Mgao wa Umeme: Tatizo ni UKAME - Kikwete akihojiwa na BBC

This is a shame..., yaani hata huu uongo haujaenda shule kabisa... Ukitaka kufanya kitu do it perfect...
Yaani hata kama ni uongo weka some credible facts..... Tofauti na hapo is insulting people's intelligence kuona kwamba wanaweza wakakubaliana na hizo fiction stories
 
Nimemsikiliza, tangu mwanzo nilijua tunaye rais dhaifu lakini leo nimekata tamaa kabisa. Nimefikia kiwango cha mwisho cha kukosa matumaini kuhusu kikwete
 
Rais Jakaya Kikwete, ameuzungumzia mgao wa umeme unaendelea sasa nchini kote, amesisitiza "tatizo ni ukame".

Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye mahojiano maalum na BBC akiwa nchini Afrika Kusini yaliyorushwa jioni hii na BBC Swahili.

Rais amesisitiza, kwa vile mitambo yetu mingi inategemea nguvu za maji, hivyo tatizo la umeme limesababishwa na ukame.

Mwandishi akahoji kuwa tangu 2006 mgawo ulipoanza, bado tuu mlikuwa mkitegemea mvua?.

Rais alijibu kuwa baada ya 2006 hatua mbalimbali zimechukuliwa kuzalisha umeme kwa njia za gesi, makaa ya mawe hata umeme wa nguvu za upepo, lakini miradi hii yote inahitaji muda muafaka wa kuagiza mashine, akasisitiza ununuzi ewa mitambo unachukua muda, "huwezi kununua mitambo ya umeme hivi hivi tuu kama unavyoingia dukani kununua koti lako, mitambo huagizwa kwa kupeleka order kiwandani utengenezewe. hata hii mitambo inayoingizwa nchini hivi sasa, iliaagizwa toka mwaka jana.

Rias Kikwete amewataka wanasiasa wasibeze juhudi za serikali kuwaletea umeme wa uhakika Watanzania.

Pia Rais Kikwete, ameuhakikishia tena ulimwengu kupitia BBC kuwa serikali yake ni sikivu, kama kuna watyu wenye hoja za msingi kuhusu utatuzi wa tatizo la umeme, wasiishie tuu kulalamika, bali waje na hoja za jinsi ya kutatua tatizo hili na serikali yake itazipokea hoja hizo na kuzifanyia kazi.

My Take.
Japo ni kweli sababu kuu ya mgao huu wa umeme ni ukame, Tanzania would have done better by now kama tatizo lilijulikana tangu 2006, ila pia huu ni wakati kwa sisi Watanzania tuitikie mwito wa rais wetu, " Tupunguze kulalamika tuu, tuje na solutions, serikali ikizikataa ndipo tuibeze kuwa "Tuliwashauri na hamkusikia!"

Pasco

Hivi kumbe ukiwa Mh. Rais Unajibu chochote hata kama kinaudhi??..watakufanyaje? Mitambo ya kufua umeme ipo mingi tu, katika hali ya dharura utasubiri mwaka mzima bwana? tuseme mvua zimegoma na Mtera imekata maji, ndo kusema tutasubiri mwaka mzima itengenezwe, hebu tusidanganyane bwana. Hatuko serious,kwisha????
 
Ndugu yangu BHT siku zote mambo mazuri hayataki haraka. Be a litle patience good things are coming!.
Yaani kweli miaka yote hiyo unataka kuniambia ni mwendo kasi gani huu unaotumika hapo?! I guess hatutafika labda tubadili njia , hiyo itakuwa na miiba hasa.I am always patient but this time they have pressed the wrong button... I have lost mine already, too bad!
 
Pasco,Unachoshindwa kuelewa ni kuwa,hii ni emergency.Kwanini tumetumia mabilioni ya dola kwa ajili ya emergency?Tuna makaa ya mawe,kwanini tunashindwa ku-convert kiwira ili tuzalishe 400mw? mbona hii kitu inapotezwa kihunihuni tu,wakati tunajua kuwa tuna uwezo huo?Kuhusu mashine kuwa show room,mbona zipo nyingi tu.
Kobelo
 
My Take.
Japo ni kweli sababu kuu ya mgao huu wa umeme ni ukame, Tanzania would have done better by now kama tatizo lilijulikana tangu 2006, ila pia huu ni wakati kwa sisi Watanzania tuitikie mwito wa rais wetu, " Tupunguze kulalamika tuu, tuje na solutions, serikali ikizikataa ndipo tuibeze kuwa "Tuliwashauri na hamkusikia!"

Pasco

I don't think so. We have been promised and promised and promised and promised, etc kuwa serikali itatatua tatizo la umeme. Watu wanalalamika b'se the promised were given have not been fulfilled. Serilali intakiwa ije na solution. We elected them to fix the problems, they promised us they will fix. Kusema kuwa tusilalamike na tuje na solutions, then you're shifting the burden from the voted to the voters. Kama tuliowaweka madarakani wameshindwa kufix matatizo waliyohaidi kufix, then wapishe wengine wanaoweza. Paso, you take is so low, I mean very low on this point.
 
huyu jamaa hamna kitu kabisa, hivi haoni mifano toka nchi jirani, kama alikuwa anajua yote hayo kwa nini alitoa miahadi mingi, eeh Mungu tuepushie magamba huyu.
 
alafu mleta thread hii umeniudhi ulipomalizia kwa kusema watz tupunguze kulalamika,tuje na solution tuone kama serikali itazikataa,hapo ndipo nilipojua wewe ni magamba tuu,raisi ,ngereja na hata pinda walisha sema mgao wa umeme utakuwa historia inamaana kuwa walikuwa na mikakati yao imewashinda wakwako wataukubali hivi wewe unaishi tz kweli,unadhani hawa hawapati ushauri wanapata ila kwa taarifa yako hilo ni chaka lao la kuchumia hela hawana dhamira la kulimaliza hivi wewe unaamini serikali ikiamua kununua mitambo miwili kama huo wa dowans haiwezi dhamira ya kweli hawana kwanza jk ni mbishi na mgumu kuelewa.
 
.........Mwandishi akahoji kuwa tangu 2006 mgawo ulipoanza, bado tuu mlikuwa mkitegemea mvua?.

Rais alijibu kuwa baada ya 2006 hatua mbalimbali zimechukuliwa kuzalisha umeme kwa njia za gesi, makaa ya mawe hata umeme wa nguvu za upepo, lakini miradi hii yote inahitaji muda muafaka wa kuagiza mashine, akasisitiza ununuzi ewa mitambo unachukua muda, "huwezi kununua mitambo ya umeme hivi hivi tuu kama unavyoingia dukani kununua koti lako, mitambo huagizwa kwa kupeleka order kiwandani utengenezewe.

Je ni mitambo gani ambayo toka 2006 imeagizwa????????????
 
Huo ndo ukweli mkubwa wangu!Kama tunabisha sisi sio tatizo, hao watawala bado wanafanya nn hapo?Yaani kosa mara ya kwanza, na ya pili pia? Haya tutasingizia waliiba kuwa si hatukuwachagua, haya basi wametuthibitishia hawawezi kutupeleka tutakapo. Tumefanya nini basi? Sisi wenyewe janga!

Mmhhhhhhh....B, hata sijui niseme nini...Ila naamini hatujashindwa kila kitu...Kwani hata kuzaa tukaijaza nchi kumetushinda????? ....LOL........
 
Ndugu yangu BHT siku zote mambo mazuri hayataki haraka. Be a litle patience good things are coming!.

Kweli mkuu??

Hivi kipimo cha kutokuwa na haraka ni kusubiri siku ngapi, miezi au miaka mingapi?
 
Mkuu ni lini serikali ya JK imewahi kusikiliza ushauri wa watu wengine!!! Jk na watu wake wanatupa ushauri wa wataalamu!! Wana-substitute na ushauri wa kisiasa, nani anaweza kumshauri JK!!!

Hawa watu ni kama donda ndugu, haliskii dawa wala nini, hotuba ngapi za shauri mbali mbali za vyama vya upinzani, wataalamu wetu, walimu wa vyuo vikuu vyetu wamewahi toa, wa vikaweka kapuni!!! Wanaamini yao, kwa hiyo sisi hatuna la kusema, tunaombwa tu tusiwabeze!!!

Sualaliliopo ni kujikumbusha enzi za JKT, disco baada ya kula kabla ya kulala, tusogeze muda tulale, tusubiri kesho!!!

Mkuu,

Hakuna serikali sikivu kama hii ya JK. Inasikiliza ushari tena sana ila shinda ya watu wanaolalamika ni kwamba hawana nasaba na wale wanaotakiwa kuishauri....yaani watu wa aina ya marehemu Shekh Yahaya Hussein (R.I.P)!
 
mwaka 2005 babayangu alisema maneno haya '' kikwete is the worst president we ever had''juzi nimeenda kumuona huko kijijin kwake akatoa tena kauli hii ''' we have the president who cannot think beyond the next meal''
du baba yako Mbabe kamanda.
 
Kwanini tuna discuss megawati 200?....zitatusaidia nini zaidi ya kutupa hasara?
When are we going to start thinking BIG,...I mean big/humongous.
 
JK ni '0' hoja zake nyepesi. Ndiyo tatizo la nchi kuongozwa kiganga badala ya kisayansi.
Vijijini wanachagua kwa wingi mafuta ya taa bei juu hata hawawezi kununua tena...mzee anakata mitaa kana kwamba hakuna kilichotokea!
 
Kweli mkuu??Hivi kipimo cha kutokuwa na haraka ni kusubiri siku ngapi, miezi au miaka mingapi?
Wee subiri tu Dc haraka ya nn? Mbona hata Masihi bado tunamsubiri! Wameleta jenereta la megawati mia, na lingine laja, na symbion watazalisha! Wee subiri tu!
 
ungemsikiliza leo wakati anahojiwa na BBC alikuwa anaonyesha kutetemeka...hana la kufanya ameenda kutafuta wawekezaji ...sijui watatumia umeme gani wakija! Ameshindwa kujiwekea vipaumbele. POLE watanzania miaka 5 ijayo?
 
Mmhhhhhhh....B, hata sijui niseme nini...Ila naamini hatujashindwa kila kitu...Kwani hata kuzaa tukaijaza nchi kumetushinda????? ....LOL........
LOL....hilo hata kwenye kambi za wakimbizi wa kivita halikwepeki kaka! (pamoja na kutkua na uhakika wa usalama wao)
 
Back
Top Bottom