Mgeja amgwaya Anne Malecela

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mgeja: Kilango sio saizi yangu
Tuesday, 28 December 2010 20:41

MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Khamis Mgeja, amesema hana nia ya kufanya malumbano na Anne Killango Malecela kwa kuwa halingani naye na anamheshimu sana .

“Sitaki kufanya malumbano ya kisiasa na Anne kwa kuwa siyo ‘size’ yangu…namshangaa kunijia juu na kunitolea maneno ya kashfa kwa mambo yasiyomhusu,” alisema na kuongeza kwamba hata imani yake ya dini inamzuia kufanya malumbano na mwanamke.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam , Mgeja alisema alieleza nia yake ya kutaka mmoja wa wanachama ambaye ni kiongozi aache kutoa maneno yasiyo na heshima dhidi ya vikao halali vya maamuzi vya CCM.

Hivi karibuni, Mgeja alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza nia ya kuwasilisha hoja dhidi ya Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kwenye kikao cha NEC akimtuhumu kuendeleza mgawanyiko ndani ya Chama. Mgeja alisema anawasilisha hoja hiyo ili Chama kiiweke kama agenda kusudi Sitta aweze kuthibitisha madai yake kuwa alienguliwa kuwania uspika kwa hila na Kamati Kuu ya CCM.

Baada ya taarifa hiyo, Anne alikaririwa akimjibu Mgeja kuwa aachane na Sitta na kuwa anapaswa kueleza kuhusu sababu gani zilizomfanya akiwa kiongozi akapoteza majimbo manne mkoani Shinyanga.

Mgeja alisema Anne ameshindwa kuelewa kuwa Tanzania imo kwenye ushindani wa vyama vingi ambako kuna kushinda na kushindwa na huko ndiko kukomaa kwa demokrasia, hivyo asianze kutafuta mchawi na kumuomba ajifunze kutoka nchi zilizopoteza dola kama Kenya , Zambia na Uingereza ambako vyama tawala viliondolewa.

Kuhusu tuhuma kuwa ametumwa na baadhi ya watu, Mgeja alisema: “Napenda kumuondoa mashaka kuwa mimi hakuna mtu yeyote au genge lolote la kunituma kwani ninao uwezo binafsi wa kujitegemea kifikra na kimtazamo na najitosheleza, hivyo anachokifanya ni sawa na mchezo wa watoto kumuangusha mtu mkubwa ambaye hawezi kutishiwa nyau.”

Aliongeza kuwa anashangaa kuona kuna uhusiano wa karibu sana kati ya Anne na Sitta kiasi cha mbunge huyo wa Same Mashariki kuamua kumjibia Sitta wakati hawatoki mkoa mmoja, sio msemaji wake na wala sio wakili wake na kuwa alichopaswa kumsaidia hapo ni kujibu hoja ya msingi ya kuondolewa kwa hila.

“Nikitaka kujibu ya Anne Killango ninaweza kuanzia Zanzibar hadi Bara na namshangaa kuulizia kupoteza majimbo Shinyanga, mbona haulizi Pemba tulikopoteza viti vyote, Kigoma, Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Iringa, Mara na Kilimanjaro anakotoka na ambako Mgeja hakuwepo?” alihoji Mwenyekiti huyo wa Shinyanga.

 

Aliongeza kuwa anashangaa kuona kuna uhusiano wa karibu sana kati ya Anne na Sitta kiasi cha mbunge huyo wa Same Mashariki kuamua kumjibia Sitta wakati hawatoki mkoa mmoja, sio msemaji wake na wala sio wakili wake na kuwa alichopaswa kumsaidia hapo ni kujibu hoja ya msingi ya kuondolewa kwa hila.

"Nikitaka kujibu ya Anne Killango ninaweza kuanzia Zanzibar hadi Bara na namshangaa kuulizia kupoteza majimbo Shinyanga, mbona haulizi Pemba tulikopoteza viti vyote, Kigoma, Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Iringa, Mara na Kilimanjaro anakotoka na ambako Mgeja hakuwepo?" alihoji Mwenyekiti huyo wa Shinyanga.

Hii tuhuma ni mpya hivi kweli Mzee wetu Sitta na Anne wana mahusiano ya karibu hata kumsukuma mama Malecela kumtetea SItta?
 
Hii tuhuma ni mpya hivi kweli Mzee wetu Sitta na Anne wana mahusiano ya karibu hata kumsukuma mama Malecela kumtetea SItta?
Hakuna tuhuma yoyote, haina maana lazima mtu awe mkoa wako au mna mahusiano fulani ndio akutetee, Mgeja ameonyesha utupu wa upeo na kuchukua hiyo point kama hoja ni ufilisi wa analytical skills kwa yeyote atakayefanya hivyo

performance plan inapimwa na magoli na mgeja kafungwa mengi kuliko aliyofunga, huwezi ati kujilinganisha na pemba au mwanza simply to justify your failure

Mgenja is kwishnehi
 
Mgeja ni mtupu. Na anakwenda katika siku zake za mwisho katika uongozi. Sitta na Anne achaneni naye, maana kulumbana na mtu asiye na elimu nalo ni tatizo jingine. Inatakiwa kuwa na kiwango cha elimu hata katika kugombea uongozi ndani ya vyama. Kiwango cha elimu cha Khamis Mgeja kinanipa mashaka makubwa maana kauli zake siku zote zinadhihirisha hivyo. Yaani anaona kujibizana na mwanamke ni kosa? sikiliza anavyosema "hata imani yake ya dini inamzuia kufanya malumbano na mwanamke." Sasa anafanya nini kwenye siasa maana kuna wanawake wengi sana huko wengine wako UWT sasa hapo hata simuelewi!
Lakini, ebu tujiulize kweli Sitta alifanya sawa kusema aliyosema kwenye vyombo vya habari kuhusu chama chake? kwa nini hakulalamikia kule kule chamani? Si ni yale yale ya Zitto Kabwe? Kama Sitta hakukosea kufanya alivyofanya, basi na Zitto asiandamwe kwa kauli hizo hizo anazofanya dhidi ya chama chake kila siku!.
 
Mama Kilango, Mgeja hapatoshi


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MJUMBE wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Khamis Mgeja, amesema hana nia ya kufanya malumbano na Anne Killango Malecela kwa kuwa halingani naye na anamheshimu sana. 'Sitaki kufanya malumbano ya kisiasa na Anne kwa kuwa siyo 'size' yangu'¦namshangaa kunijia juu na kunitolea maneno ya kashfa kwa mambo yasiyomhusu,'� alisema Mgeja na kwamba hata imani yake ya dini inamzuia kufanya malumbano na mwanamke.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es Salaam , Mgeja alieleza nia yake ya kutaka mmoja wa wanachama ambaye ni kiongozi aache kutoa maneno yasiyo na heshima dhidi ya vikao halali vya maamuzi vya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Hivi majuzi, Mgeja alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza nia ya kuwasilisha hoja yake dhidi ya Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kwenye kikao cha NEC akimtuhumu kuendeleza mgawanyiko ndani ya chama.
Mgeja alisema anawasilisha hoja hiyo ili chama kiiweke kama agenda, kusudi Sitta aweze kuthibitisha madai yake kuwa alienguliwa kuwania uspika kwa hila na Kamati Kuu ya CCM.
Baada ya taarifa hiyo, Anne alikaririwa akimjibu Mgeja kuwa aachane na Sitta na kuwa anapaswa kueleza kuhusu sababu gani zilizomfanya akiwa kiongozi akapoteza majimbo manne mkoani Shinyanga.
Mgeja alisema Anne ameshindwa kuelewa kuwa Tanzania iko kwenye ushindani wa vyama vingi ambapo kuna kushinda na kushindwa na huko ndiko kukomaa kwa demokrasia, hivyo asianze kutafuta mchawi na kumuomba ajifunze kutoka nchi zilizopoteza dola kama Kenya , Zambia na Uingereza ambako vyama tawala viliondolewa.
Kuhusu tuhuma kuwa ametumwa na baadhi ya watu, Mgeja alisema: 'Napenda kumuondoa mashaka kuwa mimi hakuna mtu yeyote au genge lolote la kunituma kwani ninao uwezo binafsi wa kujitegemea kifikra na kimtazamo na najitosheleza, hivyo anachokifanya ni sawa na mchezo wa watoto kumuangusha mtu mkubwa ambaye hawezi kutishiwa nyau.'�
Aliongeza kuwa anashangaa kuona kuna uhusiano wa karibu sana kati ya Anne na Sitta kiasi cha mbunge huyo wa Same Mashariki kuamua kumjibia wakati akiwa si msemaji wala wakili wake.
 
Back
Top Bottom