Mfuko wa Pensheni wa LAPF: Mkutano wa Sita wa Wadau-AICC-Arusha

hivi kwa nini kusiwe na mfuko mmoja tu wa pensheni kwa watumishi wa umma kuondoa huu utitiri wa mifuko usio na tija kwa wastaafu? Kila siku kuna mfuko uko arusha kufanya mikutano ya wadau ambao ni watu walewale!
ulaji watu wakale wapi. Wakurugenzi wangapi fikiria na familia zao x10= utapata idadi ya wanaofaidika na mifuko hii
 
Ingekuwa Mgeni rasmi katika mikutano hii haandikiwi Hotuba na mwenye mkutano, ningeamini yote Hawa Ghasia liyosema kuhusu LAPF. Watu wangeujua undani wa LAPF basi wanachama wangeandamana ili kujitoa kwenye Mfuko au kuing'oa Bodi na Menejimenti. LAPF inaanzisha miradi kila siku wakati mingine hata haijaanza kutekelezwa ili mkurugenzi mkuu apate 10% yake. Injinia alisimamishwa kazi kwa sababu alikataa kushirikiana na Sanga kuiba fedha za kulipia makontena ya vifaa vya hoteli ya Milinium Towers. Mizigo ilikaa bandarini bila kutolewa ikaongeza gharama za kuitoa zaidi ya 400m/. Mkurugenzi wa uwekeaji wa LAPF hajawahi hata kuulizwa wala kuandikiwa barua kujieleza. Analindwa na Sanga. Tuulize wafanyakazi tukwambie madudu yanayoendelea LAPF
 
Swadakta ndugu yangu Mentee. Eliudi Betri Sanga, mkurugenzi mkuu wa LAPF ni fisadi wa kutisha. Anamiliki magari lukuki ya kifahari nyumbani kwake, Kimara stop-over Dar es Salaam. Pia anajenga hoteli za kitalii Mwanza, Arusha na Dar. Amenunua shamba kubwa sana Kiluvya, na pia anamiliki shule ya kisasa ya Fountain of Joy, Kimara Dar es Salaam. Hivi majuzi amenunua maeneo yanayozunguka shule yake kwa mamilioni ya shilingi, kawahamisha wakazi wa maeneo hayo kupisha upanuzi wa shule yake ya kifisadi. Ana jumba la kifahari alilonunua Mikocheni. Aidha, inasemekana amefungua akaunti nje ya nchi, Uswissi, Dubai na China. Huyu jamaa anashirikiana na mjumbe wa Bodi ya LAPF, Prof. Mlacha wa UDOM kudhibiti yeyote anayeonekana kuushtukia mtandao wao wa ufisadi. Mlacha anamiliki shule kubwa ya sekondari kwao, Makanya- Same. Hivi majuzi wawili hao wameshirikiana kuishawishi Bodi ya LAPF kumwachisha kazi mtumishi mmoja, baada ya mtumishi huyo kufichua njama za Sanga na Mwanasheria mkuu wa LAPF, Fidelis Mutakyamilwa za kuiba zaidi ya dola 268,000 kwa kushirikiana na kampuni ya African Focus ya tapeli moja toka Bulgaria kwa jina la Kirov. Inasikitisha jinsi pesa za wanachama zinavyotafunwa na watu hawa. Sanga ameingia mikataba mikubwa ya ujenzi bila kujali uwezo wa Mfuko kuhimili gharama, kwa maana ya cashflow, lengo
likiwa kuvuta 10%. Matokeo yake anachakachua bajeti ya Mfuko kwa ku-manipulate financial ratios ili kuihadaa Bodi na wanachama kuwa Mfuko ni finacially sound. Wizi mtupu!!!
 
Mh! Kama haya ni kweli basi Serikali na SSRA imelala usingizi wa pono!!!!!! Inakuwaje haya yote KAMA NI KWELI yafanyike na Serikali imekaa kimya???

Hii Mifuko kuna pesa sana maana zinaingia Kama mvua hivyo ukiwa kiongozi mwenye tamaa unakuwa fisadi kwa muda mfupi sana.

No wonder walikomalia pendekezo la SSRA la kuondoka madarakani baada ya miongo 2. Regulator amewahi kufanya kazi kwenye Mifuko anajua matanuzi yakoje! Kiongozi anapokaa kwenye Mfuko muda mrefu anakuwa Mungu mtu. Yoyote anayekuja na mawazo mapya anashughulikiwa.

Serikali ishikilie msimamo wake wa kubadili ma DG waliotumikia miongo miwili. Big up regulator.

Mwisho bado naendelea kuipongeza LAPF kwa kutoa mafao bora, huduma bora na uwazi waliouonesha. Hata kuiacha hii thread iendelee kuwepo ilhali imemkosoa mkuu ni dalili ya ukomavu.

Hongera LAPF

Queen Esther
 
Kuna haja ya kupunguza hii mifuko ya ifadhi ya jamii, imekuwa mingi na inafanya kazi zile zile .
mifuko mingine inafanana hadi formula za pension (LAPF na PSPF), mifuko mingine nayo inaformula zake.
Yaani mi naona ni vurugu tupu.
Sasa tunaona jinsi mifuko inavyoanza kugombania wanachama, mifuko ambayo inajipambanua kabisa ni ya watu gani mfano (PSPF- Public Service Pension Fund) huu makusudio yake ilikuwa kuwahudumia watumishi wa Serikali kuu, sasa hivi unachukua hadi watu binafsi ngo's workers,wajasiriamali etc, LAPF nao hivyo hivyo ulikuwa unajitanabaisha na watumihi walioajiriwa na halmashauri, sasa nao kama PSPF.
Basi wabadilishe hata hayo majina yao ili waelemweke vizuri ,. Kwangu mimi haiingi vizuri akilini mfuko uitwe Mfuko wa Pensheni kwa ajili ya watumishi wa umma , halafu hapo hapo ujumuishe wajasiriamali etc,
siwatengi wala siwanyanyapai wasiokuwa watumishi wa umma, hiyo mifuko LAPF na PSPF ijibadili majina ili ieleweke.
Nadhani ingekuwa vyema pia serikali ikaangalia hii mifuko imekuwa mingi sana na inafanya kazi moja, mingine kwa kufanana kabisa na mingine tofauti kabisa hadi kuwafanya wachangiaji kulalamika.
Kwasasa hapa nchini kwetu tuna mifuko PSPF.LAPF,NSSF,PPF, GEPF
Ni heri mifuko hii iunganishwe uundwe mfuko mmoja utakaowajumuisha wananchi wote katika hali ya usawa kulingana atakavyokuwa anachangia
 
Back
Top Bottom