Mgodi wa tulawaka sasa kufungwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Audax Mutiganzi, Bukoba


KAMPUNI ya kuchimba dhahabu ya African Barrick Gold (ABG), inatarajia kufunga eneo la Mgodi wa Tulawaka ulioko wilayani Biharamulo mkoani Kagera, katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja kuanzia sasa.


Kauli hiyo ilisemwa na Mwanasheria wa ABG, Godson Killiza, wakati wa kikao cha pamoja cha na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti ya mkoa huo.


Alisema Barrick ikishafunga sehemu ya mgodi huo, wataukabidhi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Idara ya Misitu na Nyuki wautumie kama msitu wa hifadhi.


Alisema kampuni hiyo imeanza hatua za awali za kufunga eneo la mgodi, ambazo ni pamoja na kuotesha miti katika maeneo ya Kijiji cha Mavota kinachozunguka mgodi huo, kusawazisha ardhi na kuotesha mimea na nyasi za asili.


Alisema kampuni hiyo ina mkakati mkubwa wa kuyashirikisha makundi mbalimbali kabla ya kuufunga mgodi kwa njia ya vikao.


Alisema kampuni hiyo tayari imeshafanya vikao na ujumbe wa Wizara ya Maji, Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Wizara ya Nishati na Madini, Baraza la Usimamizi wa Mazingira na Idara ya Misitu na Nyuki.


Alisema kampuni hiyo inaendelea na kuandaa vikao zaidi vya kujadili mikakati ya kuufunga mgodi huo.


Aidha, alisema watakutana na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Wizara ya Fedha na Uchumi, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), waandishi wa habari na wananchi wanaozunguka mgodi wa Tulawaka.


Alisema baada ya kufungwa eneo la mgodi huo, miundombinu na mali nyingine, ukiwamo uwanja wa ndege, mashine saba za kuzalisha umeme, eneo la makazi, karakana kubwa mbili, makontena na majengo ya utawala vyote vitakabidhiwa kwa Serikali.


Alisema Barrick inataka kuliacha eneo la mgodi likiwa na uasili wake.


Alisema mashimo yote yaliyokuwa yamechimbwa katika eneo la mgodi yatafunikwa.


Aidha, alimhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, kuwa kabla ya kufunika mashimo hayo kampuni itahakikisha inafanya ukaguzi ndani ya mashimo hayo kwa ajili ya wavamizi wa machimbo wasifunikwe.

Chanzo: Mtanzania
 
Dhahabu imesiaha lazima wafunge tu. wameshatuibia na kutukamua hadi damu, asante zao kwa kutuachia mashimo.
 

Nimechanganyikiwa... Niliweka post kuwa Mr. Rweyemamu amechaguliwa kuwa New GM wa Tulawaka... all of a sudden; Wanaanza

kusema WANAIFUNGA HAKUNA DHAHABU au DHAHABU IPO ni CONTRACT ISSUE? ni ya BARRICK GOLD wana MIGODI 4

na unasikia wana MPANGO WA KUUZA... very COMPLICATED... THEY TOY WITH OUR WEALTH like LITTLE KIDS...
 
Kidumu chama cha mapinduzi! Wamekwapua madini miaka mingapi?
 

Nimechanganyikiwa... Niliweka post kuwa Mr. Rweyemamu amechaguliwa kuwa New GM wa Tulawaka... all of a sudden; Wanaanza

kusema WANAIFUNGA HAKUNA DHAHABU au DHAHABU IPO ni CONTRACT ISSUE? ni ya BARRICK GOLD wana MIGODI 4

na unasikia wana MPANGO WA KUUZA... very COMPLICATED... THEY TOY WITH OUR WEALTH like LITTLE KIDS...

Hapa panachanganya mkuu.. Rweyemamu atakuwa anasimamia kuziba mashimo na kupanda miti? "Does not sound right"
 
Naona wafunge na kule Nyamongo na kwingineko, hata hiyo gesi iishe tu maana badala ya kutuletea utajiri lazima itatuletea mafarakano bora tuendelee zetu na TANESCO yetu
 

Nimechanganyikiwa... Niliweka post kuwa Mr. Rweyemamu amechaguliwa kuwa New GM wa Tulawaka... all of a sudden; Wanaanza

kusema WANAIFUNGA HAKUNA DHAHABU au DHAHABU IPO ni CONTRACT ISSUE? ni ya BARRICK GOLD wana MIGODI 4

na unasikia wana MPANGO WA KUUZA... very COMPLICATED... THEY TOY WITH OUR WEALTH like LITTLE KIDS...

Wanajua sasa hivi hakuna kitu Tulawaka, ni mashimo tupu ndio maana wamamteua Mtanzania awe meneja wa hayo mashimo. Wao wanataka dhahabu, mashimo ni juu yenu watanzania!
 
sasa hebu pata picha ya vijiji vinavyozunguka huo mgodi unaofungwa mwakani ndio utajua kama Watanzania ni wajinga kiasi gani
 
Uongozi wa Tulawaka imekanusha taarifa hizo.Wamesema mgodi HAUTOFUNGWA.fUNGUA ATTACHMENT HIYO.
 

Attachments

  • TULAWAKA KUTOFUNGWA.pdf
    350.8 KB · Views: 100
dhahabu imekwisha, sasa tufanye tathmini ya uchimbaji, je umeleta faida gani kwa taifa/mtz? hasara gani? uwiano wa faida na hasara then tukae chini tutafakari matokeo
 
Uongozi wa Tulawaka imekanusha taarifa hizo.Wamesema mgodi HAUTOFUNGWA.fUNGUA ATTACHMENT HIYO.

mkuu wamekanusha kuufunga mgodi in 6 months time (feb 2013) wao wanasema their current reserves ni mpk oct 2013 and so the fact 'tulawaka is going down' is still a live.. "mgodi HAUTOFUNGWA" only if new reserves'll be found
 
Wenye mamlaka wangekuwa na akili, wangewaachia wachimbaji wadogo wafanye shughuli za uchimbaji, at least na sisi wananchi tungepata angalau kidogo, lakini kutokana na tamaa zao za kifisi, wakawakalibisha hawa mambweha, mwisho wa siku tunaambulia 'kufukia mashimo'....
 
baada ya madini kuisha au kubaki kidogo. je mtanzania amenufaikaje?, na raslimari za nchi
 
Mgodi umeshauzwa kwa Serikali ya Tanzania ; wanauendesha mdogo mdogo ....... Akija mwekezaji mwingine atauziwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom