Umesema kweli kabisa na sasa wasome alama za nyakati kuwa watanzania hawadanganyiki.Habari ya wametumwa na wakubwa sio jambo la kuuliza ni la wazi kabisa,, na kitendo cha baadhi ya viongozi walioko madarakani kusema eti vijana wana uhuru wa kutoa maoni yao ni wazi kabisa wanatekeleza tu maagizo kutoka kwa wakubwa. Cha kushangaza eti vijana wana uhuru wa kutoa mawazo yao, ila kina Sumaye na wengine kama Sita wakitaka kusema wamfuate raisi ama watumie vikao vya chama... Haiingii akilini na inaboa... wanataka kuficha nini??? Serikali hii imejaa visasi, chuki, ufisadi na uchafu mwiiiiingi!!
Nawashukuru sana wachangiaji wa JF,maana hii ni demokrasia mpaka hapa nimeelewa kuwa wachangiaji tupo pamoja katika kuboresha.MJUE PAULO MAKONDA ( PART 2A):teeth:
Kama nilvyosema kuwa, katika medani ya siasa ni lazima uwe makini sana katika uchambuzi na sio kujitokeza na kusema,kwa maana kuwa"Kijana huyu alisema kuwa SEKRETARIETI YA UVCCM TAIFA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI IJIUZULU"………………Hapa kiuhalisia ni kuwa kada huyu bado ni mchanga wa siasa kwani bado anachanganya mambo kwani UVCCM inaongozwa na kanuni moja ambayo imewekewa ibara ya kwanza hadi mwisho, pia katika UVCCM kunatoa wajumbe kwenda sekretariet ya CCM Taifa,yaani katibu Mkuu wa UVCCM au Naibu Katibu Mkuu, si kweli kuwa sekretariet ipo kwenye structure ya UVCCM au UVCCM ina kamati ya utekelezaji kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa ambayo inaongoza mipango ya jumuiya hiyo ya kila siku
Pia kamati ya utekelezaji hupendekezwa na wajumbe wa baraza hilo la Taifa na si kata, iweje leo mjumbe wa mkutano mkuu toka kata CCM kwenda Wilaya aje na maamuzi haya?bila yeye kupitia vikao vyake vya kata?.mbona wajumbe wa kata hawana taarifa?.
Halafu ujumbe wa kata yake haujathibitishwa,binafsi ninamshauri kuwa kama ngazi ya kata inaweza kushinikiza Taifa,hii ni hatari!wajumbe wa kata zote Tanzania wenye nafasi kama yake,wakitoa matamko kama yake,ina tija kwa taifa?
Lengo si kumuumbua,ni kumshauri tu kuwa CCM ina vijana wa aina zote,yeye asitake kuburuza watu kwa maandalizi yake ya Uenyekiti wa UVCCM Taifa.
Binafsi nadhani kuwa, kwakuwa amekiuka kanuni za chama kama wenzake za kuongelea kwenye media,naye ajiuzulu!.nani msemaji wa kata yake ya Rau? Kada huyu amepotoka.
Paul makonda anaposema kuwa wale wanatetewa na mafisadi,je,ana uthibitisho gani kuwa ni kweli?kama naye hakuwa mmoja wa kundi la mafisadi hao. Anataka kuuaminisha umma kuwa wale wanaomsomesha na kumfadhili wamemtuma?Nina ushahidi wa kutosha kuwa anatumika kupitia matamko yake.
MAMBO MAZURI ALIYOWAHI KUFANYA PAULO MAKONDA
Bila kusema yaliyopo,kijana huyu aliwahi kuandaa makongamano ya dini na kualika wanaomfadhili waongee na jamii katika maandalizi ya urais wa mwaka 2015,hasa Moshi-Ushirika,Institute of Social Work pamoja na Stefano Moshi University.
Aliweza kuwa mchapakazi katika mambo ya jamii hali hata asipotumwa,ni dhahiri kuwa akishauriwa na akashaurika atakuwa kijana safi kwa miaka ijayo nje ya jumuia na chama tawala.Aache kutumika vibaya na kujitafutia maadui katika jamii.
MIPANGO YAKE YA MUDA MREFU.
Kutumia media kujitangaza ili kutimiza ndoto zake za kisiasa UVCCM, na kiuchumi katika kuelekea urais wa mwaka 2015-2025.Niseme kuwa atafute njia mbadala ya kuwahudumia watanzani kwani hana uwezo katika nyanja ya siasa na uongozi.
"kila kijana anaweza kuwa na urafiki au undugu na kiongozi yeyote wa kitaifa,tusifike mahali tukawa mbuzi wa kafara kwa maslahi ya viongozi hawa………."anda:

Umri unamsumbua huyo mzee... Anamdanganya nani? Hata mtoto wa primary analiona kama anabisha amuulize Lowassa watoto walivyo na vision now days, aliulizwa swali akashindwa kulijibu mpaka sasa hivi!
mjiniKatibu Mkuu,
Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM),
Morogoro Road/Opposite to Lumumba street,
S.L.P 0000,
DAR ES SALAAM.
YAH:HATIMA YA UVCCM NA SIASA ZA CCM/TANZANIA.
Nimesoma habari mbali mbali kuhusu Maazimio ya kikao cha Baraza kuu la UVCCM wiki iliyopita mjini Dodoma,nina haya yafuatayo:-
1.Hivi Hussein Bashe ni mtu sahihi kwa sifa na uwezo wa kuisaidia UVCCM itimize majukumu yake kwa CCM na Watanzania? Hii ina maana mtu huyu awe mwenyekiti wa kamati ya kukusanya na kupendekeza Muundo na mahitaji ya UVCCM ya sasa na ijayo kufuatia kauli ya mhe.Rais kikwete kuwa CCM lazima ijivue Gamba ,UVCCM mnaona Hussein Bashe anaweza kusimamia mabadiliko tarajiwa? Biashara na Siasa zitenganishwe UVCCM, pia Wasomali hawawezi kutusaidia kuiendeleza nchi yetu; vinginevyo UVCCM ibinafishwe kwa wageni kama viongozi wa sasa mmeshindwa.
2.UVCCM kuweni mbele katika hoja nzito za kitaifa badala ya kutaka kuzuia demokrasia ya uhuru wa mawazo/kujieleza kwa kuwataka wanaCCM wasiongelee mambo ya taifa lao mpaka vikao rasmi vipitishe,hii sio sahihi hata Wamarekani wanajadili nini maslahi ya nchi yao kuingia kijeshi nchini Libya na jana spika wa Bunge la Marekani Mhe.John A.Boehner amemwandikia Barua Rais wake Mhe.Barrack Obama awajulishe Wamarekani malengo halisi ya kwenda Libya na kwa vipi watapima mafanikio hayo(www.nytimes.com/Boehner presses Obama on Libya Action) maana Majeshi yameingia Libya kwa Azimio la UN na ARAB LEAGUE sio Bunge lao.
3.UVCCM isiige siasa za Afrika kusini kati ANCYL vs ANC au JULIUS MALEMA vs JACOB ZUMA
kwa kufanya hivyo mtavuruga CCM maana vijana ndio tegemeo la CCM,na nyinyi hamtakuwa salama pia.
4.UVCCM Jaribuni kuwa watafiti ili muweze kumshauri m/kiti wa CCM Taifa hasa masuala muhimu nchini kwa vijana yakiwemo (a).Mgawo wa umeme unavyoua Biashara ndogo ndogo(hizi ni ajira za vijana),
(b)Udhaifu wa management ktk vyuo vikuu ulivyokero kwa wanafunzi,(c )Kuongeza "competences" kwa Graduates maana kwa sasa wengine wanahitimu wakiwa bado dhaifu kutokana na mfumuko wa vyuo vikuu nchini,(d).Ombeni mfumko wa bei uwe controlled maana hela ina kosa thamani kama zimbabwe,etc.
Nakutakia kazi njema,
Ndimi
Mussa Mnyeti-0787 330518,
Mwanachama wa UVCCM/CCM.
Sina hakika kama kimefanyika kitu kwa vijana rejesha nidhamuKaribu kwenye mjadala huu ambao unalenga kujitathimini kwa vijana juu ya heshima yao kwa wazee. Mjadala huu utakuwa unarejea matukio mbali mbali ambayo yamefanywa na vijana.Kuanza na naweka orodha a matukio ya wanasias vijana dhidi ya viongonzi wao.
Nitaanza kwa kutoa mifano:-
1. Mwampamba na Sonza walipokuwa Chadema walikuwa wanatuhumiwa kuwavunjia heshima viongozi (wazee wa chama) wa chama chao mitandaoni....na inasemakama mpaka sasa wanafanya hivyo.
2. Nape wa CCM inasemakana aliwahi kutoa kauli ya kuudhi na kuvunja heshima kwa wazee...kuwa wao wanasubiri kufa tu...!
3. Kijana (sina hakika kama ni mwanasiasa sana) aliwahi kumpiga kibao Mzee Mwinyi(Rais mstaafu) hadharani akipinga maelezo ya Mzee Mwinyi.
4. Vijana wa UVCCM waliwahi pia kuwatukana viongozi wa chama chao pia. Ushahidi huu hapa chini
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uvccm-viongozi-wastaafu-na-hatima-ya-ccm.html
5. Pia na Mbunge wa Arusha Mh. Lema naye inasemekana anawavunjia heshima wazee wa CCM
6. Serukamba Mbunge wa Kigoma aliwatukana wazee kwa vijana waliokuwa bungeni na waliokuwa wanasikiliza kupitia runinga na redio...pale alipotamka tusi kwa lugha a kiingereza.
7. Mh. Lissu aliwahi pia kutamka kuwa ...neno...SILLY....bungeni...hilo pia ni kuwa wavunjia heshima wazee kwa vijana...
8. mweshimiwa waziri Kijana Mkaa wa mia aliwahi kusema anaongea na mwenye mbwa wala haongei na mbwa...huko huko bungeni(kama nimekosea nisahihisheni).
8. Orodha ni ndefu....ila kabla sijahau pia...kuna na suala la Makonda, Paul kumkwida Jaji Warioba.
Sasa kwa matukio haya na mifano mingine....huko mitaani. Vijana tumeangukia/wameangukia wapi mpaka sasa wanasahau umuhimu wa utamaduni wetu watanzania wa kuwaheshimu wazee. Ni nini kifanyike ili kurudisha heshima ya vijana kwa wazee?
Karibu kwenye mjadala.
SOURCE:VIJANA NA HESHIMA KWA WAZEE: Tumebadili utamaduni wetu wa Kitanzania...!?