Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa kumpata Rais wa Tanzania: CCM, TISS + Umaskini na Ujinga wa mTanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sniper, Mar 30, 2011.

 1. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,942
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naanza kwa kumnukuu Sumaye kwamba makundi matatu yanayoamuru nani awe kiongozi wa wananchi ni Wananchi, Chama mgombea anachotoka na Dola.
  Tangia uhuru, mtaji mkuu wa viongozi wa CCM kuingia madarakani umekuwa ni Umaskini na Ujinga wa mTanzania. Mtaji mwingine ni pamoja na TISS na vyombo vya dola. Mfumo mzima wa viongozi wa CCM kuingia madarakani umekuwa ukirahisishwa na vitu vifuatavyo:

  1.UMASKINI
  (a) Umaskini wa mTanzania.
  Asilimia kubwa ya watanzania wako vijijini, na ni hao ambao wengi wao ni maskini. Ni umaskini huo (pamoja na ujinga) unaopelekea fikra zao kuamua kuchagua viongozi wenye ushawishi mkubwa kifedha kuliko walio makini na wenye nia ya maendeleo. Mwananchi wa kijijini anawaza kwanza kesho atakula nini kuliko sera za kuletewa umeme au kujengewa daraja ambazo amekuwa akidanganywa kwa miaka nenda rudi. Mwananchi huyo anaona ni bora amchague mgombea anayemhadaa kwa khanga na kofia ya kujisitiri kuliko sera ambazo zimekuwa hazileti maendeleo kwa miaka mingi.

  (b) Umaskini wa mTanzania, mwanaCCM.
  Ni wazi kuwa ukitaka kugombea uongozi CCM ni lazima uwe na uwezo wa kifedha zaidi ya mgombea mwenza wa kuwashawishi wajumbe au wananchi wanaokuchagua. Sera za maendeleo sio kigezo muhimu tena. Hii ni katika ngazi zote udiwani, ubunge mpaka Uraisi na hilo limeshuhudiwa kwenye chaguzi zilizopita mfano ni pamoja na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika kumuingiza JK madarakani 2005 na 2010.

  Umaskini huu wa mwanaCCM ndio mtaji wa mgombea kupata nguvu na madaraka kichama. Nguvu ya kichama ndani ya CCM imekuwa ikipatikana kutokana na uwezo wa kifedha wa mwanachama na sio uadilifu au utumishi wake ndani ya chama. Wanachama wenye uwezo kifedha na wasio waadilifu wamekuwa wakiendelea kuogopwa, kutetewa maovu yao na kupata madaraka ndani ya chama na serikali kutokana na ufadhili wao.

  Mgombea wa CCM amekuwa haumizi kichwa kuhusu sera za kuleta maendeleo kwa kuwa anajua wajumbe hawana shida nazo hizo. Wajumbe wana shida na "noti nyekundu", kama mgombea mwenye uwezo wa kuzimwaga kuliko mwenzake anayegombea naye ndiye anayechaguliwa.
  Hii imeshuhudiwa kwenye chaguzi zote za miaka ya karibuni kuanzia NEC, UWT, UVCCM, Umoja wa wazazi n.k. Siku za chaguzi za viongozi wa CCM ukiwa mkoa husika, utashuhudia ni jinsi gani wagombea wanavyopita kwenye ma guest house usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi kugawa "bahasha" kwa wajumbe ili wachaguliwe. Hawapiti kueneza sera zao bali "bahasha" maana ndio zinazofanya mgombea wa CCM achaguliwe.


  2.UJINGA
  (a)Ujinga wa mTanzania.
  Huu ndio mtaji mkuu wa CCM, ujinga wa mTanzania. Asilimia kubwa ya watanzania wako vijijini, na ni hao ambao wengi wao hawajasoma ama wamesoma kwa kiwango cha chini cha elimu. Kutokana na ujinga uliowatawala, mwananchi wa kijijini fikra zale zinamtuma ni kheri amchague kiongozi aliyempa khanga na kofia kuliko yule aliyekuja na kuongea mambo ya msingi zaidi na hakumpa hata senti tano. CCM wamekuwa wakitumia ujinga huu(pamoja na umaskini) wa mTanzania kwa kusimamisha wagombea wenye uwezo mkubwa wa kifedha.

  Uchaguzi wa 2010 unaonyesha hili dhahiri pale waTanzania wa mijini walipokataa kuwa wajinga tena wa kuhadaiwa khanga na kofia kwa kuchagua Chadema badala ya CCM. Mtaji wa CCM umebaki vijijini ambako wananchi wengi bado wamebaki na akili ya kumpa kura yule atakayempa kofia, khanga au kubandika Tangazo kubwa la kijani "Chagua CCM" mbele ya kibanda chake.

  (b)Ujinga wa mTanzania, mwanaCCM.
  Inasikitisha kuona mjumbe wa CCM anashindwa kutambua ni kiongozi gani anayefaa katika kuleta maendeleo ya waTanzania na badala yake anachagua viongoz kutokana na ushawishi wao wa kifedha. Naungana asilimia 100% na aliyesema (nimemsahau jina) kuwa wanafikiria kwa matumbo.

  Wajumbe wanashindwa kutambua kuwa wanafanya maamuzi kwa niaba ya wananchi na hiyo bahasha wanayopewa (yenye nyekundu kadhaa), haitoweza kuwalisha wananchi hata kwa mlo mmoja, ni mjumbe na familia yake ndio watakao shiba matumbo na ni kwa siku chache kulinganisha na maendeleo ambayo yangepatikana kwa kumchagua kiongozi makini bila kuzingatia ushawishi wake wa kifedha.


  3. TISS VYOMBO VYA DOLA
  Kila mTanzania mwenye akili timamu anajua kuwa TISS imepoteza mwelekeo na ni kati ya idara ambazo sasa hivi hazitekelezi moja kwa moja majukumu yake ipasavyo. Kwa mujibu wa sehemu ya nne ya sheria inayounda (TISS) ya mwaka 1996, kazi na mamlaka ya TISS ni kukusanya habari, kuchunguza na kutathmini habari zote zinazohatarisha usalama wa taifa na hatimaye kuishauri serikali hatua muafaka za kuchukua kwa maslahi ya taifa.

  Miaka ya karibuni TISS imekuwa kama kitengo cha usalama ndani ya CCM, imeacha majukumu yake muhimu ya kulinda maslahi ya Taifa na sasa imebaki kujihusisha na wizi wa kura ili kumwingiza Rais wanayemtaka madarakani. Kazi zingine za TISS "ilizojiundia" ni pamoja na kubeba mikoba ya viongozi, kuwakuwadia mabibi viongozi, kuhesabu vizibo na kujigamba kwenye mabaa kuwa "unanijua mimi? mimi usalama!"

  Rais aliyepo madarakani ndie mwenye uwezo wa kumchagua mkurugenzi mkuu wa TISS. Hii inamfanya bosi wa TISS kuobey matakwa ya bosi wake, Rais, mwenyekiti wa CCM, wakati ambapo idara hii inabidi ifanye kazi yake kwa uhuru bila kuingiliwa. Kuingiliwa huku ndiko kunakoifanya idara hii kuacha kazi zake na kuanza kazi za kijasusi za kuisaidia CCM.

  Ushauri kwa TISS
  • Taratibu za kumpata bosi wa TISS zibadilishwe (asiteuliwe na Rais) ili kuepusha conflict of interests baina ya usalama wa taifa na siasa.
  • UWT wote wasijishugulishe na ushabiki wa vyama vya siasa
  • Recruitment procedures za TISS ziangaliwe upya. Siku hizi ukitaka kuwa UWT inabidi umjue mtu huko au mmoja wa ndugu yako awe ni UWT. Hii inapelekea kuwa na UWT ambao hawajui kazi zao hasa ni nini na ndio tunaokutana nao kwenye mabaa kila siku wakituambia "unanijua mimi? mimi usalama!"

  4.MVUTO WA MGOMBEA KWA WANANCHI.
  Baada ya Mwalimu Nyerere kufariki, CCM imekosa ujasiri wa kumsimamisha mgombea wa kiti cha Uraisi ambaye wanamwamini anafaa bila kuangalia mvuto kutoka kwa wananchi, kama alivyofanya Nyerere alipomsimamisha Mkapa. Uchaguzi wa mgombea umelenga zaidi kwenye swali "ni mgombea gani ambaye tukimsimamisha tuna uhakika wa kushinda?". Swali ambalo limekuwa likijibiwa na TISS. Hili ndilo linalopelekea viongozi wa CCM kupigana vikumbo kila siku kwenye vyombo vya habari, ili kutafuta mvuto wa kwao wenyewe au wa mtu wanayemtaka.

  URAISI WA 2015
  Kuna usemi usemao "Mwenye kisu kikali ndiye mla nyama". Kutokana na 1,2, 3 & 4 hapo juu, Raisi wa 2015 ni mgombea wa CCM ambaye atakuwa na ushawishi mkubwa wa kifedha na kichama UNLESS waTanzania tuubadilishe mfumo huu.

  "It doesn't have to be the way it is, Just because for the past 54 years, every day it is ". Watanzania inabidi tubadilike. Ugumu wa maisha ulioletwa na Serikali ya JK umewafumbua baadhi ya waTanzania wa mijini na kuona kumbe khanga na kofia hazisaidii. Matokeo ya ubunge 2010, majimbo ya mijini yanadhihirisha hili.

  Njia rahisi ya kubadilisha mfumo huu ni kuhamasisha elimu ya demokrasia vijijini. Vyama vya upinzani inabidi kuelekeza nguvu zake zaidi vijijini, ili wananchi wapate kujua ni kiongozi gani wakimchagua atawasaidia.
   
 2. p

  plawala JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tiba ya umaskini na ujinga ni kubadilisha katiba na kuweka mamlaka kwa wananchi wenyewe.
  Ujinga na umaskini huu ni wa kimfumo,elimu ya uraia itasaidia mambo kama kuwa na fikra mgando na hofu ya mabadiliko
  Hayo yote yanawezekana lakini inabidi kazi ifanyike
  Kuhusu TISS imefikia hatua mpaka baadhi ya wakuu wa wilaya wanatishia madiwani wanaotaka kutenda haki kuondolewa kwenye nafasi zao kwa msaada wa TISS.ulivyosema ni kweli
   
 3. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,232
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  well said,,
   
 4. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,942
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  2015 huu mfumo waTanzania inabid tuubadili
   
Loading...