Mgao kuanza!

Kutokana na uchakavu wa mitambo bla bla bla... mgao wa umeme kuanza nchini kote kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne (+or -) .. bla bla bla..

Habari ndiyo hiyo.. miradi ya Jenereta iko juu! Hatimaye salimu amri mnunue majenereta ya Dowans kwa Bilioni 69 ambayo mmeshawalipa bilioni karibu 40 kuyasafirisha!

Bongo tambarare bwana tumeshazoea adha aina zote ndio maana mtanzania nchi yoyote anaweza kuishi isipokuwa yenye vita tu sababu hatujazoea. Haijawahi kutokea ndani ya Mwezi mzima umeme uwe stable bila kukatika hovyo na muda mwingine bila taarifa.
 
Maumivu tunayapata. Lakini tumepigwa ganzi hatuyasikii. Uchaguzi unakuja; na hawa hawa wanaotuletea maumivu na kutuongezea ufukara tutawachagua tena.

Miafrika bana. Kazi kweli kweli.
 
Bora kubadili uraia ukaishi Rwanda au Burundi kuliko kwendelea kuona aibu kama hizi.
 
Haya yote ni mazao ya kukosa maamuzi magumu, ufuatiliaji na mipango thabiti

Waziri huyuhuyu amekuwa pale miaka yote anazunguka na magazeti tu mkononi na kugomnbana na walinzi badala ya kubana wataalam walete sustainable electricity plan ya nchi
tunakaa hukonga hadi nguzo za umeme
tunaripoti kila kitu

lakini waziri ameshindwa kuondoa siasa kwenye mhimili huu wa uchumi

kinachonisikitisha, kwanini JK anamuacha pale??

Idris tumemsema weee kaishia
zitto alisema hapa tukaona dawa ni kumuwasha makombora

tuamke watz... ni sisi ndio matatizo

unahsangaa hata kakobe tu anachukua miezi ili aamue kuiruhusu serikali kuendeleza watu wake

WE NEED ONE DICTATOR AT LEAST FOR 18 MONTHS
 
Kutokana na uchakavu wa mitambo bla bla bla... mgao wa umeme kuanza nchini kote kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne (+or -) .. bla bla bla..

Habari ndiyo hiyo.. miradi ya Jenereta iko juu! Hatimaye salimu amri mnunue majenereta ya Dowans kwa Bilioni 69 ambayo mmeshawalipa bilioni karibu 40 kuyasafirisha!

Zile $600m+ alizokopa Idris toka mabenki zilifanya nini?
 
wakati mwingine huwa natamani kuikimbia nchi yangu..lakini..
Labda iko siku isiyona jina mambo yatakuwa shwari .
Tufunge na kuomba :mad:
 
Wafanyakazi wa Tanesco wanafikiri wameajiriwa kuwatangazia watanzania juu ya mgao kwasababu ya uchakavu wa mitambo. Wanasahau wako pale kuhakikisha wanatengeneza umeme. Hayo mambo ya uchakavu wa mitambo au umeme usiotosha wako kama expertise in the area hawawezi kutupa majibu yake?
 
Inaonyesha wazi Tanesco halifanyi biashara na hawaelewi faida ya biashara yenyewe. Mgao wa umeme utalipunguzia shirika mapato makubwa tu lakini si mgao tu peke yake hata kukatika katika mara kwa mara kwa umeme pia unalikosesha mapato shirika.

Watendaji wakuu na wafanya kazi sidhani kama wanaelewa kama wapo hapo kibiashara wao wanadhani wanawapa wateja huduma ya bure ndio kwa maana hawajali kabisa eneo moja kukosa umeme hata kwa saa 12 bila ya kuurudisha hiyo ndio michezo yao ya kila siku.

Hadi hapo Serikali itakapofikiria kuwapa watendaji wenye akili ya kibiashara zaidi, Shirika hili haliwezi kumaliza matatizo yake kwa miaka 100 kwenda mbele.
 
Afisa mawasiliano nae anasema kwa tabasamu ooh gharama za uendeshaji ni ngumu na mitambo ni chakavu pia tunazalisha kwa hasara hatuna faida ndo maana tunakumbwa na tatizo hili..Mmmh
hapa nilipo kila siku umeme unakatika hata kwa masaa 10 na zaidi habari ya mgao imeniacha hoi kwani mie nilijua mgao ulishaanza long time ..
 
Kwani alishawahi kueleweka?! Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?

JB,

Alivyokuwa Tabora juzi, amesema maneno ya kusgangaza... "watanzania vumilieni katika maisha yenu magumu, serikali ianyafanyia kazi, na tusitegemee kama yatabadilika kwa fedha za wawekezaji wagen..." Nilishangazwa sana na haya.

Muungwana leo ameshau kabisa slogan zake "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" Arrg...ngoja tusonge na mgao tuone...:mad:
 
Afisa mawasiliano nae anasema kwa tabasamu ooh gharama za uendeshaji ni ngumu na mitambo ni chakavu pia tunazalisha kwa hasara hatuna faida ndo maana tunakumbwa na tatizo hili..Mmmh
hapa nilipo kila siku umeme unakatika hata kwa masaa 10 na zaidi habari ya mgao imeniacha hoi kwani mie nilijua mgao ulishaanza long time ..

sometime inabidi ucheke tu .Na mafuriko yote gharama za uendeshaji ni ngumu. Sasa tutegemee nini Ikiwa masika vifaa chakavu. ikiwa kiangazi kina cha maji kimeshuka.

Kumbe ile mikopo waliyochukua benki ya kuimarisha miundombinu haikufanya kazi yake badala yake wakakarabati nyumba wa wakubwa kwa mamilioni.

Wataalam na wenye data kwani IPTL,Songas wanachangia % ngapi ya mahitaji ya grid kwa siku?
 
Ndo maana nahisi jamaa wamejipa kazi rahisi kabisa ya kusubiri muda wa kuwaita waandishi wa habari na kuwatangazia mgao wa umeme badala ya kuwaita ili kuwatangazia kupatikana kwa vyanzo vingine vya umeme. Kama kuna sehemu tumepachafua na kupachakaza basi ni Tanesco. Sijui hata kama watu pale wanajua wanatakiwa kufanya nini!!!
 
Sie hatuna mgao wa umeme,haujawahi kuwepo umeme kwetu, zamu yetu haijafika tangu uhuru, so kutushawishi kupinga mgao wa masaa 5 ni unyanyapaa wa hali ya juu, tupiganieni tupate angalau nguzo tuanze kuishi kwa matumaini then we CAN support you in your strike.masika hii wamewadanganya chanzo maintanance, kiangazi ukame, jamaa ni mabingwa wa kujenga vijisababu hamuwawezi, kinachofata watawaambia uhaba wa mafuta ya transfoma,!!!!
 
Hivi viongozi wetu ni wehu au sisi wananchi (wapiga kura) ndio wehu? maana hamuwezi kusema maneno yale yale kila siku na hakuna linalobadilika. Kuna tatizo hatulioni, kwamba pengine anayeambiwa maneno hayo ni kiziwi na mnadhani anasikia au msemaji ni bubu anadhani kelele zake zinaeleweka.
 
Kutokana na uchakavu wa mitambo bla bla bla... mgao wa umeme kuanza nchini kote kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne (+or -) .. bla bla bla..

Habari ndiyo hiyo.. miradi ya Jenereta iko juu! Hatimaye salimu amri mnunue majenereta ya Dowans kwa Bilioni 69 ambayo mmeshawalipa bilioni karibu 40 kuyasafirisha!
Please can someone put Tanesco's strategic plan here? seems alot of excuse to defend the truth, when are we going to have reliable power supply in the country?
 
wakati mwingine huwa natamani kuikimbia nchi yangu..lakini..
Labda iko siku isiyona jina mambo yatakuwa shwari .
Tufunge na kuomba :mad:

Kweli kabisa tena tuombe mungu atuinulie wakina wakina Kalebu la sivyo kanani tutaisikia tu kwani sisi tunajiona mapanzi tu!
 
Kutokana na uchakavu wa mitambo bla bla bla... mgao wa umeme kuanza nchini kote kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne (+or -) .. bla bla bla..

Habari ndiyo hiyo.. miradi ya Jenereta iko juu! Hatimaye salimu amri mnunue majenereta ya Dowans kwa Bilioni 69 ambayo mmeshawalipa bilioni karibu 40 kuyasafirisha!

Huu ujanja ujanja na kutufanya watanzania wajinga tutaumaliza lini. Maana kwa mtu mwenye akili timamu huwezi ukamwambia eti machine moja moja imeharibika katika kila kwenye plant ya kuzalisha umeme, yaani Kidatu machine mmoja imeharibika, ubungo nako moja imeharibika na mtera nako hivyo hivyo pamoja na kihansi!!! How comes zote ziharibike muda mmoja!! If we are serious we need to find out how and why? Je, hakuna subotage kwamba ni deal la wazee wa Dowans kwamba wamewanunua baadhi ya technician for the said porpose ya kuuza Mitambo yao ya dowans??, Hapa binafsi na wasiwasi sana na hilo.

Na hi je Idrisa bado yupo Tanesco au ameshaondoka !!! kama yupo bado anafanya nini na nafasi ilishatangazwa kitambo!!! na kama ni mtuhumiwa wa ufisadi wa rada, hiyo tabia ya kifisadi atakuwa ameshacha lini?? Basi aondoke salama asije akalipuliwa na kuchomewa nyumba zake na watanzania wenye hasira.
 
Maumivu tunayapata. Lakini tumepigwa ganzi hatuyasikii. Uchaguzi unakuja; na hawa hawa wanaotuletea maumivu na kutuongezea ufukara tutawachagua tena.

Miafrika bana. Kazi kweli kweli.

Lakini nyie wapiga kelele watu wa mjini mnaopata umeme mbona ni negligible chunk ya voters, walio wengi vijijini hawaujui huo umeme kwa hiyo CCM haina cha kuikosesa usingizi kuhusu mgao. Sana sana mkijifanya kutaka kuchagua upinzani UWT and all government machinery wanaingia kazini kuhakikisha CCM inashinda.

Mambo yatabadilika pale "the masses" walioko vijijini wakiamka na kuwakataa hawa CCM kwenye ballot box ambapo kwa msingi huo sidhani kama hata wataweza kutumia hizo machinery zao ku-dictate outcome on their favour.

Kwa hiyo kazi bado ni mbichi mpaka watu wengi watakapoamka nadhani ndio kupona kwa nchi kunaweza kutokea otherwise status-quo itaendelea na wapiga kelele wa mjini tutaendelea tu with little effect.
 
Back
Top Bottom