Mfumko wa bei za bidhaa-Hatari!!!

Kituku

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
238
24
Habari wanajamii
Nimeona nishee dukuduku langu pamoja nanyi wanajamii, ingawa ninafahamu kuwa si wote wanaoathirika na hali hii kutokana na utofauti wa vipato vyetu. ila ninaamini kwamba kuna baadhi yetu tunaumia na hili.
Hivi huu mfumko wa bei za bidhaa serikali inatufikiria nini wananchi??? kumekuwa na kupanda kwa gharama za bidhaa kila kukicha, kila mtu ana aamua apandishe kulingana na maamuzi yake, hivi serikali haitufikirii sisi tunaopokea mishahara ya TGs D???
Mafuta taa/kupikia/gari bei juu, hapa kwetu dizel mpaka 2200, sukari sasa ni 2000 @kg, mchele 1200, harage bei juu,bia juu daladala wamepandisha nauli.. Jamani hawa EWURA na wengineo wapo wapi? kwanini bei zanapanda tu watu wakiamka asubuhi? ..

Hali hii bunge halijajadili budget na makodi yake, je budget ikishapitishwa sisi wa vipato vya chini tutaweza kuishi kweli?... wabunge baada ya kujadili hali ya uchumi na mfumuko wa bei kazi kubishania ubora wa vyama....
Natamani kuukana utanzania mie!!!!
 
Ndiyo maana mimi niko tayari kwa maandamano ya kuipinga Serikali hii siku yoyote, Kuana mtu athiriki na mfumko wa bei!? hata kama unapokea mil 5, lazima utaathirika tu kwa njia moja au nyingine.....
 
Inauma sana, yaani hakuna anaedadisi au hata kutoa sababu ya vitu hivi... kweli ??? au ndio biashara huria?
 
kweli inaumiza. ulipotamani kuukana utanzania nadhani kuna mbadala wake na uendelevu wake, naomba nishirikishe nini kitafuata?
 
Najiaandaa kwa ya walioyafanya wa Misri na Tunisia
 
Kweli kabisa, yaani utafikiri serikali imelala usingizi hakuna hata anegusia kama vile ni jambo la kawaida.... au walishapanga kabla??
 
Back
Top Bottom