Mganda amficha mtoto akidai million 2

Mar 6, 2010
74
0
MTU anayedaiwa kuwa ni raia wa Uganda (Jina linahifadhiwa) anasakwa kwa tuhuma za kumteka mwanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya msingi Chuma mkoani Tanga, Amani Mohamed (7) ambapo ili amrejeshe kwenye familia yake ametaka kulipwa Sh 2 milioni na ametoa muda wa siku 14 asipotimiziwa basi maisha ya mtoto huyo yatakuwa hatarini.

Mganda huyo anadaiwa alifikia nyumba ya kulala wageni inayofahamika (jina linahifadhiwa ) ambapo alitengeneza urafiki wa karibu na mtoto huyo aliyekuwa kipenzi cha watu wengi wa rika tofauti kutokana na nidhamu aliyokuwa nayo kulingana na alivyolelewa na familia yake.

Baba mdogo wa mototo huyo Musa Salimu alisema tangu mtoto alipotekwa hadi leo hii bado hajapatikana na hajulikani mahali alipo wameshindwa kuishi kwa amani ikiwa ni pamoja na kushindwa kula kama sehemu muhimu ya maisha ya binadamu wa kawaida na hawajui la kufanya.

Hata hivyo alisema tayari walitoa ripoti polisi na hatua kadhaa zimeanza kuchukuliwa ambapo baadhi ya watu wanaelezwa kukamatwa kwa mahojiano ingawaje bado hayajazaa matunda kwa mtoto wake huyo kupatikana na kuungana na familia yake ikiwa ni pamoja na kuhudhuria masomo.

Alisema awali mtekaji huyo alitoa siku 10 apewe Sh 2 milioni na sasa ameongeza siku nyingine tatu ambapo mtoto huyo alitoweka nyumbani kwao tangu Machi 9 mwaka huu na aliwahi kuzungumza kwa simu na bibi yake huku akimueleza kwamba hajui mahali alipo chini ya uangalizi wa mtekaji huyo.

Kwa mujibu wa mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni ni kwamba raia huyo wa Uganda alifika kwenye nyumba hiyo ya wageni na kudai kwamba aliingia nchini akimfuatilia rafiki yake aliyekuwa akisoma naye Makerere Uganda ambaye alimuazima cheti chake ili aweze kufanyia kazi Tanzania.

Alisema mganda huyo alieleza kwamba rafiki yake alishindwa mtihani alimuazima cheti hicho ambacho pia yeye angeweza kukitumia kufanyia kazi nchini Uganda ambapo kwenye kitabu cha wageni namba ya pasipoti yake ilisomeka 19214.
Mmoja wa wasamaria wema aliyeungana na familia hiyo ili kuwasaidia upatikanaji wa mtoto huyo, Alphonce Mboya alitoa wito kwa wasamaria wema kuisaidia familia ili kumbaini mtu huyo ambaye mpaka sasa hajulikani alipo na nini lengo lake hasa ingawaje anahitaji fedha hizo.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom