Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,786
Mfumo wetu wa kumpata Rais wa Jamhuri ya Tanzania uonekane wa kidemokrasia na halali zaidi ni kuufumua na kuja na mfumo eleweka unaozingatia haki na usawa.
Nilitafakari kwa kina uhalali wa mfumo wa uchaguzi wa Marekani na hoja ya kuchagua Rais kwa kutumia " electoral votes" badala ya " popular votes" na kubaini kuwa mfumo huo nihalali, mahiri,mzuri na wakuigwa na nchi zenye mfumo wa muungano na kuwa na Rais mmoja mtendaji.
Jamhuri ya muungano ni nchi mbili zilizoungana( Tanganyika na Zanzibar) na zina mfumo wa kuwa na Rais moja mtendaji,hivyo inapaswa Rais anaechaguliwa awe ana uhalali wa kupata ridhaa za pande zote za nchi washiriki wa Muungano.Hivyo kuondosha dhana ya mmoja mkubwa ya kumtawala mwenzake.
Kwa mfano tokea mfumo wa vyama vingi ulipoanza kutumika wakumpata Rais wa Jahuri ya muungano waTanzania hakuna awamu hata moja ambayo Rais wa Jamhuri alikubaliwa na wapiga kura wengi kutoka Zanzibar, nchi mshirika wa muungano.
Mara zote chaguo la wazanzibari limekuwa mgombea wa chama cha upinzani.Kwa vile maamuzi ya wazanzibari walio wengi hayathaminiwi hata kidogo,hali inyaleta manun'guniko upande mmoja na kumfanya hata Rais mwenyewe kutowajibika ipasavyo kuwahudumia watu ambao kwake hawana umuhimu katika uchaguzi wa uteuzi wake.
Ukiwepo mfumo ambao utalazimu mgombea urais ahalalishe ushindi wake kwa kuapata zaidi ya nusu ya kura halali au za juu zaidi za kura ziliopigwa Zanzibar. Njia hii itawafanya wagombea na vyama vyao wachacharike na kuwajibika ipasavyo kuhakikisha kuwa haki za utawala zinatapakaa pande zote za muungano ikiwa kama wanataka kushika hatamu za kutawala JMT.