Mgodi wa Sh 7 bilioni, wauzwa kwa Sh900m (makubwa haya Tanzania)

ramson34

Senior Member
Oct 29, 2009
109
4
Send to a friend Wednesday, 12 May 2010 05:39 0diggsdigg

Ramadhan Semtawa

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe amesema kamati yake imeanza mchakato wa kuchunguza tuhuma za ufisadi katika mgodi wa madini wa Nyanza Mines ulio Kigoma Kusini unaodaiwa kuuzwa kwa Sh90milioni tofauti na thamani yake halisi ya Sh7.8 bilioni.

Tuhuma hizo zimeibuka katika kipindi ambacho Watanzania bado hawajapata majibu kuhusu kashfa nyingine ya mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ambao uliuzwa kwa bei poa ya Sh700 milioni kwa kampuni ya Tanpower Resources Limited ambayo ilimudu kulipia Sh70 milioni tu.

Tayari serikali imetangaza kuurejesha mgodi huo mikononi mwake.

Lakini Zitto jana aliibuka na kashfa nyingine ya uuzaji wa mali za umma kwa bei poa wakati alipoieleza Mwananchi kuwa kuna tuhuma kwamba mgodi huo wa muda mrefu umeuzwa kwa Sh90 milioni tu.

Akizungumza na Mwananchi jana, Zitto alisema kamati yake itakaa na Spika wa Bunge kuomba mamlaka ya kushughulikia mgodi wa Nyanza kuhusu tuhuma kama hizo.

Zitto alisema ombi la kutaka kamati yake kuchunguza mgodi huo tayari pia limewasilishwa kwa Spika wa Bunge likitaka atumie mamlaka yake ili bunge lichunguze mchakato mzima wa ubinafsishaji wake.

Mwananchi iliona nakala ya barua ya wakazi wa Kigoma Kusini, wakiongozwa na David Kafulila ambayo ilipelekwa kwa spika na nakala yake kupelekwa kwenye kamati hiyo ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Zitto, ambaye kamati yake ina dhamana ya kusimamia mali za mashirika ya umma, alisema tayari kamati imepata barua hiyo ya wananchi na kwamba inachosubiri ni kupata maelekezo ya spika.

Alifafanua kuwa suala hilo liliwahi kujitokeza pia katika kamati ya Jaji Mark Bomani, lakini hadi inamaliza muda wake, haikuwa imepata taarifa za kutosha licha ya kutuma mwakilishi wake.

Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, ambaye alipata umaarufu kutokana na kukomalia kashfa za madini, alisema wakati Kamati ya Jaji Bomani inafanya kazi yake, ilimpeleka Idd Simba kwenda Kigoma Kusini kufuatilia tuhuma hizo, lakini majibu yaliyopatikana hayakuwa ya kuridhisha.

"Nimeamua kulifuatilia suala hili kwa karibu na kwa kasi... liliwahi kujitokeza kwenye kamati ya Mzee Bomani. Kamati ikampeleka Mzee Idd Simba lakini hadi tunamaliza hakukuwa na majibu ya msingi," alieleza Zitto.

Aliongeza kuwa katika kuondoa utata huo wa ubinafsishaji, kamati yake itakutana na pande zote mbili, ikiwemo shirika linalosimamia Ubinafsishaji na Mali za Umma (CHC) kupata undani wa sakata hilo.

"Kamati itatuma wajumbe ambao watakuwa pamoja na watu kutoka CHC kwa kuwa wao ndio wanahusika na ubinafsishaji wa mashirika ya umma, kamati yangu itataka kupata majibu ya msingi," alisisitiza Zitto.

Zitto alisisitiza kwamba safari hii asingependa kuona suala hilo halipatiwi ufumbuzi.

Sehemu ya barua hiyo inaonyesha hofu ya mchakato mzima wa ubinafsishaji wa mgodi huo ambayo ni pamoja na baadhi ya mitambo yake kuuzwa nchini Iran kwa Sh4.5 bilioni.

"Mgodi huo tajwa hapo juu (Nyanza Salt Mines Limited, zamani) ulikuwa mali ya umma na kubinafsishwa kwa kampuni ya wahindi ya Great Lake Mining corperation Ltd, mwaka 1999 ambao pamoja na mambo mengine, serikali ilitangaza msingi wa uamuzi huo ulikuwa kuendeleza mgodi huo ambao awali ulijulikana kama Nyanza Salt Mines Ltd na sasa Nyanza Mines Ltd baada ya kubinafsishwa," inasema sehemu ya barua hiyo.

Kwa mujibu wa barua hiyo, kabla ya mgodi huo kubinafsishwa, serikali ilitathmini thamani ya majengo, magari na mashine mbalimbali zilizokuwa zikimilikiwa na mgodi huo na kubainika kuwa thamani yake inafikia Sh7.8 bilioni.

"Mpaka siku ya kuuzwa akiba pekee yake ilikuwa Sh1.5 bilioni, achilia mbali chumvi na vifaa mbalimbali ambavyo mwekezaji alivikuta," inaeleza barua hiyo.

Madai mengine yaliyokuwamo kwenye barua hiyo ni malipo ya malimbikizo ya waliokuwa wafanyakazi katika kampuni hiyo ambao waliachishwa kazi kama ilivyoandikwa kwenye tangazo la serikali la Januari 11,mwaka 1995.

"Pamoja na ukweli kuwa wawekezaji walikuta visima vya chumvi ambavyo haijulikani vitakauka baada ya miaka elfu ngapi, taarifa zilizopo mgodi huu uliuzwa kwa Sh900 milioni sawa na Sh0.9 bilioni kwa wawekazaji wa Kihindi, lakini amelipa Sh90 milioni tu," inaongeza barua hiyo
 
Nimuhimu vilevile ni muhimu kujua thamani halisi ya mitambo baadaya ya depreciation na vilevile aina ya mitambo [inawezekana mitambo ya kizamani sana hata spea hakuna na inabidi mwekezaji anunue mipya. hivyo tunahitaji taarifa ya kina zaidi ili tuweze kujadili
 
Nimuhimu vilevile ni muhimu kujua thamani halisi ya mitambo baadaya ya depreciation na vilevile aina ya mitambo [inawezekana mitambo ya kizamani sana hata spea hakuna na inabidi mwekezaji anunue mipya. hivyo tunahitaji taarifa ya kina zaidi ili tuweze kujadili
kwa ujumla mgodi umetawaliwa na ardhi yenye madini na duniani kitu ambacho akina depreciation ni ardhi pamoja na madini kwa hiyo basi kutokana na tasmini ndogondogo tuu kitu kikubwa katika mgodi huu kama kime appreciate yaani kimeongezeka thamani kinaashiria ya kuwa mgodi huu ulitakiwa kuuzwa kwa bei ya juu zaidi kwani ukiangalia katika nchi za wenzetu ekari moja tuu ya inakadiriwa kuuzwa kwa takribani mamilioni ya shilingi kwa hiyo inabidi tupate taharifa zaidi za mgodi huu
 
Back
Top Bottom