Mgao wa umeme wa kufa mtu watangazwa, Juni 2011 na kuendelea

poleni wabongo kwa sisi tulioko madongo kuinuka nlishasahau kama umeme huwa unakatika au maji.
Kilichopo tafuteni umeme mbadala.nendeni kariakoo kuna wakala mjapan anauza convertor
nunua hizo na betri zake 2 garama sii kubwa sana ni kama laki 6 inategemea ww unataka kutumia vifaa gani
nahisi fen tv taa sii inatosha? unaichaji wakati umeme unaporudi na una uwezo wa kuitumia hata wiki 2 bila shida
.kwa wale wasio na umeme inabidi wanunue kajenereta kadogo kwa kuchajia.
Sijui tutalalamika hadi lini wkt tunajua Tanesco kumejaa ufisadi.
hata kama wanaosha visima vya gesi walitakiwa kuwa na source mbadala.
wabongo kama mmenielewa changamikeni hizo convertor ukijifunga
kwa miezi 2 unanunua ukipunguza kukaa bar na kutoa ofa kila wakati,kuchangia changia harusi,
kujinyima mavazi ya garama utaweza.
Tunaweka mno starehe au kupenda kuonekana na watu tuna uwezo kifedha
ilihali hatutaki kuwaza umeme mbadala majumbani mwetu.kazi kwenu.
Kwa wale ambao wana nyumba zao tembeleeni pale ubungo external kuna bwana mmoja
yeye mtaalamu wa umeme wa upepo atakuja kwako atapima eneo atakufungia umeme
na kutegemea na matumizi yako ndio bei inategemea lakini sii kubwa pia wapo kawafungia
hawana shida hadi friji wanatumia nk.


Mkuu tupatie maelekezo vizuri,jina na tunafikaje hapo pamoja na hata namba zao za simu, si unajua kkoo unaweza ukazunguka kumbe duka lipo hapo hapo.
 
tatizo letu watanzania tunaongea nyuma ya desktop na SIPIYU tu... kama tumeona enough is enough lets do something about it!

huu upuuzi kamwe hautaisha kwa style hii, shurti tutiane adabu kwanza ili tuheshimiane... nilmeangalia mkuu akifungua sijui ndio warsha ya mawaziri na makatibu wakuu leo yani, kama una bastola unaweza kuibatua TV yako.. its rubbish hakuna hata mmoja anayeonekana anakerwa na hali ya maisha ya watanzania kwa sasa
 
MmH! Jana ilikuwa tatizo ni maji hakuna Mtera, leo gesi!! Makubwa hayo! Lakini tumezoea. Wana JF tafuteni mbadala. Windmill, Solar na nyinginezo.
 
Na sikirini.
tatizo letu watanzania tunaongea nyuma ya desktop na SIPIYU tu... kama tumeona enough is enough lets do something about it!

huu upuuzi kamwe hautaisha kwa style hii, shurti tutiane adabu kwanza ili tuheshimiane... nilmeangalia mkuu akifungua sijui ndio warsha ya mawaziri na makatibu wakuu leo yani, kama una bastola unaweza kuibatua TV yako.. its rubbish hakuna hata mmoja anayeonekana anakerwa na hali ya maisha ya watanzania kwa sasa
 
hao TANESCO ni balaa kwa kifupi wanakera, kuna wakati niliwahi kumsikia mkuu wa nchi akisema kuwa kuna mikakati ya muda mrefu, mfupi na ya kati,ya kulitoa taifa katika giza, could someone tell me hizo ahadi utekelezaji wake umefika wapi?
 
Wadau kuna kila dalili kwamba lile sakata la Dowans bado linatutafuna kwani leo" MGAO WA UMEME UMEANZA MOROGORO" wakati hakuna maelezo yaliyotolewa zaidi ya ule mgao utakaoanza 19/05/2011.Hii imekaaje huko kwingine?
 
SHIRIKA la Umeme Tanzania [Tanesco] umetangaza ratiba ya mgao unaotarajia kuanza Mei 19 mwaka huu katika mikoa ipatayo 12 ya Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo kutoka kitengo cha mawasiliano Makao Makuu imesema kuwa, mgawo huo utahusisha Mkoa wa Dodoma, Morogoro, Mara, Tabora, Pwani, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Iringa, Mbeya, Manyara na Dar es Salaam.

Mgao huo unatarajiwa kuanza Mei 19 mwaka huu katika mikoa iliyoanishwa na shirika hilo, unaotarajiwa kukatika kwa awamu ambapo baadhi ya maeneo utakatika kuanzia saa 2 asubuhi na kupata umeme saa 12 jioni na baadhi ya maeneo utakatika majira ya saa 12 jioni na kurejea saa 5 usiku.

Mgao huo uliotangazwa n shfirika hilo unatarajiwa kudumu wka kipindi cha mwezi mmoja.
 
Huku kwetu walianza mgao tokea wiki mbili zilizopita nashangaa kusikia mgao unaanza tarehe 19
 
Back
Top Bottom