MGOGORO: Malumbano ya UVCCM, Viongozi wastaafu na Hatima ya CCM

Hivi Pengo ni nani nchi hii ukiondoa uongozi wake ndani ya RC.

Ni Mtanzania wa kawaida, lakini ukimpima kwa integrity yake yuko juu,ni kiongozi wa dhehebu la kikatoliki, ni mmoja kati ya wanaharakati wazalendo wa kitanzania, ni mwanachama mwaminifu wa TANU.nI MMOJA KATI YA WATANZANIA WANAOLILIA MAISHA BORA LAKINI HAYAPATIKANI KUTOKANA NA SERA NA UONGOZI MBOVU WA CCM
 
Kila papa ana sharubu hivyo wakati mwingine ndani ya nyumba anakosa nani aitwe baba wa familia. Ukiona hivyo hiyo familia imeparanganyika. Na ukiona mtindo wa kila hoja kutolewa tamko ujue mambo hayaendi sawia.

Si kila jambo linapoongelewa lipokewe kwa mtazamo hasi na kwamba linamlenga mtu au raisi. Matendo na matukio yanayojiri ndo hukumu tosha mpaka hawa vijana wanakurupuka (sijui kwa kutumwa au kupenda) kutoa shutuma na kejeli (matusi) ilhali wakubwa zao walengwa wamekaa kimya.

Ndio hao hao tusipoangalia watakuja chukua uongozi wa nchi in the near future Unategemea nini hapo?
 
UVCCM hawana mamlaka kutung'oa-Chiligati

*Makamba asema hayo ni maoni ya vijana
*Lowassa ahoji nani asiyeona uchumi ulivyo?

Na John Daniel

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Maponduzi (NEC) Itikadi na Uenezi, Bw. John Chiligati amesema
licha ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuwa na haki ya kutoa maoni, lakini hawana mamlaka ya kuiondoa sekretarieti madarakani.

Wakati Bw. Chiligati akitoa kauli hiyo, wajumbe wenzake wa sekretarieti waliotakiwa kuachia ngazi kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa 'kumsaidia' mwenyekiti wametofautina kuhusu kauli hiyo huku wakishindwa kuzungumzia kwa uwazi wito huo wa vijana.

Jana gazeti hili liliwakaririwa vuoa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ukiitaka sekretarieti ya chama hicho kujizulu kabla umoja huo haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani Pwani, Bw. Abdallah Ulega wakati akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa humo, huku akisisitiza kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita, na kuwa ndiyo imekuwa ikitoa siri kwa chama cha upinzani cha CHADEMA.

Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.

Akizungumza na Majira jana Bw. Chiligati alisema kimsingi vijana hao wametumia uhuru wao ndani ya chama kutoa maoni yao na kwamba haoni sababu ya hatua hiyo kusumbua vichwa vya watu kwa kuwa ni jambo la kawaida kikatiba.

"Ni haki yao kutoa maoni, sioni cha ajabu hapo, vijana wana haki ya kuzungumza na kutoa maoni yao kwa uhuru kabisa.

"Lakini Secretarieti inachaguliwa na NEC na tunawajibika kwa NEC kupitia Kamati Kuu, hao waliotuchagua ndio wana mamlaka ya kutuondoa, lakini hilo haliwakatazi vijana kutoa maoni," alisema Bw. Chiligati.

Alipoulizwa changamoto waliyopata na iwapo wanajiandaa kuwasilisha mapendekezo yao kwenye vikao vya juu kutokana na wito wa UVCCM hakuwa tayari kutoa majibu ya moja kwa moja badala yake alisisitiza kuwa hayo ni maoni ya vijana.

"Nimesema hayo ni maoni ya vijana na wana haki ya kuyatoa," alisistiza Bw. Chiligati bila kufafanua.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba alisema licha ya kuheshimu uhuru wa kutoa maoni lakini haamini kama yaliyoandikwa katika vyombo vya habari ndiyo yaliyozungumzwa na UVCCM mkoa wa Pwani.

"Hayo ndio maoni ya vijana, wamekaa kwenye baraza lao na wakaona hivyo. Hayo ndio maoni yao mimi sina cha kusema," alisema Bw. Makamba.

Alipotakiwa kujibu iwapo katiba, kanuni na taratibu za CCM zinatoa nafasi kwa umoja huo kuondoa secretarieti iwapo imeshindwa kutimiza wajibu wake alisema;

"Ni maoni yao, lakini pia sina hakika kama yaliyoandikwa yako sawa sawa," alisema Bw. Makamba bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Alipoulizwa hatua atakazochukua kama Mtendaji Mkuu wa CCM kuhusu wito huo wa UVCCM alisema yeye hawezi kujitetea kupitia magazeti na kusisitiza kuwa hayo ni maoni ya vijana.

"Siwezi kufanya kazi ya kujitetea kwenye magazeti, wao ni vijana wa CCM, wamekaa kwenye baraza lao wakasema, sasa unataka nisema nini? alihoji Bw. Makamba na kuongeza, "Nasema hivyo ndivyo walivyoona. wajumbe wengine wa sekretarieti hiyo hawakupatikana kutoa maoni yao kwa simu zao zilikuwa zinaita bila majibu.

Mbali na sekretarieti, vijana hao waliwashambulia mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye wakisema kauli zao za kukikosoa chama hazina lengo zuri bali ni njia tu ya kutafuta urais 2015

Akizungumzia suala hilo, Bw. Lowassa ambaye pia alionywa na vijana hao kutoa maoni nje ya vikao wakati anayo nafasi ya kukutana na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Jakaya Kikwete, alisema maoni yake kuhusu uchumi hayana sababu ya kusubiri vikao.

"Nilikuwa vijijini kwenye ziara sijasoma magazeti, lakini wewe nikikuuliza hali ya uchumi utasema kuwa ni nzuri?Nani asiyejua kuwa kuna hali ngumu ya uchumi! Hata bei ya nyanya imependa hilo nalo tusubiri vikao? alihoji Bw. Lowassa.

Alisema kama mtu anataka kuwania urais mwaka 2015 hawezi kuanza kampeni kwa sasa kwa kuwa kufanya hivyo ni kutoa nafasi ya kushughulikiwa na kuchafuliwa na maadui. Bw. Sumaye hakupatikana jana kwenye simu yake.

Majira ilipomtafuta Makamu Mwenyekiti Taifa wa CCM, Bw. Pius Msekwa ili kuzungumzia wito huo wa UVCCM, alisema hawezi kusema lolote kwa kuwa hayo ni maoni ya vijana na kila mmoja anayo haki ya kutoa maoni yake.

"Hayo ni maoni ya vijana, sasa unataka nitoe maoni gani?" alihoji Bw. Msekwa.
 
KAZI KWELI KWELI
WAENDE TU LOLIONDO WAKAYAMALIZE MASHETAN YAO
BENO R U THR??WAHI BANA KWA BABU

UVCCM wataka kumtimua Makamba

*Wamo pia Membe, Chiligati na Makala
*Yadai wameshindwa kumshauri mwenyekiti

Na Edmund Mihale, Bagamoyo

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka sekretarieti ya chama hicho kujizulu kabla umoja huo
haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.

Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa wa Pwani jana, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani humo, Bw. Abdallah Ulega alisema kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita.

"Katika uchaguzi uliopita tulishinda kwa kupata asilimia 61 ya kura zilizopigwa ukilinganisha na mwaka 2005, ukijiuliza ni kweli CCM imepoteza imani kwa wananchi kwa kiasi hicho jibu linakuja kuwa sekretarieti haikuwajibika ipasavyo, hivyo tunasema kama wamechoka waondoke kama hawataondoka lazima waondolewe hawafai," alisema Bw Ulega.

Alisema kuwa watu walimo katika sekretarieti hiyo ndiyo wanatoa siri kwa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) na imeshindwa kumshauri na kumtetea rais katika mambo mengi ya msingi hadi anaposimama na kujitetea mwenyewe.

Mkutano huo ulihudhuliwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na wenyeviti umoja huo kutoka katika Mikoa ya Kagera, Lindi Kigoma, wabunge kadhaa na Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la jumuiya hiyo, Bw. Ridhiwan Kikwete.

Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.

Mbalio na sekreterieti hiyo, Bw. Ulega alisema kuwa watu wengi walio katika serikali wanatakiwa kujibu hoja za dhidi ya serikali akutokana na vitengo vyao na si lazima wasubiri Rais Kikwete kujibu hoja hizo.

"Kuna watu wa kujibu hoja, katika mfumuko wa bei yuko gavana na watu wa kumsaidia amewekewa, kuna naibu gavana na wakurugenzi wengine, shughuli yake ni kujibu hoja ya mfumuko wa bei lakini anainuka rais na kujibu hoja hiyo wao wanafanya nini.

"Labda watuambie kama wanamilikiwa na bwana wengine na kumuacha rais akihangaika pekee yake, naomba niseme tena bila kumung'unya, kama wanahisi hawezi kazi wakae pembeni na kama wanatumukia mabwana wawili watachanika msamba," alisema Bw. Ulega.

Alisema ni kitendo cha kushangaza kwa Mawaziri Wakuu Wastaafu, Bw. Edward Lowassa na Bw. Fredrick Sumaye kushindwa kukutana na rais na kumpa ushauri, na kukimblia katika magazeti na kutoa shutma.

"Hawa watu ni mwaziri wakuu wastaafu, wanaweza kufanya ahadi kwa dakika 30 tu wakaonana na rais lakini wanakimbilia katika magazeti na kutoa kauli zinazohatarisha amani na kukivuruga chama," alisema.

Alisema Bw. Lowassa ni Waziri Mkuu mstaafu, mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, alipaswa kuwa mwangalifu katika kauli zake anazotoa hususani kutaka mishahara ipande huku akijua kuwa hali ya uchumi si nzuri.

Bw. Ulega alisema kauli hizo zimelenga kutaka urais mwaka 2015, jambo ambalo kwa sasa wamechelewa kwa kuwa liko mikononi mwa mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete kuwa kuwa ndiye anayemjua rais wa 2015.

Alisema viongozi hao wameacha utaratibu mzuri wa chama hicho kutoa maoni yao kupitia vikao na kutoa shutuma zao kupitia magazeti wakidhani wanakikomoa chama, nchi itaendelea kusonga mbele na kuwapa pole wale wanaodhani rais lazima atoke kaskazini.

"Kama wanataka urais wasubiri muda wachuke fomu na kuwashawishi wajumbe wawachague lakini kwa kumtukana mwenyekiti hawatapata kamwe kwa kuwa yeye ndiye anayejua ni nani muadilifu, hivyo wasiharibu nchi kwa maslahi yao. Wao wameshiba na sasa wamevimbiwa watauache na sisi tule kama wao.

"Mimi nasema hapa simung'unyi maneno tuziogope sana fedha zao, mimi sijala hata shilingi moja ya mtu na sihitaji kufanya hivyo," alisema.
 
Safi sana maadui wanapogombana wao kwa wao. Msema kweli ndani ya ccm ni adui wa ccm!!
 
Dawa ya matatizo ya CCM ni moja tu - fukuza Mwenyekiti basi! Hizi nyingine zooooooooooooooooooote ni longolongo.
 
Sijaelewa mantiki ya kuingiza CDM katika hili. Fafanua tafadhali.
 
Hawa watoto hawana radhi ya wazee wao yaani wanakashifu hadi viongozi wa dini na viongozi wengine wastaafu. Ningekuwa kiongozi mkuu wa CCM nisha BAN hawa miezi 18 ama zile ban zinaishiaga tu kwa akina Nyimbo? Unajua hakuna kosa kubw akama hili la vijana kukosa na kutothamini radhi ya wazee. Pumbafu sana mitoto hii isiyo na nidhamu hata kidogo
 
Hivi Pengo ni nani nchi hii ukiondoa uongozi wake ndani ya RC.

Huyu shekh ana udini kuliko member wote jf, yaani hajasoma thread aone inaeleza nini anakimbilia kuhoji Pengo ni nani. Naomba mjaribu kuangalia post zake, ukisikia masnitch ndo kama huyu.
 
"Nilikuwa vijijini kwenye ziara sijasoma magazeti, lakini wewe nikikuuliza hali ya uchumi utasema kuwa ni nzuri?Nani asiyejua kuwa kuna hali ngumu ya uchumi! Hata bei ya nyanya imependa hilo nalo tusubiri vikao? alihoji Bw. Lowassa.

Hivi haya maneno hayana ukweli au ndio kuvaa miwani za mbao na kujipendekeza!
 
UVCCM wa sasa ni vijana wasio na heshima na adabu, hawajui nafazi zao wala wajibu wao kama uvccm. mara kadhaa nimewaona wakijipeleka kwenye vyombo vya habari na kutoa taarifa zilizojaa upupu na unafiki. Nafikiri utoto wa siasa ndiyo unawafanya wajisahau
 
*Makamba asema hayo ni maoni ya vijana
*Lowassa ahoji nani asiyeona uchumi ulivyo?

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Maponduzi (NEC) Itikadi na Uenezi, Bw. John Chiligati amesema
licha ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuwa na haki ya kutoa maoni, lakini hawana mamlaka ya kuiondoa sekretarieti madarakani.

Wakati Bw. Chiligati akitoa kauli hiyo, wajumbe wenzake wa sekretarieti waliotakiwa kuachia ngazi kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa 'kumsaidia' mwenyekiti wametofautina kuhusu kauli hiyo huku wakishindwa kuzungumzia kwa uwazi wito huo wa vijana.

Jana gazeti hili liliwakaririwa vuoa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ukiitaka sekretarieti ya chama hicho kujizulu kabla umoja huo haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani Pwani, Bw. Abdallah Ulega wakati akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa humo, huku akisisitiza kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita, na kuwa ndiyo imekuwa ikitoa siri kwa chama cha upinzani cha CHADEMA.

Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.

Akizungumza na Majira jana Bw. Chiligati alisema kimsingi vijana hao wametumia uhuru wao ndani ya chama kutoa maoni yao na kwamba haoni sababu ya hatua hiyo kusumbua vichwa vya watu kwa kuwa ni jambo la kawaida kikatiba.

"Ni haki yao kutoa maoni, sioni cha ajabu hapo, vijana wana haki ya kuzungumza na kutoa maoni yao kwa uhuru kabisa.

"Lakini Secretarieti inachaguliwa na NEC na tunawajibika kwa NEC kupitia Kamati Kuu, hao waliotuchagua ndio wana mamlaka ya kutuondoa, lakini hilo haliwakatazi vijana kutoa maoni," alisema Bw. Chiligati.

Alipoulizwa changamoto waliyopata na iwapo wanajiandaa kuwasilisha mapendekezo yao kwenye vikao vya juu kutokana na wito wa UVCCM hakuwa tayari kutoa majibu ya moja kwa moja badala yake alisisitiza kuwa hayo ni maoni ya vijana.

"Nimesema hayo ni maoni ya vijana na wana haki ya kuyatoa," alisistiza Bw. Chiligati bila kufafanua.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba alisema licha ya kuheshimu uhuru wa kutoa maoni lakini haamini kama yaliyoandikwa katika vyombo vya habari ndiyo yaliyozungumzwa na UVCCM mkoa wa Pwani.

"Hayo ndio maoni ya vijana, wamekaa kwenye baraza lao na wakaona hivyo. Hayo ndio maoni yao mimi sina cha kusema," alisema Bw. Makamba.

Alipotakiwa kujibu iwapo katiba, kanuni na taratibu za CCM zinatoa nafasi kwa umoja huo kuondoa secretarieti iwapo imeshindwa kutimiza wajibu wake alisema;

"Ni maoni yao, lakini pia sina hakika kama yaliyoandikwa yako sawa sawa," alisema Bw. Makamba bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Alipoulizwa hatua atakazochukua kama Mtendaji Mkuu wa CCM kuhusu wito huo wa UVCCM alisema yeye hawezi kujitetea kupitia magazeti na kusisitiza kuwa hayo ni maoni ya vijana.

"Siwezi kufanya kazi ya kujitetea kwenye magazeti, wao ni vijana wa CCM, wamekaa kwenye baraza lao wakasema, sasa unataka nisema nini? alihoji Bw. Makamba na kuongeza, "Nasema hivyo ndivyo walivyoona. wajumbe wengine wa sekretarieti hiyo hawakupatikana kutoa maoni yao kwa simu zao zilikuwa zinaita bila majibu.

Mbali na sekretarieti, vijana hao waliwashambulia mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye wakisema kauli zao za kukikosoa chama hazina lengo zuri bali ni njia tu ya kutafuta urais 2015

Akizungumzia suala hilo, Bw. Lowassa ambaye pia alionywa na vijana hao kutoa maoni nje ya vikao wakati anayo nafasi ya kukutana na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Jakaya Kikwete, alisema maoni yake kuhusu uchumi hayana sababu ya kusubiri vikao.

"Nilikuwa vijijini kwenye ziara sijasoma magazeti, lakini wewe nikikuuliza hali ya uchumi utasema kuwa ni nzuri?Nani asiyejua kuwa kuna hali ngumu ya uchumi! Hata bei ya nyanya imependa hilo nalo tusubiri vikao? alihoji Bw. Lowassa.

Alisema kama mtu anataka kuwania urais mwaka 2015 hawezi kuanza kampeni kwa sasa kwa kuwa kufanya hivyo ni kutoa nafasi ya kushughulikiwa na kuchafuliwa na maadui. Bw. Sumaye hakupatikana jana kwenye simu yake.

Majira ilipomtafuta Makamu Mwenyekiti Taifa wa CCM, Bw. Pius Msekwa ili kuzungumzia wito huo wa UVCCM, alisema hawezi kusema lolote kwa kuwa hayo ni maoni ya vijana na kila mmoja anayo haki ya kutoa maoni yake.

"Hayo ni maoni ya vijana, sasa unataka nitoe maoni gani?" alihoji Bw. Msekwa.
 
Ni Mtanzania wa kawaida, lakini ukimpima kwa integrity yake yuko juu,ni kiongozi wa dhehebu la kikatoliki, ni mmoja kati ya wanaharakati wazalendo wa kitanzania, ni mwanachama mwaminifu wa TANU.nI MMOJA KATI YA WATANZANIA WANAOLILIA MAISHA BORA LAKINI HAYAPATIKANI KUTOKANA NA SERA NA UONGOZI MBOVU WA CCM

Malizia basi kusema kuwa ni mfadhili mkuu na mwanachama mwaminifu wa Chadema
 
Back
Top Bottom