kufanya masomo ya udaktari kwani masomo ni magumu,muda ni mrefu mpaka umalize masomo hayo na ukimaliza maslahi kiduchu,vifaa duni ukigoma unafutiwa usajili nadhani katika hili hata uzalendo unaenda unapungua kwa kiasi kikubwa siasa zimetawala sna bongo
 
Back
Top Bottom