Mgaya hujawatendea haki wananchi wa Mbeya mjini

Ground Zero

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
342
95
Kitendo cha Katibu Mkuu wa wa TUCTA Nicolaus Mgaya kutambulisha wageni bila kumtambua Mbunge wa Mbeya mjini Mheshimiwa Sugu inaleta sura mbaya. Hata mkuu wa mkoa naye kashindwa kutambua uwepo wake sijaelewa ni kupitiwa au wamefanya makusudi.
 
Mbunge wa Mbeya Mjini amatambulishwa na Waziri wa Kazi na Ajira Mh.Mgosi Kabaka.
 
Nafikiri Waziri ndio aliowaalika wabunge wote walioenda maana waziri Kabaka amewatambulisha!!tupunguze jazba
 
Kitendo cha Katibu Mkuu wa wa TUCTA Nicolaus Mgaya kutambulisha wageni bila kumtambua Mbunge wa Mbeya mjini Mheshimiwa Sugu inaleta sura mbaya. Hata mkuu wa mkoa naye kashindwa kutambua uwepo wake sijaelewa ni kupitiwa au wamefanya makusudi.

Ametambulishwa na mheshimiwa waziri wa kazi kama mjumbe wa kamati ya bunge ya masuala ya jamii
 
Acha kupotosha! Na ushabiki mwingine ni wa kijinga!

Sugu hakualikwa na TUCTA wala mkoa wa Tanga hivyo hawakuwa na mamlaka ya kumtambulisha.

Sugu alialikwa na wizara ya kazi na ajira na ndiyo sababu Waziri Kabaka amemtambulisha!
 
Ata nami mwanzo nilitahamaki sana.
Ila baadae bibi Kabaka akamtambulisha nkapata amani kidogo maana nilidhani ni mambo ya Kichama zaidi
 
Ni itifaki tuNdg. Mtoa mada..!! Wabunge wale wa kamati ya bunge walialikwa na Wizara ndiyo maana wametambulishwa na wazir muhusika...!! kuna neno hapo!!??
 
Kitendo cha Katibu Mkuu wa wa TUCTA Nicolaus Mgaya kutambulisha wageni bila kumtambua Mbunge wa Mbeya mjini Mheshimiwa Sugu inaleta sura mbaya. Hata mkuu wa mkoa naye kashindwa kutambua uwepo wake sijaelewa ni kupitiwa au wamefanya makusudi.

Huyo ndio Mgaya, kelele zote zile zilikua njaa tu, saa hizi anatafuna kila kitu kasahau
 
Chuki binafsi dhidi ya mwakilishi wa wananchi nafsi moja haiwezi ikadhulumu nafsi mia hii yote inatokana na kwamba sugu anatoka upinzani hapo ndo unamjua yupi anatumika na yupi hatumiki
 
Back
Top Bottom