Mfungwa Tarime apanda juu ya mti na kutisha kujiuwa

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,481
1,364
Mfungwa mmoja wa gereza la tarime amepanda juu ya mti na shuka na kuanza kupiga kelele ya kwamba wananyanyaswa gerezani humo kwa kupigwa na kutopata chakula na kuna wenzao wawili teyari wamekwisha fariki. Ametisha kutumia shuka hilo kujiuwa endapo atapanda askari ktk mti huo na kudai hadi aje mkuu wa mkoa ndio atashuka na kudai vyombo mbalimbali vya haki za binadam wafike gerezani hapo kufanya uchunguzi, pia amedai kajitoa muhanga kwaajili ya wenzake na endapo atashuka anajua watamfanyia fitna kwa kumnyanyasa. Polis wametanda nje na ndani ya gereza hilo kuzuia waandishi wa habari kupiga picha eneo hilo walilodai hairuhusiwi kupiga picha, kwani kutokana na urefu wa mti huo watu walioko nje ya gereza hilo wanamwona.

Source WAPO radio
 
Kila mahali bora ya jana. Hongera kwa kujitoa sababu ya wenzio
 
Back
Top Bottom