Mgogoro mkubwa waikumba CHADEMA kwenye kumpata mgombea ubunge Jimbo la Arumeru

kumbuken chama kinaendeshwa na watu na si malaika. Chama kuna wakati kinakosea, kinapokosea ni lazima kikosolewe. Hoja inajibu kwa hoja.
 
Wanabodi..
Mgogoro mkubwa unakinyemelea Chadema wilayani Arumeru baadhi ya wananchama na wagombea waliochukuwa fomu za kuomba nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho.

Wagombea pamoja na wanachama wa chama hicho wanapinga kitendo cha mgombea mwenzao, Joshua Nassari kuitisha harambee na kuchangisha fedha kwa ajili uchaguzi huo wakati chama bado hakijapitisha jina la mgombea.

Nassari, aliitisha harambee ya kuchangisha fedha Arusha alipata takribani Sh10 milioni katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na Lema.

Wafuasi wa Chadema waliochukuwa fomu mbali na Nassari, ni Goodlove Temba, Yohane Kimuto, Rebbeca Mugwisha, Samwel Shami Sanjari na Anna Mgwilla.

Mchakato wa kuchukuwa fomu umefungwa juzi na jina la mgombea kujulikana Machi 3.
Wagombea wote kwa ujumla wamepinga kitendo hicho kuwa kimekiuka taratibu za chama.

Wagombea hao wamekwenda mbali zaidi na kusema hawapewi ushirikiano kama anaopewa mwenzao Nassari.

nahakika huo sio mgogoro mkubwa, nadhan hapo umeongeza chumvi, tatizo hapo ni huyo mgombea kuchangisha hela kabla ya majibu ya uchaguzi ndan ya chama.
 
Source plz!!!!

Lakini nashangaa kwanini watu hawaelewi,kwani Nasari katoa rushwa au watu wamempa hela,nadhani watu wamempa hela kwaajili ya mapenzi yao kwake...mimi sishangai watu kumpa ushirikiano Nasari,ni kitu cha kawaida kama wao hawapati ushirikiano ina maana kuwa hawakubaliki kama wagombea...na watuambie kuwa hawapati ushirikiano toka kwa nani...kama ni kwa wanachama na wapenzi wa CDM ni kweli,wengi wanamtaka JOSHUA NASARI...may be kama hawapati ushirikiano kwa uongozi naweza nikasema kuwa hilo ni tatizo na halipaswi kuonekana....vinginevyo wewe mleta uzi tupe source na usilete siasa za CCM ukadhani na sisi ni watu wanaotamani madaraka kama huko kwa majambazi....

kama vile uliingia akilini mwangu,umewajibu kamanda.hao wengine wanaolalama wanatumika,c wanajua hata mmoja akipitishwa tu mfano Bw kimuto,inakula kwa chadema
 
Wanabodi..
Mgogoro mkubwa unakinyemelea Chadema wilayani Arumeru baadhi ya wananchama na wagombea waliochukuwa fomu za kuomba nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho.

Wagombea pamoja na wanachama wa chama hicho wanapinga kitendo cha mgombea mwenzao, Joshua Nassari kuitisha harambee na kuchangisha fedha kwa ajili uchaguzi huo wakati chama bado hakijapitisha jina la mgombea.

Nassari, aliitisha harambee ya kuchangisha fedha Arusha alipata takribani Sh10 milioni katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na Lema.

Wafuasi wa Chadema waliochukuwa fomu mbali na Nassari, ni Goodlove Temba, Yohane Kimuto, Rebbeca Mugwisha, Samwel Shami Sanjari na Anna Mgwilla.

Mchakato wa kuchukuwa fomu umefungwa juzi na jina la mgombea kujulikana Machi 3.
Wagombea wote kwa ujumla wamepinga kitendo hicho kuwa kimekiuka taratibu za chama.

Wagombea hao wamekwenda mbali zaidi na kusema hawapewi ushirikiano kama anaopewa mwenzao Nassari.

Weka picha mkuu
 
Migogoro katika jamii si tatizo, suala ni uzito wa hoja inayosababisha mgogoro. Kwa mtazamo wangu, unachokiita 'mgogoro ndani ya chadema arumeru' ni suala la kutengeneza ili kufurahisha nafsi yako na wenye mtazamo kama wako kiitikadi. Kila mtu ana haki ya kutafuta rasilimali zitakazo muwezesha kugombea. Hao wengine pia wanaweza kuitisha harambee wakati wowote wakiona inafaa kufanya hivyo, na pia wanahaki ya kumualika kiongozi yeyote wa CDM taifa. Kama hawakufanya hivyo ni hiari yao, labda kama walijaribu kuitisha harambee wakazuiwa na viongozi wa CDM waseme na wathibitishe ili sasa tuanze kujadili hoja hiyo.

Arumeru tunajua uwezo wa Nassari, alifanya vizuri uchaguzi uliopita na wananchi wengi wa jimbo la Arumeru mashariki wanamwamini na wako tayari kumuunga mkono. Nafahamu kuwa kule Mbuguni wako watu waliojitolea kuhakikisha kampeni za mgombea wa CDM zinafanikiwa kwa kutoa muda na rasilimali zingine. Kwao wanaamini mgombea sahihi wa kupeperusha bendera ya CDM ni Nassari.

Ccm jiandaeni taratibu kuwa chama pinzani. Msiwe na shingo ngumu, wananchi wanaendelea kuwakataa. Watu wa Arumeru hawatarudia makosa wakati huu.

Aiseee am not used to ila naomba uniruhusu kukuita lofa si tusi ni neno tu la kiungwana;

.......Eti huyu mleta mada anajifurahisha yeye na watu wa sampuli yake na yule wa MWANANCHI anamfurahisha nani?
.......Eti na wale wengine wana haki ya kufanya harambee je ni wakati gani HAKI hiyo inaanza kutumika??
.......Eti hao wengine wanaweza KUITISHA harambee kwa hiyo unakubali kuwa Joshua aliitisha harambee??
.......Eti kualika viongozi wa CDM Kitaifa kwa hiyo Lema pale alikuwa anawakilisha ngazi za juu na kwa hiyo unatuaminisha kuwa Nassari alishakuwa mteuke kabla???
.......Eti CCM wajiandae kuwa Chama cha upinzani hili ni kwa muktadha gani???? Ni wakati gani Chama tawala kinaitwa cha upinzani???

Mimi nadhani jaribu kuongea kidogo juu ya mambo mengi kuliko kuongea sana juu ya jambo dogo.......
 
Kimuto ashagombea TLP misimu mi3,atuambie kwa nini kamkimbia lyatonga? Na huyu ndo muanzisha choko choko,wanajamvi mnakumbuka aliyewaongoza wameru kupigana miaka 2 ilopita ndo huyu askari polisi mstaafu mpaka shamba la Kimaro likapigwa kiberiti akafa mmoja.kisa shamba,huwa anataka ubunge sana tu
 
Hapa sioni mgogoro kama huyu mpambe wa MAGAMBA anavyodai. Mimi naona Watu MAKINI wakifanya maandalizi ya AWALI kwa UMAKINI MKUBWA. Kuweka silaha za Vita tayari kwa Mashambulizi. Jambo hili linawatia KIWEWE wale ambao "taa zao hazina mafuta". Ole wao maana watati hautawangoja. VIVA CDM!!!
 
Source plz!!!!

Lakini nashangaa kwanini watu hawaelewi,kwani Nasari katoa rushwa au watu wamempa hela,nadhani watu wamempa hela kwaajili ya mapenzi yao kwake...mimi sishangai watu kumpa ushirikiano Nasari,ni kitu cha kawaida kama wao hawapati ushirikiano ina maana kuwa hawakubaliki kama wagombea...na watuambie kuwa hawapati ushirikiano toka kwa nani...kama ni kwa wanachama na wapenzi wa CDM ni kweli,wengi wanamtaka JOSHUA NASARI...may be kama hawapati ushirikiano kwa uongozi naweza nikasema kuwa hilo ni tatizo na halipaswi kuonekana....vinginevyo wewe mleta uzi tupe source na usilete siasa za CCM ukadhani na sisi ni watu wanaotamani madaraka kama huko kwa majambazi....

CCM yataka kumtosa mtoto wa Sumari Arumeru

soma kwa makini kipengele BUNDI CHADEMA, si unajua mwananchi=CDM kwa hiyo habari imefichwa kiaina
 
nahakika huo sio mgogoro mkubwa, nadhan hapo umeongeza chumvi, tatizo hapo ni huyo mgombea kuchangisha hela kabla ya majibu ya uchaguzi ndan ya chama.

Heshima kwako CPA nikubaliane na wewe kwa silimia za kutosha kuwa ni kweli mgogoro si mkubwa na hata mleta hoja Bwana Ritz hakuuweka katika namna ya kuonesha kuwa mgogoro ni kubwa ila sisi wachangiaji ndio tunaopelekea mgogoro huo kuonekana mkubwa. Na hilo tatizo ulilolisema haswa ndilo linaloleta haya yote manake kitendo hicho kimsingi kimekiuka taratibu za kiutendaji ndani ya Chama manake akiulizwa muhusika hizo hela alizopewa ni za nini jibu sijui litakuwa lipi. Manake kama CDM wangekuwa na Kampeni za ndani kutafuta mgombea walau justification zingepatikana.

Lakini CPA in politics ili mgogoro uwe mdogo pia lazma tuangalie tunatumia vigezo gani manake lile tatizo wewe unaloliona ni dogo ndilo wenzio watalitumia kama loophole kukuattack hivyo ili huu mgogoro uonekane mdogo wahusika hawana budi kulitolea tamko ili na wale wagombea wengine wajue si kwamba tu wametendewa haki bali wameona hiyo haki imetendeka.....
 
Wanabodi..
Mgogoro mkubwa unakinyemelea Chadema wilayani Arumeru baadhi ya wananchama na wagombea waliochukuwa fomu za kuomba nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho.

Wagombea pamoja na wanachama wa chama hicho wanapinga kitendo cha mgombea mwenzao, Joshua Nassari kuitisha harambee na kuchangisha fedha kwa ajili uchaguzi huo wakati chama bado hakijapitisha jina la mgombea.

Nassari, aliitisha harambee ya kuchangisha fedha Arusha alipata takribani Sh10 milioni katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na Lema.

Wafuasi wa Chadema waliochukuwa fomu mbali na Nassari, ni Goodlove Temba, Yohane Kimuto, Rebbeca Mugwisha, Samwel Shami Sanjari na Anna Mgwilla.

Mchakato wa kuchukuwa fomu umefungwa juzi na jina la mgombea kujulikana Machi 3.
Wagombea wote kwa ujumla wamepinga kitendo hicho kuwa kimekiuka taratibu za chama.

Wagombea hao wamekwenda mbali zaidi na kusema hawapewi ushirikiano kama anaopewa mwenzao Nassari.
Kama kawaida yako umeanza ule umbea wako.
 
Kufikiri kumbe nako taabu saana ehe! Nasari yeye kaonyesha nia ya kugombea ubunge na ili kutimiza nia hiyo akaamua kuitisha harambee. Hakuna cha ajabu hapo hata wao wana haki ya kuitisha harambee ili wakipita fedha hizo ziwasaidie kupiga kampeni na wawaite viongozi na watu wanaodhani watawasaidia kufanikisha harambee hiyo kama wakina Lema.

Wanadai hawapewi ushirikiano na viongozi. Katika nini? Kuitisha Harambee? Je wamepanga Harambee zao na kuwaita hao viongozi wakawakatalia?

Ingekua Nasari kahonga na akakamatwa na chama kisimchukulie hautua hapo tungesema lakini kwa hili tu, Please, give us a break!
 
JF ni jukwaa huru sio mali ya Chadema kila member ana haki ya kuanzisha thread cha msingi ni kufuata sheria na kanuni za JF.

Wewe mbona upo sehemu mbili upo kwa Lowassa halafu upo na Chadema.

Labda watu wangekuamini zaidi kama ungeweka na chanzo cha habari yenyewe. Kuweka tuu habari kama hivi, hata mimi naweza kupika habari na kuiweka hapa. JF ni jukwaa huru lakini nafikiri what matters most ni credibility ya habari zinazowekwa hapa. JF kuwa jukwaa huru haina maana kuwa unaweza kuanzisha thread za kupika ambazo ni rahisi wati ku-question their credibility.

Hili ni angalizo tuu.
 
Tatizo la Pro-Chadema JF ndio ili, badala ya kujibu hoja wanaleta porojo kwenye mambo ya msingi.

Mbona migogoro ya CCM, NCCR Mageuzi, CUF, mnaijadili kwa kasi ya ajabu, kubalini ukweli Arumeru kuna mgogoro.

Kwani lazima pro-chadema wachangie, simchangie nyie mapro ccm/cuf au wewe mpaka pro chadema wachangie ndo muwasho ukuache.
 
Wanabodi..
Mgogoro mkubwa unakinyemelea Chadema wilayani Arumeru baadhi ya wananchama na wagombea waliochukuwa fomu za kuomba nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho.

Wagombea pamoja na wanachama wa chama hicho wanapinga kitendo cha mgombea mwenzao, Joshua Nassari kuitisha harambee na kuchangisha fedha kwa ajili uchaguzi huo wakati chama bado hakijapitisha jina la mgombea.

Nassari, aliitisha harambee ya kuchangisha fedha Arusha alipata takribani Sh10 milioni katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na Lema.

Wafuasi wa Chadema waliochukuwa fomu mbali na Nassari, ni Goodlove Temba, Yohane Kimuto, Rebbeca Mugwisha, Samwel Shami Sanjari na Anna Mgwilla.

Mchakato wa kuchukuwa fomu umefungwa juzi na jina la mgombea kujulikana Machi 3.
Wagombea wote kwa ujumla wamepinga kitendo hicho kuwa kimekiuka taratibu za chama.

Wagombea hao wamekwenda mbali zaidi na kusema hawapewi ushirikiano kama anaopewa mwenzao Nassari.

akili yako hata kwenye kifuniko cha peni haijai!!!!!!kavu-e pichu ndo kazi yako kubwa iliyobaki!migogoro unaileta wewe???migogoro iko magambani (A+B)
 
Tatizo la Pro-Chadema JF ndio ili, badala ya kujibu hoja wanaleta porojo kwenye mambo ya msingi.

Mbona migogoro ya CCM, NCCR Mageuzi, CUF, mnaijadili kwa kasi ya ajabu, kubalini ukweli Arumeru kuna mgogoro.

lazima utakua mfuasi wa tendwalization theory

Heshima kwako CPA nikubaliane na wewe kwa silimia za kutosha kuwa ni kweli mgogoro si mkubwa na hata mleta hoja Bwana Ritz hakuuweka katika namna ya kuonesha kuwa mgogoro ni kubwa ila sisi wachangiaji ndio tunaopelekea mgogoro huo kuonekana mkubwa. Na hilo tatizo ulilolisema haswa ndilo linaloleta haya yote manake kitendo hicho kimsingi kimekiuka taratibu za kiutendaji ndani ya Chama manake akiulizwa muhusika hizo hela alizopewa ni za nini jibu sijui litakuwa lipi. Manake kama CDM wangekuwa na Kampeni za ndani kutafuta mgombea walau justification zingepatikana.

Lakini CPA in politics ili mgogoro uwe mdogo pia lazma tuangalie tunatumia vigezo gani manake lile tatizo wewe unaloliona ni dogo ndilo wenzio watalitumia kama loophole kukuattack hivyo ili huu mgogoro uonekane mdogo wahusika hawana budi kulitolea tamko ili na wale wagombea wengine wajue si kwamba tu wametendewa haki bali wameona hiyo haki imetendeka.....

hapo umeongea mkuu, inabidi uongozi utolee tamko ili kutoa utata juu la jambo hili! Siasa banaa, kama mpira, one mistake one goal. Ngoja tuwasikie wanasiasa wenyewe, wanasema nini na maneno yao matamu!
 
Labda watu wangekuamini zaidi kama ungeweka na chanzo cha habari yenyewe. Kuweka tuu habari kama hivi, hata mimi naweza kupika habari na kuiweka hapa. JF ni jukwaa huru lakini nafikiri what matters most ni credibility ya habari zinazowekwa hapa. JF kuwa jukwaa huru haina maana kuwa unaweza kuanzisha thread za kupika ambazo ni rahisi wati ku-question their credibility.

Hili ni angalizo tuu.

EMT,
Naona mapenzi na Chadema yamekujaa utaki kukubali kabisa, naona leo umeamua kuomba source...MWANANCHI FEB 27 2012..

Vipi hapo umekubali au na hiyo source huitaki.
 
Wakati mwingine ni bora ukakaa kimya au ukatafakari jambo kabla hujaposti.ulucho kiposti hakina ukweli wowote mana harambee hiyo haikufanywa na JOSHUA ilifanywa na marafiki zake na wapenzi wa chadema wakati huwo Joshua alikuwa marekani.
 
Back
Top Bottom