Mganga wa jadi kutoka Sumbawanga

ABEDNEGO

Senior Member
Aug 20, 2009
109
30
Leo asubuhi toka ninatoke home Kibamba kwa Mkurya nimehesabu mabango ya Mganga wa jadi kutoka Sumbawanga hadi Ubungo kwenye mata yapata 19 ,Ni mabango tofauti yako kando ya barabara na moja pale Kimara Baruti liko kituoni kabisa,Sasa swali langu, Kwanza haya mabango wanalipia ushuru? Pili hawa waganga wa Sumbawanga ndiyo wana soko sana hapa Jijini? Na ni kwanini wajitangaze hivyo?Ina maana kwetu tuliotoka Sumbawanga ndiko chimbuko la uganga wa jadi????
 
Wameandika mabango kadiri ya sehemu wanakotoka, maana hawaonei aibu taaluma yao. Ilikuwepo kabla ya dawa za kisasa kuwepo. Hawa ni tofauti na wale waliozika jadi zao kwa kutanguliza mbele jadi za wengine. Wanatoa fundisho la kujali jadi.
 
Hao wote ni waongo, kuna mmoja nimewahi kwenda nikakuta ameyapanga madawa yake majina ya vijiji vya Sumbawanga. Alipogundua mimi ni wa huko akawa mkali na akanifukuza, kisa nilimsemesha kilugha kumbe hata sumbawanga hakufahamu. Kifupi ni kuwa wengi wanatumia Sumbawanga kujipatia wateja!
 
Siongezi wala sipunguzi. Posutaaa "mkombe".
 
Hao wote ni waongo, kuna mmoja nimewahi kwenda nikakuta ameyapanga madawa yake majina ya vijiji vya Sumbawanga. Alipogundua mimi ni wa huko akawa mkali na akanifukuza, kisa nilimsemesha kilugha kumbe hata sumbawanga hakufahamu. Kifupi ni kuwa wengi wanatumia Sumbawanga kujipatia wateja!
Mkuu wewe unaonekana mkweli,tunaomba utueleze ulienda kufanya nini kwa mganga?
1-kutaka kupandiswa cheo
2-Dawa ya nguvu za kiume
3-kumwita mpenzi wa mbali
4-kuomba mganga usikatiwe umeme nyumbani kwako
 
Mkuu wewe unaonekana mkweli,tunaomba utueleze ulienda kufanya nini kwa mganga?1-kutaka kupandiswa cheo2-Dawa ya nguvu za kiume3-kumwita mpenzi wa mbali4-kuomba mganga usikatiwe umeme nyumbani kwako
Ahahahahaaah!! Nilipita tu kutoa salamu kwa kujua ni mtu wa nyumbani, kumbe ni tapeli!!
 
Hao wote ni waongo, kuna mmoja nimewahi kwenda nikakuta ameyapanga madawa yake majina ya vijiji vya Sumbawanga. Alipogundua mimi ni wa huko akawa mkali na akanifukuza, kisa nilimsemesha kilugha kumbe hata sumbawanga hakufahamu. Kifupi ni kuwa wengi wanatumia Sumbawanga kujipatia wateja!
kuna mwingine Bukavu kaandika anatoka Sumbawanga Namanyere wateja kibao.
 
Hawo ni wengi sana Jijini Dar kila kona Mganga kutoka Sumbawanga anatibu kiharusi,kisukari,Ukimwi,Mvuto wa mapenzi,Kurudishiwa mali ulizoibiwa nk nk Hawa ni matapeli wa kupindukia wanatumia Sumbawanga kama deal ,Kwani tunaaminishwa kuwa huko ndiko kiboko ya wachawi.Jamani kama jirani yako ni mganga wa kutoka Sumbawanga mweendee kwa mjumbe amtimue maana ndo wanadanganya vijana wetu kuwa vibaka kwani wakiwafanyia dawa hawakamatwi!!! Piga ua hao ni matapeli ya mjini tuu.
 
Yaani hawa jamaa wanakera sana, mbona Sumbawanga kwenyewe hatuwaoni.....huku nako wanatudanganya kuna vibao vya waganga kutoka Tanga na Bagamoyo!!!
 
Hao wote ni waongo, kuna mmoja nimewahi kwenda nikakuta ameyapanga madawa yake majina ya vijiji vya Sumbawanga. Alipogundua mimi ni wa huko akawa mkali na akanifukuza, kisa nilimsemesha kilugha kumbe hata sumbawanga hakufahamu. Kifupi ni kuwa wengi wanatumia Sumbawanga kujipatia wateja!

Aisee great thinker kumbe na wewe huwa unaitumiaga hiyo huduma ya nguvu za giza? Ina maana asingetumia majina ya vijiji vya sumbawanga au usingeshtuka ulikuwa upate huduma ya kimapepo pale?
 
Ulienda kwa mmoja then ukahitimisha kuwa wote ni waongo ? Nafikiri mganga atakuwa anatibu magonjwa yanayoeleweka na wengi,inapokuja mgnga anatibu hata vyeo maofisini binafsi hapo naona ni utapeli tu,Naamini mganga wa kienyeji atakuwa anatibu magonjwa ambayo ni hakika yanajulikana,Malaria,pumu,TB nk.Lakini mganga anayemwita mpenzi,anarudisha mali iliyopotea,anaongeza mvuto na mengine mengi yafananayo na hayo Hakika hizo ni nguvu za giza wala si uganga.
Tuwape heshima zetu waafrika wenzetu wanaojua tiba za asili za magonjwa yetu,tuache kuwabeza waganga wa asili wa ukweli.
 
Back
Top Bottom