Mgodi wa Tulawaka kufungwa

FrankGM,
Jiji la Johannesburg limejengwa kutoka na dhahabu ya Afrika kusini. Unaweza kuniambia hata siku moja tunaweza kuilinganisha miji yetu Kahama, Mwanza na Shinyanga na Johannesburg? Acha bwana!
 
hayo kwa kweli ni maneno ya wafanya biashara huo mgodi sio rahisi kufungwa soon, utafungwa labda kwenye 2011-12, sasa hiyo ni lugha ya kujifanya wanapata hasara ili waingie kwenye misamaha ya kodi,
sio siri katika Tanzania sidhani kama palishawahi kuwa na mgodi kama wa Tulawaka, ni mgodi mdogo sana lakini ndio mgodi unaotoa dhahabu nyingi kuliko yote TZ, can u imagine, huo mgodi ndio uliojenga mgodi wa buzwagi ambao ndio utakua mgodi mkubwa kuliko yote Tz,
pamoja na plan za kufunga huo mgodi, ukifika katika vijiji ambavyo vimeuzunguka huo mgodi utashangaa maana kuna umaskini wa kutupwa,
hii nchi nadhani viongozi wetu sio wazima kunako ubongo
 
Basi na wawe wastaarabu kidogo. Kabla ya kuondoka angalau kwanza wafukie hayo makorongo waliotuachia. Wanategemea hata hiyo kazi tufanye sisi?
Wanatarajia kufunga baada ya miaka miwili, kwahiyo wanachofanya sasa ni maandalizi ambayo yanajumuisha ufukiaji wa mashimo kisha kupanda miti na kuhakikisha mazingira yamekuwa kama walivyoyakuta.
Hilo lisikutie shaka, hoja nzito iliyopo ni kuwa dhahabu imekwisha na hatujanufaika ilivyopasa
 
Heri yaishe. Hatimaye Mafisadi watakosa cha kufisadi na akina Barrick wataondoka na hapo tutapata viongozi wa kweli kweli na siyo hawa wanaowekwa na akina RA.
Kwa hilo la kuondoka Barrick ndugu yangu sema jingine hawawezi kuondoka leo wala kesho.
Pale Bulyanhulu hazina iliyopo bado kama miaka hamsini (50yrs)
 
Back
Top Bottom