Mgao wa umeme: WaTanzania tuamke, tuukatae

wanaopata mimba ni kiherehere chao.
Wanaoathiriwa na mgao wa umeme ni uzembe wao.
Mawazo ya 'kwamba tunamgao wa umeme ni ya chadema' wao hawaoni mazuri wanaona mabaya tu.
Serikari imefanya mambo mengi mazuri tangu uhuru, ikiwa ni pamoja na mgao wa umeme usiokwisha. Hayo yote ni maendeleo.
Ccm wamejitahidi sana kama si wao nchi ingekuwa haina hata generator, lakini sasa watu wengi wamejua generator, mishumaa, taa za chemli, torch za kucharge na solar.
Ngeleja tunakupongeza kwa utendaji wa hali ya juu ulio makini na wenye tija. Raisi anapaswa kukupa uwaziri mkuu.
 
Tuwape muda mpaka 1/8/2011 kama awana solution atukutane Mnazi Mmoja tarehe 2/8/2011 saa 10:00AM kupinga mgao wa umeme,
Hapo sasa ndo umeongea,ateuliwe mtu wa kutoa taarifa polisi (sio kuomba kibali maana kuandamana ni haki ya kila raia), naaga ofisin kwamba sintofika siku hiyo.
 
Mwenye mkakati mzuri aulete mi niko tayari kuunga mkono,kwanza walioingia mkataba wa IPTL kama wako hai na wapo kwenye utendaji wa serikali hadi sasa hivi kwanini tusiwafukuze kinguvu sisi wananchi wenyewe..naombeni majina yao japo tuwafaham na hatua zingine zije..
Yuko jamaa anaitwa Jakaya Kikwete ni waziri wa Fedha wa Serikali ya Rais Mwinyi ndio kaingia huo mkataba.
 
tatizo kubwa la watanzania ni waoga wa kudai haki zao za msingi suala umeme limechangiwa kwa kiasi kikubwa na woga wetu tujilaumu wenyewe ,haki ya mtu haimbwi bali inatafutwa .sasa ni muda muafaka wa kuitafuta haki yetu watanzania tubadilike jamani .wanaoumia ni sisi wananchi sio vingozi hima watanzania twendeni tukadai haki ya kupata umeme masaa 24
tuko pamoja
 
Mkuu inategemea wewe unatoka Tanzania ipi. Cahnzo cha mgao au tatizo la umeme kinajulikana, lakini still bado watu wamelala. Tunatatzi la kulalamika tu lakini hatufanyi lolote.

Nakumbuka General Ibrahim Badamasi Babangida aliwahi kusema akiwa ziarani hapa Tanzania kuwa "it is easy to rule Tanzania than to ride a herd of cattle", wakati ule tuliona kejeli, lakini ni ukweli sasa tunauona. Ujinga huu ungetokea Lagos au Abuja sidhani kama "TANESCO" wa kule wangechekewa kama hapa.

Ni nini chanzo cha mgao wa umeme? mimi binafsi na wengi humu JF hatujui kwanini Tanzania hivi sasa inapata umeme kwa masaa 6 tuu kwa siku.
 
Uoga wetu ndio umasikini wetu, tumezidi kuwa waoga kuandamana ili kudai haki zetu, kwanza hatujui haki zetu ni zipi na uoga wa kuzidai ndio umejaa.Tutazidi kuonewa, kunyanyaswa na kuteswa mpaka tutakapo jitambua kama hao wenzetu wa senegal.
 
Huu mgao upo uswahilini tu,wengine hatujawahi kuupata kabisa,mi nadhani tuandamane la sivyo..waswahili wanasema..UOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO.Watanzania tuamke.
 
Unajua sikujua kumbe Ngeleja alikuwaga mwanasheria wa kampuni ya Caspian??????????!!!!!!!!!!!!!!!!
Dahhhhh imekula kwetu tutaendeshwa na mgao mpaka tutie akili
 
Jamani watanzania wenzangu,nimechoka kabisa Serikali ya Ccm na hakika nipo tayari kwa lolote hakika sina cha kupoteza tena kwani Mgao wa umeme umenimaliza kabisa umenifanya masikini sijui ninakuwa mgeni wa nani mimi,mke na watoto.Ninachukia sana Wanasiasa kwani wametufikisha hapa.
 
Pole sana ndugu yangu nakupa pole nikiwa mwenye uchungu pia cz biashara yangu ya barafu nimeiacha,ama kwel serikali imenipa rikizo ya lazima
 
Wana Jf nashawishika kusema ya kuwa kama Edward Lowassa angekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, leo hii hakika kusingekuwa
na mgao wa umeme,nashawishika kusema hayo kwani kila mtu anajua fika spidi aliyokuwa nayo huyu Mheshimiwa katika masuala
ya kiutendaji.Najua kuna watakaobisha lakini hayo ni maoni yangu binafsi ,wadau,naomba kuwakilisha.
 
Kweli akili ni kama parachute kufanya kazi lazima ifunguke! LOWASA ndiye aliua mpango wa Tanesco kununua mitambo ya umeme akaleta Richmond iliyobadilika majina dowans mpaka leo symbion. TOKA NDANI YA SHIMO LA UVIVU WA KUFIKIRI.
 
Wakuu,hii hali ya umeme,serikali haionekani kama inashugulikia.Ila pia ni 50 ya uhuru hatuna umeme wa uhakika lakini tuna uhakika wa kununua Rada,Ndege,Richmond,EPA.Sasa je CHADEMA ituunganishe nchi nzima ili tudai haki zetu za msingi
 
Wakuu,hii hali ya umeme,serikali haionekani kama inashugulikia.Ila pia ni 50 ya uhuru hatuna umeme wa uhakika lakini tuna uhakika wa kununua Rada,Ndege,Richmond,EPA.Sasa je CHADEMA ituunganishe nchi nzima ili tudai haki zetu za msingi

Kule Misri na Tunisia hawakutegemea vyama kudai haki zao za msingi. Kama unategemea vyama kupata haki zako za kimsingi sahau.
 
Maandamano ya nini na jana tumeona mtambo mmoja umeshushwa na mingine ipo njiani, na mchuchuma mkataba tayari na kazi imeshaanza, msituletee fujo hapa. Ya Arusha hayajawatosha?
 
  • Thanks
Reactions: Omr
Je ni kweli serikali haiwezi kuvalia njuga suala la umeme na kulimaliza? au ni mpango wa kuwamaliza baadhi ya wanasiasa.

Nikitafakari kauli ya Sitta kuwa waliolifikisha taifa hili hapa wawajibishwe, akimaanisha kuanzia kwenye sakata la richmond, najiuliza
yeye akiwa kama waziri ndani ya serikali, amependekeza suala hili katiaka baraza la mawaziri?

Kuzungumza katika mkutano wa hadhara kwamba wahusika wawajibishwe, licha ya kuwa kwa upande mwingine ni haki yake, lakini kisiasa inaonekana ni njia ya kutafuta public support, bila yeye mwenyewe kuchukuwa hatua stahiki kama waziri ndani ya serikali.

Sambamba na mpango wa kujivua gamba na kuwatumia watu waoga na walaini kama R.A kumvunja nguvu E.L, je huu mgao wa umeme ulioliokithiri ndiyo karata yao ya kuwafanya watu wamchukie E.L? Kwamba yeye ndiye kasababisha hivyo, ni fisadi na hafai?!

Mimi ninaamini kuwa CCM wapo tayari kupata wanachokitaka at any cost ya watanzania, kuwasulubisha wananchi ili kushinda vita yao ya kisiasa.

Mtazamo tu !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom