IPECACUANHA
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 3,216
- 1,906
Hivi kweli hakuna wa kutatua tatizo hili? Mgao Umepitiliza masaa 16 na bado unaendelea. Garama ya mgao huu itarudisha nyuma miaka 20. Nahisi wasimamishe michakato yote ya kujiunga katika eneo la kiuchumi la afrika mashariki. Wakati wakenya, waganda, wanyarwanda wanazalisha sie tumesimama halafu tuungane kwa lipi? Inatia hasira sana hali hii. Hivi hakuna wa kuunganisha sauti zetu kwenye hili???Naona tunalia mmoja mmoja ndio maana ngeleja na wenzie wanaendelea "burudani" kama kawa...Suala hili linahitaji uwajibikaji wa hali ya juu na sio huu tunaouona. Au ndio wanataka tuseme bora ya lowasa na Richmond yake kuliko hiki cha Pinda? Naona kuna kitu nyuma ya pazia na Raisi anafumbia macho.Hasiraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa