Mgogoro Hazina, BoT, serikalini; hakuna malipo!

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Kuna taarifa kwamba mgogoro kati ya BoT na Hazina umesababisha kukwama kwa malipo serikalini kwa zaidi ya wiki tatu sasa,na baadhi ya maeneo hata mishahara hawajalipwa.

Wanasema baadhi ya watendaji wa serikali wanaambiwa kuna mgogoro kati ya BoT na hazina na wengine wanaambiwa ni kudorora kwa uchumi. Wakati uchumi una dorora wakubwa wa TICS wanafanya upuuzi na kusababisha kusinyaa kwa huduma za makontena kwa siku mbili bandarini wiki iliyopita na kusababisha hasara kubwa.

Mambo mengine ni mengi yanayoumiza uchumi na serikali imelala usingizi kila mtu akipigania kitumbua chake na wahalifu wakiendelea kuitesa serikali bila kufanywa lolote. Wameiba na wanatumia fedha za wizi kuendesha siasa na kuwatisha watawala hata Rais, ambaye anaogopa kuwachukulia hatua. Wananunua watendaji wakiwamo wa dola, wananunua haki hata mahakamani, wananunua haki hata katika mitandao na vyombo vya habari, watanunua hata familia zetu (kama hawajaanza) maana njaa inasababisha utu kutoweka.

Inauma sana.
 
Watanzania wajifunze kuishi na uchaguzi wao... kama serikali yao iko tayari kutumia bilioni 61 kununua majengo matatu Marekani na imehalalishwa kwa sababu kuna matarajio ya matokeo bora huko mbeleni well.. hakuna wa kulalamika.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Collapse of the system!

Kawaida ukiona kunazuka migogoro kwenye taasisi nyeti namna hiyo ujue pana shida...na shida yenyewe si ndogo!
Hapo ujue kuna mbishano wa payments, ambapo upande mmoja utakuwa unatumia taaluma, wakati upande mwingine ukitaka kupiga deal!
Ndullu na Mkullo mmesafiri?
 
hawa wakubwa wakati wanajichukulia midola hazina sijui hawakujuwa kama siku zitakwisha, hiyo ya kununua mijengo mitatu kwa mihela yote hiyo nayo ni vichekesho, sasa kama huko mbeleni matokeo kama hayatakuwa bora...... tuna wakati mgumu kiuchumi halafu watu bado wanacheza kamali.
 
Na kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yangu serikalini, safari hii nimeshuhudia serikali ikizitumia Wizara na idara zake Exchequer hewa. Mfano mwezi uliopita wizara yetu ilitumiwa exchequer ya Operating Cost (OC) lakini ilipoaingizwa kwenye system (mtaandao) ya malipo na baadae malipo yakaanza kufanyika kwa kutumia hiyo exchequer then Voucher list kupelekwa hazina baadhi ya malipo yaliondolewa na hazina na kubakisha malipo ya mshahara tu kwa kile walichodai kuwa hakuna pesa BoT.

Sasa cha kujiulliza kama pesa hakuna BoT ni kwa nini walituma Exchequer hewa?
 
Watanzania wajifunze kuishi na uchaguzi wao... kama serikali yao iko tayari kutumia bilioni 61 kununua majengo matatu Marekani na imehalalishwa kwa sababu kuna matarajio ya matokeo bora huko mbeleni well.. hakuna wa kulalamika.

Kununua jengo hilo ni moja, lakini jengo la ghorofa 6 New York kwa nchi inayoomba hata vyandarua vya kuzuia mbu ni maajabu ya Mussa! $24 million ni mansion ya nguvu hata kwa viwango vya wauza mafuta -Saudia. Na gharama za kuendesha jengo kama hilo ni kubwa sana. Hivi tuna shughuli gani kubwa hivyo huko New York zaidi ya kupitisha kibakuli kiasi kwamba tunahitaji jengo la ghorofa 6?

Tumeambia miradi mingi ya barabara imesimama kwa sababu hakuna hela.Mishahara imekwamba. Na kama haitoshi wafadhili nao wamepunguza hela walizo ahidi. Mfano Uiengereza wanapunguza msaada kwenye budget yetu by 30%. Tukumbuke Uiengereza ndio wanatoa kiasi kikubwa kwenye bajeti kuu ya serikali kuliko mfadhili mwingine yoyote. Wanachangia takribani 30% ya hela yote inayotelewa na wafadhili (combined). Kwa hiyo kama wanapunguza ni kwamba tutaumia vibaya. Kwa hali hii inakuwaje tununue majengo ya ki-celebrity?
 
Serikali ya CCM ni kiziwi!

Ahsante luten kanal Dr Dr Dr Dr Dr J Kikwete kwa kuimalza CCM,utaondoka nayo 2015
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Honestly naomba Mr David Cameron atangaze "kupata msaada lazima mkubali ushoga". Najua it's a thorny issue politically, and they will decide not to. Then tuanze kujitegemea tuone kama watanunua majumba huko nje.
 
@MtamaMchungu, If I had my way ningemwambia David Camoron aoengezee moja, wimbo wa Taifa utakuwa ni ule wa Malkia na atakayekataa hatopata hata cent moja. Hapo utaona wakubwa wanaachana ni hii scandal ya kuwapogia magoti wawekezaji ili walipe kodi? Na ile habari ya 5 yrs tax-holiday nina hakika ingepotea! Please Camoron toa ultimatum.
 
Ni ukweli mtupu umeandika kwa hasira, bila shaka mshahara hujapata au ulichelewa sana. Acha tunyooke tupate akili
 
Kununua jengo hilo ni moja, lakini jengo la ghorofa 6 New York kwa nchi inayoomba hata vyandarua vya kuzuia mbu ni maajabu ya Mussa! $24 million ni mansion ya nguvu hata kwa viwango vya wauza mafuta -Saudia. Na gharama za kuendesha jengo kama hilo ni kubwa sana. Hivi tuna shughuli gani kubwa hivyo huko New York zaidi ya kupitisha kibakuli kiasi kwamba tunahitaji jengo la ghorofa 6?

Tumeambia miradi mingi ya barabara imesimama kwa sababu hakuna hela.Mishahara imekwamba. Na kama haitoshi wafadhili nao wamepunguza hela walizo ahidi. Mfano Uiengereza wanapunguza msaada kwenye budget yetu by 30%. Tukumbuke Uiengereza ndio wanatoa kiasi kikubwa kwenye bajeti kuu ya serikali kuliko mfadhili mwingine yoyote. Wanachangia takribani 30% ya hela yote inayotelewa na wafadhili (combined). Kwa hiyo kama wanapunguza ni kwamba tutaumia vibaya. Kwa hali hii inakuwaje tununue majengo ya ki-celebrity?

Kila kinachofanyika ni kibaya mbele za watu, nadhani makubwa tena ya hatari yaja upesi...,
 
Honestly naomba Mr David Cameron atangaze "kupata msaada lazima mkubali ushoga". Najua it's a thorny issue politically, and they will decide not to. Then tuanze kujitegemea tuone kama watanunua majumba huko nje.

Mkuu kumbuka hatuna pakutokea kwa serikali hii.Hiliyokwenda Uk KUOMBA CHENJI YA DILI LA RADA..
Tayari serika la uk imekata msaada yake wa pesa mpka tukubaliane na ushoga.
Lazima serikali itakubali.
 
Kwa hali ilivyo ni hakika nchi imefilisika. Miradi mingi ya miundo mbinu imekwama, serikali inadaiwa na wakandarasi wa ndani zaidi ya 500bn.

Kinachokera ni Vasco Da Gama kuendelea kula good time ulaya, achilia mbali matumizi mabaya ya fedha serikalini.
 
Honestly naomba Mr David Cameron atangaze "kupata msaada lazima mkubali ushoga". Najua it's a thorny issue politically, and they will decide not to. Then tuanze kujitegemea tuone kama watanunua majumba huko nje.

Nyerere alisema, " Mtu mwenye akili, akikupa ushauri wa kipumbavu na wewe ukaufuata/ukaukubali, ATAKUDHARAU sana."
 
Watanzania wajifunze kuishi na uchaguzi wao... kama serikali yao iko tayari kutumia bilioni 61 kununua majengo matatu Marekani na imehalalishwa kwa sababu kuna matarajio ya matokeo bora huko mbeleni well.. hakuna wa kulalamika.
Mzee Mwanakijiji, hili halina tatizo as long as tulibudget hiyo pesa na katika budgeting, hizo ndizo priorities tulizojiwekea!.

Wachumi wa Tanzania wamegundua kuweka priority kwenye huduma za afya na elimu kutaboresha life expectancy ya Watanzania ambao tunazaliana sana, hivyo bora kutelekeza huduma za afya na elimu ili Watanzania wengi zaidi waishie darasa la saba na baada ya hapo waishi kidogo tuu na kujifia ili kumaintain reasonable population density ambayo itakuwa accomodatable kwa nchi washitiri kuendelea kutufadhili!.

Kitendo cha Tanzania kununua jumba la haja hapo NY kunaiondoa Tanzania kwenye kundi la nchi masikini wa kutupwa mpaka kugeuka real estate investor huko US, angalau sasa TTB, CRDB, TIC etc watafungua US branches!.
 
Honestly naomba Mr David Cameron atangaze "kupata msaada lazima mkubali ushoga". Najua it's a thorny issue politically, and they will decide not to. Then tuanze kujitegemea tuone kama watanunua majumba huko nje.

Nyerere alisema, " Mtu mwenye akili, akikupa ushauri wa kipumbavu na wewe ukaufuata/ukaukubali, ATAKUDHARAU sana."
 
uko sahihi MMM kwamba tujifunze kuishi na uchaguzi wetu. Ni kweli tupu!
 
Back
Top Bottom