Mgogoro kati ya wakata miwa na wazungu - illovo

BABA KEREN

Member
Jun 5, 2011
29
12
Jana tarehe 19 August 2011 Katika Kiwanda cha Kuzalisha Sukari cha Kilombero kwa sasa kinajulikana ILLOVO kulikuwa na Hali ya sintofahamu na iliyopelekea Wakata Miwa kuchukua Maamuzi Magumu ya kuacha Kazi Wote kwa kutokukubaliana na Uongozi wa kiwanda hicho, Wakata miwa hao ambao wangi wao hutoka katika Mikoa ya IRINGA na MBEYA pamoja na RUKWA walifikia uamuzi huo baada ya makubaliano kati yao na Bodi ya Kiwanda hicho kutokuwa Mazuri, Katika malalamiko yao wameelezea kufanyishwa kazi ngumu na manyanyaso ya hali ya juu na Ubaguzi uliokithiri kati ya wa Raia wa Kigeni na Wenyeji wa Inchi hii ya Tanzania,
Aidha katika kuthibisha kutokujaliwa kwao wakata miwa hao walinipeleka hadi sehemu ambazo wao wanalala na kunionyesha Mkataba unaotumika kwa shughuli za ukataji miwa,angalia zaidi picha Number moja hadi ya Mwisho na baadhi ya File niliyoweka hapo chini naamini utaelewa zaidi kilichojiri Kiwandani Hapo,Kazi ni Kwako Mwana Jamii.Nawasilisha! Hati ya Mshahara kwa Kibarua wa Illovo 19 August 2011.JPG Kiwanda Cha Sukari Kilombero (Illovo) 19 August 2011.JPG Hiki ndicho Kitanda cha Kibarua wa Kiwanda cha Illovo 19 August 2011.JPG Vibarua wakipata Ushauri toka kwa FFU 19 August 2011.JPG Vibarua wakitoka nje ya Kiwanda cha Illovo 19 August 2011.JPG Sehemu ya Kwanza ya Mkataba wa Kibarua.JPG Sehemu ya Pili ya Mkataba wa Kibarua.JPG
 

Attachments

  • Vibarua wakitoka nje ya Kiwanda 19 August 2011.JPG
    Vibarua wakitoka nje ya Kiwanda 19 August 2011.JPG
    120 KB · Views: 52
  • Morogoro.docx
    15 KB · Views: 101
Back
Top Bottom