Mgogoro wa Dayosisi ya Pare umeishaje....!?

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Wadau, ningependa kufahamu ni utatuzi upi umefikiwa na Askofu mkuu wa kanisa la Kilutheri dhidi ya mgogoro ule wa Dayosisi ya Pare ambapo wenyewe wale wa Upareni walitaka waundiwe dayosisi yao n watenganishwe na Same kwa sababu wanawanyonya...

Je, wametenganishwa?
Aksanteni....
 
Aisee Mbonea, unajua nimekuwa najaribu kufanya utafiti kuhusu migogoro ya kidini (intra) hapa Tanzania. Kwa sasa nimelenga upande wa Kikristo (nafikiri nitafanya huku tu). Sasa hili swali ulilouliza nafikiri lina maana sana kwangu. Wacha nitege masikio nisikilizie wanasemaje wadau, labda nitapata source za uhakika hapa hapa.
 
Wala hupati jibu mambo ya kiroho waachie wanamaombi ,yale ya usuluhishi yaachie mahakama
 
Mgogoro wa dayosisi ya Pare na Mwanga unaelekea kwisha. Tarehe 11 Novemba walikuwa na sala ya pamoja. Kwa sasa inaelekea kuwa wauumini wa pande zote mbili wanasali kwa pamoja. Wachungaji wa pande zote wanashirikiana.
 
mbonea,
bora wananchi wa South Pare tupewe dayosisi yetu wenyewe. kuna wanasiasa wa North Pare(Mwanga)walikuwa wanaitumia dayosisi kwa manufaa ya kisiasa sasa alipopatikana askofu mpya ndiyo wakaona waazishe chokochoko za kumuondoa.
mara ya mwisho nilisikia Dr.Leonard Mtaita amekataa uteuzi wa kuchukua nafasi ya Askofu Mstaa Msangi. sijui nini kilimsukuma kukataa nafasi hiyo. nahisi Mtaita anatokea South Pare.
wananchi waliowengi wangependa kuwa na Pare moja yenye masikilizano. tatizo kuna wanasiasa wanaona ushawishi wao utapungua hilo likifanikiwa.
 
Back
Top Bottom