Mgogoro mkubwa waikumba CHADEMA kwenye kumpata mgombea ubunge Jimbo la Arumeru

Mi sioni tatizo kwa Nassary kuchangisha kwani hata baada ya kuchangisha aliwahi kusema yuko tayari kumpisha Dr. Slaa kama atataka kugombea na ataheshimu maamuzi ya chama. Nina wasiwasi na mtoa mada kuwa ni mmoja wa wanaomba usiku na mchana Chadema ipoteze Jimbo hilo. Nikija upande wa wagombea hakuna hata mmoja aliyejitokeza hadharani kulalamikia hilo, labda ritz angetueleza amekutana wapi na wagombea hao wa Chadema na walimlalamikia/walimweleza yeye akiwa na uhusiano gani nao? Je ni mamluki kutoka ccm? Je CDM hakuna viongozi? Hii inatupa kuwa kumbe CCM mna mamluki mliowatuma asanteni kwa taarifa.

asilimia mia moja nakuunga mkono. People's power!
 
Je, kutakuwa na makosa kama fedha zilizochangwa zilikuwa ni kwa ajili ya kusaidia CDM ishinde Arumeru Mashariki? Yaani, kama mgombea atakayepitishwa siyo Joshua fedha hizo zaweza kutumiwa kumsaidia mgombea mwingine kushinda?

Swali jingine ni la muhimu na ninaamini ipo hoja nzuri tu: Je CDM ina sera gani kuhusu kujichangishia fedha kusaidia kampeni yako bila kuvunja sheria ya matumizi ya wakati wa uchaguzi? Hili ni swali muhimu sana kwa vyama vyote vya siasa. Kwa mfano, Lowassa anapopita kila kona ya nchi je ni sehemu ya maandalizi ya kuja kugombea? Kama ni ndiyo, tunaweza kusema ameanza kampeni mapema? Je anapotoa misaada mbalimbali tunaweza kusema ni sehemu ya kujiwekea mazingira ya kugombea?

Swali hili la kwa Lowassa laweza kuwahusu watu wengine vile vile wenye kutaka kuja kugombea, ni wakati gani mwananchi anaweza kutoa misaada kwenye jimbo lake bila kuonekana ana malengo ya kugombea. Kwa mfano, binafsi ningepiga marufuku mwananchi yeyote aliyetoa msaada wwenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1 kugombea katika uchaguzi unaofuata. Itakuwa mshike mshike!
 
ya ritz anahaki ya kupost issue yoyote anayoona inafaha kwa mustakabali wa taifa letu,coz siasa ya tz kwa sasa ni ccm na chadema so kama kunaweakness chadema tuko huru kusema mapungufu yake, kama ccm pia tuko huru kuyasema,but kwa issue hii naona hakuna mapungufu kwa chadema, coz hata kwa wenzetu kwa mfano USA Barack obama B4 kuteuliwa na chama chake alifanya fundrising ya maana ili iweze kumsadia katika harakati zake za kuwa us pres,nt only that bt also hata siasa zetu zinahiyo hii kitu so fundrising sio mgogoro kwa chadema hizo ni harakaati za ccm kuwawagawa chadema waonekane kuwa na mgogoro kumbe sio,tumewabaini janja yao
 
eli arumeru kuna mgogoro mgombea mmoja katoa rushwa wengine wamepinga,cc ya chama imekodi ukumbi ikulu mzimu wa baba wa taifa ukawafumba macho waka shindwa kutegua kitendawili wakarudisha mpira golini kwao umenaswa na adui kipa kashika na msuli tunasubiria tarehe 1 mwezi wa 3.

chama kimoja kinachangisha wananchi.
chama kingine kinagawa hela kwa wananchi.
 
CHADEMA ni chama makini naamini hakuna mgogoro na suala hilo litapatiwa ufumbuzi bila kuzua mgogoro.
 
Kweli JF inakosa credibility ya u-great thinker kwa mtindo huu. We care much about dismissing people than dismissing arguments. Mtoa hoja sioni tatizo lake hapa hata kama ni declared anti-Chadema.Tujadili hoja. Hii kwama ni kweli ni ukweli usiopingika kuwa demokrasia imekandamizwa.Tukumbuke what is CHADEMA.Kutekeleza demokrasia ni wajibu wa CHADEMA wala sio option.Hakuwezekani watu kuanza kumchangia huyu jamaa kabla ya kupata ridhaa ya Chama kupeperusha bendera wakati kuna wengine anachuana nao,That's a clear bias and partiality.No democracy in that.Lazima tuwe wakweli na tusimamie ukweli sikuzote,otherwise hatutakuwa na tofauti na wenzetu wa magamba waliokunywa green blood ya uitikadi.This is wrong and should not repeat.
 
Kweli JF inakosa credibility ya u-great thinker kwa mtindo huu. We care much about dismissing people than dismissing arguments. Mtoa hoja sioni tatizo lake hapa hata kama ni declared anti-Chadema.Tujadili hoja. Hii kwama ni kweli ni ukweli usiopingika kuwa demokrasia imekandamizwa.Tukumbuke what is CHADEMA.Kutekeleza demokrasia ni wajibu wa CHADEMA wala sio option.Hakuwezekani watu kuanza kumchangia huyu jamaa kabla ya kupata ridhaa ya Chama kupeperusha bendera wakati kuna wengine anachuana nao,That's a clear bias and partiality.No democracy in that.Lazima tuwe wakweli na tusimamie ukweli sikuzote,otherwise hatutakuwa na tofauti na wenzetu wa magamba waliokunywa green blood ya uitikadi.This is wrong and should not repeat.

Wewe unaona haiwezekani ni maoni yako na sababu zako wengine tunaona inawezekana hakuna kosa kabisa hata nyumbani unapojiandaa kupanda shamba unaandaa mbegu hizo ni sababu zetu kwa hiyo tukubaliane kutokukubaliana lakini hakuna sababu ya kumshutumu mtu
 
huo mgogoro unautaka wewe ili iwe ngoma droo na MAGAMBA!? hilo sahau kabisa MAGAMBA hayana chao kabisa pale ARUMERU EAST bora wachapelapa mapema kama NGUNGURI.
 
Kwa hali halisi ilivyo arumeru NASARY bado anakubalika na walio wengi kupeperusha bendera ya CDM. Nafikiri huu haukuwa wakati wa kutafuta mgombea mwingine ambaye atatupa wakati mgumu kuanza kumtambulisha na muda wenyewe hauruhusu kubwa ni kukubaliana nae kwani jitihada za kuchukua jimbo alizionyesha 2010. Wagombea wenza toka CDM arumeru acheni kuingiza tofauti kwa wakati huu "SHIKAMANENI KUWAONDOA MAGAMBA KWANZA"
 
Usituchoshe na utetezi wako fyongo, jaribu kusoma kichwa cha 'thread' hii tena.

Hahahahahahaha Bwana "Gwalishenzi" its just eaten yours mzee watu kama ninyi huwa nakuiteni malofa (sorry though) mzee binafsi siongozwi na kichwa cha thread naongozwa na content and theme ninyi ndio wala ukiona heading chasema Raisi afumaniwa basi kwa kuwa si mchanganuaji una conclude kwa uwepesi wa heading kwamba atakuwa Raisi wa Nchi kumbe sivyo, Kajipange upya.
 
Je, kutakuwa na makosa kama fedha zilizochangwa zilikuwa ni kwa ajili ya kusaidia CDM ishinde Arumeru Mashariki? Yaani, kama mgombea atakayepitishwa siyo Joshua fedha hizo zaweza kutumiwa kumsaidia mgombea mwingine kushinda?

Swali jingine ni la muhimu na ninaamini ipo hoja nzuri tu: Je CDM ina sera gani kuhusu kujichangishia fedha kusaidia kampeni yako bila kuvunja sheria ya matumizi ya wakati wa uchaguzi? Hili ni swali muhimu sana kwa vyama vyote vya siasa. Kwa mfano, Lowassa anapopita kila kona ya nchi je ni sehemu ya maandalizi ya kuja kugombea? Kama ni ndiyo, tunaweza kusema ameanza kampeni mapema? Je anapotoa misaada mbalimbali tunaweza kusema ni sehemu ya kujiwekea mazingira ya kugombea?

Swali hili la kwa Lowassa laweza kuwahusu watu wengine vile vile wenye kutaka kuja kugombea, ni wakati gani mwananchi anaweza kutoa misaada kwenye jimbo lake bila kuonekana ana malengo ya kugombea. Kwa mfano, binafsi ningepiga marufuku mwananchi yeyote aliyetoa msaada wwenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1 kugombea katika uchaguzi unaofuata. Itakuwa mshike mshike!

Mi nadhani kwa swali la kwanza kama swala ni kusaidia mgombea yeyote basi na hao wengine nao walipaswa kufanya vivyo hivyo ila pawe na balance haiwezekani mkawa wa5 ati mmoja ndiye awe kinara wa michango tu kwa ajili ya kukidaidia Chama sasa ili hao wengine nao wafanye hivyo ndipo hapo swali lako la pili linapokuwa enforced juu ya Sera za Chama husika kama sera zinaruhusu au lah, manake naamini kama taratibu zinaruhusu hao wengine wasingeshindwa kufanya hivyo hata kama wasingefikia kiwango alichofikia huyo mwenzao; na huo mfano wako wa kwa Lowassa na wagombea wengine mi nadhani kwa kutumia mifano hiyo tutakuwa tunaongozwa na Hisia na Habari za kusikia manake hili Nassary na wenzie wao wameshatangaza kugombea huyo Lowassa ama wenzie wametangaza lini?? Manake kama tukitumia kigezo cha kutoa misaada nani ajuaye ya kesho???
 
chalii, unajua raia waengi hawajui siasa wanarukia tu mada,swala la kuchangisha pesa ni la kawaida katika siasa,pia anaweza akachangisha pesa kipindi cha kura za maoni akatoswa pia kama hatawavutia wapiga kura hivyo hiyo sio hoja ya kujadili. leteni hoja zenye mashiko tusihangaike na umbeya wa raia.
 
Msitake kila mada iwafariji, itakuwa ni ufinyu wa fikra na kukwepa ukweli na changamoto.

Suala siyo kutaka Chadema wafarijike au kukwepa changamoto, tunataka ritz atuambie alikutana na mgombea gani na wapi akamlamikia kama nani? Au ni yeye kwa mtazamo wake tu, ila kaamua tu kuwachafulia ili wasichaguliwe?
 
Sasa mbona umepost "mgogoro mkubwa WAIKUMBA...halafu maelezo ndani unasema "mgogoro UNAKINYEMELEA"? Hujui kuutunga hadithi?
Wanabodi..
Mgogoro mkubwa unakinyemelea Chadema wilayani Arumeru baadhi ya wananchama na wagombea waliochukuwa fomu za kuomba nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho.

Wagombea pamoja na wanachama wa chama hicho wanapinga kitendo cha mgombea mwenzao, Joshua Nassari kuitisha harambee na kuchangisha fedha kwa ajili uchaguzi huo wakati chama bado hakijapitisha jina la mgombea.

Nassari, aliitisha harambee ya kuchangisha fedha Arusha alipata takribani Sh10 milioni katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na Lema.

Wafuasi wa Chadema waliochukuwa fomu mbali na Nassari, ni Goodlove Temba, Yohane Kimuto, Rebbeca Mugwisha, Samwel Shami Sanjari na Anna Mgwilla.

Mchakato wa kuchukuwa fomu umefungwa juzi na jina la mgombea kujulikana Machi 3.
Wagombea wote kwa ujumla wamepinga kitendo hicho kuwa kimekiuka taratibu za chama.

Wagombea hao wamekwenda mbali zaidi na kusema hawapewi ushirikiano kama anaopewa mwenzao Nassari.
 
Mbona mbunge mmoja alipewa25elfu akaenda kupiga kampeni kwa kusaidiwa kwa harambee leo ni mbunge mbishi vizuri tu. Harambe haina tabu yeyote!
 
Wanajaribu kuangalia ni nani atakaye watoa aibu ya kuangukia pua kama ilivyokuwa Uzini na Igunga.
 

Mkuu hii habari imeandikwa na Mwananchi sijui kwanini povu linakutoka bure.Habari za Bwana Nassari kuchangisha fedha tulizisikia wote tena wengine humu jamvini walitoa ahadi ya kibao leo gazeti limefichua kwamba Nassari kabla hajapitishwa na chama chake tayari alishavuta fedha kibao kupitia harambee unadhani washindani wenzake ndani ya chama wametendewa haki ?.




Mwananchi.



Mkuu wangu hawakutendewa haki wana haki ya kulalamika hii ni sehemu ya demokrasia ambayo imo ndani ya katiba ya JMT.Ulitaka wakandamizwe halafu wanyamaze ?.



Wewe umeiona Mwananchi lakini bado haujaridhika unataka mleta asema alikoipata ha ha ha ha,sema haujaipenda habari yenyewe.



Habari za kuchangisha fedha Bwana Nassari kila mtu anajua ni kweli.Habari kwamba mchakato wa uchaguzi ndani ya cha CDM ulikuwa bado haujakamilika kila mtu anajua.Sasa naomba unijuze mnafiki ni nani kati yako wewe na ritz ?.



Amiliki, chama makini ni chama kinachotii sheria na kufuata taratibu na kanuni.Mtu makini na jasiri ni yule anayekubali makosa na kuyasahihisha na si kupindisha kama wewe unavyojitahidi.




Kama CDM taifa wamefikia hatua ya kumbeba mtu ambaye ana uwezo wa kujibeba mwenyewe siku ikitokea wakambeba mtu asiyebebeka ?.Nadhani ifike mahali CDM wafuate sheria,kanuni na taratibu ambazo nina hakika zipo isipokuwa zimewekwa pembeni.




Suala la uraia wa mgombea wa CCM limeingiaje hapa au ndiyo sehemu ya utetezi ha ha ha ha.



Mleta mada hana hizo tabia kabisa,sema kaleta habari usiyoipenda pengine hii ni sababu tosha ya kumbandika majina mabovu.





Nassari alisthubutu mwaka 2010 sawa lakini afuate taratibu za chama.

Lets be very fair kwenye hili na tuache ushabiki

1.Huu si mgogoro na wala si "mgogoro mkubwa", mwandishi kanyofoa habari iliyokuwa kwenye mwananchi ikisema "bundi ainyemelea cdm" ambayo haikupewa uzito na ufafanuzi ulitolewa na mwenye nyikti wa cdm wa wilaya. Mleta habari kaichakachua habari ile, inayonyesha huyu ni kada wa chama kingine na sio cdm

2. Wakati wa fund raising Nassari hakuwa Arusha alikuwa US, marafiki zake walifanya fund raising bila yeye kuwepo. So hakuitisha, na wala hawezi kulaumiwa kwa hilo. Besides, wagombea wote wamekumbushwa kufuata taratibu, so hii issue is none starter as a matter of fact

3.Haijalishi nani atapitishwa, resources zilizotolewa sio za Nassari ni za CDM, zitatumika kwa atakayepitishwa na CDM, hata kama sio Nassari mfano magari etc. Waliotoa hawakuwepo masharti kuwa ni kwa ajili ya Nassari peke yake na kama akipitishwa mtu mwingine watawithheld misaada/michango yao. So kwa mgombea kulalamika kwa chama kuwa na kianzio hata kabla mteule hajajulikana ni uzandiki!!

4.Hakuna kanuni ndani ya CDM AU CCM inayomzuia mtu kuchangisha fedha kwa ajili ya kujiandaa kugombea, mbona CCM wanachangia wagombea wao fedha za kuchukulia/kununulia fomu ya kugombea?.

5. Nassari ana mtaji wa kura nyingi alizopata kwenye uchaguzi uliopita, itakuwa rahisi kwa chama kumnadi na kumfanyia kampeni, anajua alishindwa wapi uchaguzi uliopita, arekebishe wapi etc. Ikumbukwe lengo la CDM ni kushinda, si kujaribu, kama ni kujaribu walijaribu 2010 wakashindwa. No time to waste.

6. Kuna aliyekuwa anagombea CCM akashindwa akahama haraka haraka kwenda CDM na kuchukua fomu, huyo asipopitishwa ataanza maneno kama haya ya kipuuzi. Watu wa hivyo ni hatari katika chama, sijui alikubaliwa vipi kuwa mwananchama for few hours na kuchukua fomu ya kugombea.

7. Binafsi naiona kazi ya kamati kuu ya cdm nyepesi sana, kumpitisha mgombea anayeweza kushinda, na sio atakayajaribu kushinda, CDM hawana hiyo luxury. Nassari amekamilika kwa kila kitu, so what else CDM need?
 
Ata hao wengine nao waitishe harambee waone kama hawatapata sapoti,ikitokea hivyo wajue hawakubaliki.
 
Nadhani hoja ya wahusika si swala la kuchangisha ama kupewa pesa kwa mwenzao hoja ni kwa nini tendo hilo lifanyike kabla Chama hakijampitisha mgombea??? Kama kweli kuna DEMOKRASIA kwa tendo hilo then the so called Democracy is raped......

Demokrasia ndani ya Chadema?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom