Mgao wa umeme wa kufa mtu watangazwa, Juni 2011 na kuendelea

Sababu kubwa ni kuadimika kwa gesi kutoka Songosongo.
 
Nchi hii shida na taabu haziishi, CCM wanatuzoesha shida na taabu hizi.
Kuna kundi la watu ndani ya chama lina maslahi na mgao huu wa umeme.
 
Tujuze mkuu, mgao unaanza lini tena na kwa muda gani AAAAAGGGGRRAAAAAAABbb
 
Jamani, si juzi walisema wamefungua zabuni ya kufua umeme wa ziada!, ni kampuni gani iliyoshinda zabuni hiyo?. Kampuni iliyoshinda itaanza kuzalisha umeme lini?.
 
Kazi kweli! Less than 15% ya wtz ndio wana access ya umeme lakini hata hivyo Gtz inashindwa kuhakikisha uhakika wake.

Mwisho wa siku utasikia takwimu uchumi wetu umekuwa sana na tatizo la ukosefu wa umeme haukuathiri kitu...
 
sikosefu wa gesi, ni kwamba mitambo ya songo songo itasimama kwa ajili ya inspections kwa about a week, won't be gas supplied. Mgao lazima maana asilia 70 ya umeme unatokana na ges
 
Jamani hii nchi wacha tu tuandamane kila siku maana ni soo. Inamaana hao hawakujua kwamba wanatumia gesi wakaweka reserve au ndo mpaka iishe ndo waanze kutafuta mzabuni. Kwanini serikali yetu inapenda kuishi jana badala ya kuishi kesho.
 
Sisi huku kanda ya Kaskazini tangu jana nimewataarifu ya kwamba mgao ni mtindo mmoja labda wanakazia zaidi. Acha ije2! Yenye mwanzo na hata mwisho wake upo. Si ndiyo CCM! Hamna tabu.
 
Baada ya nahau za Magamba chacha wanaanza kutafuta fursa ya kujilipa wao na fisadi papa RA. Kama nilivyosema siku nyingi na signature yangu hapo chini. Watanzania wataendelea kulia na kusaga meno hadi pale watakapoweza kumwondoa m k w e r e pale Magogono kwa sababu yeye ndio kimbilio la mafisadi.
 
Nikisoma,nikiangalia au nikisikia habari za TANESCO,ATCL,TTCL,DAWASCO siku zote huwa naanza kuona kizunguzungu hata kabla habari hiyo haijaisha.
 
Mlimani tv habari

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco ametangaza kutakuwepo mgao wa Umeme kuanzia tarehe 16 May kutokana upungufu wa megawatt zaidi ya 200. Amesema mvua zinazonyesha hazijaketa nafuu yoyote

(nilipatwa na hasira kuhusu taarifa hizi nikashindwa kusikiliza vizuri maelezo zaidi)
 
Lazima upate hasira Mkuu, tatizo la umeme ni la miaka 19 sasa, ndiyo miaka 19 tangu 1992 lilipoanza rasmi na hadi leo hii hakuna ahueni yoyote ile ya kuondoa adha hii isiwepo tena.
 
Lazima upate hasira Mkuu, tatizo la umeme ni la miaka 19 sasa, ndiyo miaka 19 tangu 1992 lilipoanza rasmi na hadi leo hii hakuna ahueni yoyote ile ya kuondoa adha hii isiwepo tena.

mkuu una maanisha kabla ya 1992 hakukua na tatizo la umeme?
nilikua mdogo sana na nilikua porini,kwenye vibatari!
 
mkuu una maanisha kabla ya 1992 hakukua na tatizo la umeme?
nilikua mdogo sana na nilikua porini,kwenye vibatari!

Kabla ya tatizo la mgao kuanza rasmi 1992 umeme ulikuwa wa uhakika kama ukikatika basi ni kwa masaa machache sana na wakati mwingi sababu zinazoeleweka zilikuwa zinatolewa labda kuweka nyaya mpya, kubadilisha transformer(s) au matengenezo ya kawaida tu, siyo kama ilivyo sasa. Hili swala la kina cha maji kimepungua kule Mtera au Kidatu sikuwahi kabisa kulisikia.
 
haya ndio matunda ya ccm! Ngoja nipate japo :majani7: ili nipoteze japo mawazo na kupunguza hasira mie.
 
Back
Top Bottom