Mkuu Kukutia Ole.
Mkuu wangu bandiko lako limenifurahisha hakika JF inakosa magreat thinker kama wewe.Mleta hoja kaeleza vizuri badala ya kujibiwa kaishia kuambulia kebehi kwakuwa kaleta habari zisizopendwa kusomwa/kusikiwa na wanajamvi wengi.
Yalikuwa ni makosa makubwa sana kutendwa na Bwana Nassari na wote walioshiriki kuchangisha fedha kwaajili ya kampeni wakati chama kikiwa katika mchakato wa kumtafuta mgombea.Ni kweli Bwana Nassari ana nguvu kuliko wagombea wengine lakini hiyo haimpi haki ya kuchangisha fedha kabla hajateuliwa na chama chake.Pamoja na makosa yalifanywa bado hakuna dalili za mgogoro kwakuwa wanachama waliokandamizwa hawana nguvu/mvuto mkubwa katika jamii sana sana wanaweza kutumika.
CDM makao makuu ni vyema wakaweka utaratibu ili hali kama hii isitokee tena.Walioshiriki kuchangisha fedha kabla ya mchakato wa uchaguzi ndani ya chama haujakamilika wapewe karipio kali.
Heshima kwako Mkuu Ngongo.
Tatizo Pro-Chadema JF hawataki kukosolewa hawajui kama ukitaka kusonga mbele lazima ukubali kukosolewa.
........za kenge uchanganye na za kunguru!!
Tatizo la Pro-Chadema JF ndio ili, badala ya kujibu hoja wanaleta porojo kwenye mambo ya msingi.
Mbona migogoro ya CCM, NCCR Mageuzi, CUF, mnaijadili kwa kasi ya ajabu, kubalini ukweli Arumeru kuna mgogoro.
Wanabodi..
Mgogoro mkubwa unakinyemelea Chadema wilayani Arumeru baadhi ya wananchama na wagombea waliochukuwa fomu za kuomba nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho.
Wagombea pamoja na wanachama wa chama hicho wanapinga kitendo cha mgombea mwenzao, Joshua Nassari kuitisha harambee na kuchangisha fedha kwa ajili uchaguzi huo wakati chama bado hakijapitisha jina la mgombea.
Nassari, aliitisha harambee ya kuchangisha fedha Arusha alipata takribani Sh10 milioni katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na Lema.
Wafuasi wa Chadema waliochukuwa fomu mbali na Nassari, ni Goodlove Temba, Yohane Kimuto, Rebbeca Mugwisha, Samwel Shami Sanjari na Anna Mgwilla.
Mchakato wa kuchukuwa fomu umefungwa juzi na jina la mgombea kujulikana Machi 3.
Wagombea wote kwa ujumla wamepinga kitendo hicho kuwa kimekiuka taratibu za chama.
Wagombea hao wamekwenda mbali zaidi na kusema hawapewi ushirikiano kama anaopewa mwenzao Nassari.
wanabodi..
Mgogoro mkubwa unakinyemelea chadema wilayani arumeru baadhi ya wananchama na wagombea waliochukuwa fomu za kuomba nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho.
Wagombea pamoja na wanachama wa chama hicho wanapinga kitendo cha mgombea mwenzao, joshua nassari kuitisha harambee na kuchangisha fedha kwa ajili uchaguzi huo wakati chama bado hakijapitisha jina la mgombea.
Nassari, aliitisha harambee ya kuchangisha fedha arusha alipata takribani sh10 milioni katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na lema.
Wafuasi wa chadema waliochukuwa fomu mbali na nassari, ni goodlove temba, yohane kimuto, rebbeca mugwisha, samwel shami sanjari na anna mgwilla.
Mchakato wa kuchukuwa fomu umefungwa juzi na jina la mgombea kujulikana machi 3.
Wagombea wote kwa ujumla wamepinga kitendo hicho kuwa kimekiuka taratibu za chama.
Wagombea hao wamekwenda mbali zaidi na kusema hawapewi ushirikiano kama anaopewa mwenzao nassari.
JF thinker never buy utumbo like this
try again later
Trashedhoto:hoto:hoto:hoto:hoto:hoto::A S-coffee::A S-coffee:
Chanzo tafadhari.
Sasa kama hawapewi ushirikiano ndani ya chama na wao wamekwishaona hilo wanasubiri nini kwa mfano?????
Hivi wakishaanza kuwaza ubunge akili huwa hazichambui mambo kwa uyakinifu????
Kusoma hawajui may be.......na picha pia hawaoni???
me nmesoma pia gazeti la mwananchi tar 26 hii habari ipo pia. lakini mtoa mada naye aseme kama ameipata wp
Wewe ni mnafiki sana
Masaburi at work. Nani kawazuia na wao kuchangisha! Ni mgogoro ambao hata wao wenyewe hawaujui ni kitu inataka kutengenezwa na CCM lakini haitafanikiwa. Chadema ni Chama Makini.
Mkuu hizi habari nimekua nazisikia kwamba Nasari anabebwa na CDM Taifa. Kuna haja uongozi taifa,mkoa na wilaya wakutane haraka na kuondoa tofauti zinazoanza kujitokeza. Kadri CDM inavyopata umarufu migongano kama hii itajitokeza sana. Uongozi ngazi zote wawe tayari kutumia
busara kumaliza tofauti kama hizi.
Naona suala la uraia limekwisha sasa Ritz aka Yasoda aamua kuhamia issues za chademahoto:
Na mleta uzi unaoneka una asili ya umbea,majungu,ushambenga,unoko,usengenyaji,nk...ati mgogoro mkubwa,nani kakwambia bwana? Acha kuleta tabia zako za ajabu hapa.
ao waliochukua fomu wawe na hekima kijana nasari aldhubutu 2010 na bado anania njema ao waliofunguka muda uhu watulize mzukax wamwache chali wetu akapambane.kama na wenyewe wana jeuri waitishe haraaambeeee.
Mkuu hii habari imeandikwa na Mwananchi sijui kwanini povu linakutoka bure.Habari za Bwana Nassari kuchangisha fedha tulizisikia wote tena wengine humu jamvini walitoa ahadi ya kibao leo gazeti limefichua kwamba Nassari kabla hajapitishwa na chama chake tayari alishavuta fedha kibao kupitia harambee unadhani washindani wenzake ndani ya chama wametendewa haki ?.
Mwananchi.
Mkuu wangu hawakutendewa haki wana haki ya kulalamika hii ni sehemu ya demokrasia ambayo imo ndani ya katiba ya JMT.Ulitaka wakandamizwe halafu wanyamaze ?.
Wewe umeiona Mwananchi lakini bado haujaridhika unataka mleta asema alikoipata ha ha ha ha,sema haujaipenda habari yenyewe.
Habari za kuchangisha fedha Bwana Nassari kila mtu anajua ni kweli.Habari kwamba mchakato wa uchaguzi ndani ya cha CDM ulikuwa bado haujakamilika kila mtu anajua.Sasa naomba unijuze mnafiki ni nani kati yako wewe na ritz ?.
Amiliki, chama makini ni chama kinachotii sheria na kufuata taratibu na kanuni.Mtu makini na jasiri ni yule anayekubali makosa na kuyasahihisha na si kupindisha kama wewe unavyojitahidi.
Kama CDM taifa wamefikia hatua ya kumbeba mtu ambaye ana uwezo wa kujibeba mwenyewe siku ikitokea wakambeba mtu asiyebebeka ?.Nadhani ifike mahali CDM wafuate sheria,kanuni na taratibu ambazo nina hakika zipo isipokuwa zimewekwa pembeni.
Suala la uraia wa mgombea wa CCM limeingiaje hapa au ndiyo sehemu ya utetezi ha ha ha ha.
Mleta mada hana hizo tabia kabisa,sema kaleta habari usiyoipenda pengine hii ni sababu tosha ya kumbandika majina mabovu.
Nassari alisthubutu mwaka 2010 sawa lakini afuate taratibu za chama.
Kama mtu umeamua kuingia kwenye kuomba fursa ya kugombea ubunge moja ni pamoja na kujiandaa,kujipima upepo kama kuna watu watakuunga mkono ikiwemo hata kuitisha harambee,si kosa kabisa alifanya vizuri,kama atapitishwa tayari atakuwa na mtaji wa kujiwezesha kufika maeneo mbalimbali
Sasa kama hawapewi ushirikiano ndani ya chama na wao wamekwishaona hilo wanasubiri nini kwa mfano?????
Hivi wakishaanza kuwaza ubunge akili huwa hazichambui mambo kwa uyakinifu????
Kusoma hawajui may be.......na picha pia hawaoni???