Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo: CDCF

Wale Wabunge waliotarajiwa kupinga huu mfuko, hasa wapinzani nao wameziba masikio na pamba. Hapa ndio kwa kiasi fulani tunapata Wabunge wetuwengi wako Bungeni kwa maslahi yao binafsi kuliko kuangalia Wananchi wanataka nini.
 
Hapa sio issue ya wananchi wanataka nini, hapa ni ulaji na kuhodhi majimbo kwa kisingizio cha mimi nimeleta maendeleo haya a haya hivyo nichagueni mpaka kufa kwangu. Tunatengeneza wabunge wa maisha.
 
Kesho ndio bunge linapiga kura kuupitisha muswada huo hivyo kugeuka sheria na kuanza kufanya kazi baada kusainiwa na JK. Ili muswada huo upite kiulaini, leo wabunge watafanya semina usiku pale bunge ili kuweka msimamo wa pamoja kesho kazi iwe kuupitisha tuu kwa ulani kama unamsukuma mlevi.
kikao hicho cha usiku ni cha faragha, waandishi hawaruhusiwi.
 
Labda yako ni word ya zamani ndo maana ikashindwa maana nimejaribu kudowload naona madudu tu.
 
Soma hii kwa ufasaha zaidi
''If you share text files with people who work in other languages, download text files across the Internet, or share text files with other computer systems, you might need to choose an encoding standard. Word uses the encoding standard to convert the file to and from Unicode. For more information, type the keywords About encoded text files in the Office Assistant.''
 
Mkutano wa kukusanya maoni ya wadau kuhusu muswada wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (Comunity Development Catalyst Fund-CDCF) uliofanyika jana mchana kwenye ukumbi wa Msekwa ulitawaliwa na vuta nikuvute kati ya Wabunge na wanaharakati wakiongozwa na Policy Forum.

Mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mbunge wa Mpwapwa, George Malima Lubeleje, ulifunguliwa kwa hotuba ya Waziri wa Serikali za Mitaa, Bibi Celina Kombani aliyeutetea mfuko huo huku akiungwa mkono na wabunge wote waliochangia wakiwemo wa upinzani ambapo Dr.Slaa alikomelea msumari wa moto kwenye jeneza la wanaharakati kuupinga muswada huo.
Nimefanikiwa kuupata muswada wenyewe na kuuscan sambamba na taarifa ya Policy Forum.
Swali ni moja tuu, baada ya kuuona muswada wenyewem hawa wanaoendelea kuupinga ni kweli wanasukumwa na utashi wao na dhamira za dhati, au ni kupuliza tarumbeta kusuport msimamo wa wafadhili wanaowapo fedha na posho za kuendesha mashirika yao?.
NB. Nimejaribu kuatach muswada na msimamo wa serikali zimenigomea

Namimi nina swali moja kwako: kama unaona nongwa kwa AZAKI kupewa misaada ya fedha na wafadhili ili wapinge uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo ya jimbo, mbona unafumba macho wakati wafadhili hao hao wanapochangia bajeti yetu kwa asilimia karibia 40? au ndio ule msemo kunya anye kuku, akinya bata uharo????
hapa wala kwa mtu mwenye uelewa mzuri na asiyesukumwa na maslahi binafsi au kushabikia mambo anaelewa wazi kwamba mfuko huu ni kwa ajili ya kuwasaidia wabunge. Kama mtu ulikuwa makini kuwasikiliza wanapojieleza/kuuelezea mfuko huu wanajigonga gonga tu, kwakuwa lengo mahsusi la mfuko huu ni kuwasaidia kupata fedha ya kutoa takrima.
kama kuna mtu alifuatilia mjadala wa jumapili star tv, maelezo ya Cheyo na Juma Nhunga yalikuwa yanatofautiana juu ya dhana nzima ya uanzishwaji wa mfuko huu. Hata juzi walipokutanishwa wabunge na wanaharakati dodoma, bado maelezo ya wabunge yalikuwa yanatofautiana, mathalani maelezo ya Godfrey Zambi na Dr. Slaa yanatofautiana. Kilichoko hapa ni kwamba kuna baadhi ya wabunge wako very smart wanapouzungumzia mfuko huu ili mtu usiweze kuona dhamira ya mfuko huu, sasa wale wasiojua kuchagua maneno ndio huwa wanakurupuka na kujikuta wametoboa siri wanayoificha.Takrima imepigwa chini mahakama kuu imeibukia bungeni kwa mara nyingine tena. Kaaaazi kweli kweli watanzania.
 
Hapa sio issue ya wananchi wanataka nini, hapa ni ulaji na kuhodhi majimbo kwa kisingizio cha mimi nimeleta maendeleo haya a haya hivyo nichagueni mpaka kufa kwangu. Tunatengeneza wabunge wa maisha.

Mkuu Pasco hapa sijakuelewa vizuri, unaunga mkono kuanzishwa kwa mfuko huu na unawashangaa wanaharakati kuupinga japo unaamini kuwa lengo lake ni kutengeneza ulaji na kuhodhi majimbo.
Msimamo wa Dr. Slaa katika hili ni vyema ukatazamwa kwa kuangalia role yake katika kuanzishwa kwa muswada huu. Picha yenyewe ilianzia kwake, yeye na kamati anayoiongoza walianza kufanya utafiti juu ya mifuko kama hii huko Kenya, Malawi na India.Kwa bahati mbaya Slaa na wenzake hawakwenda kujifunza bali walitaka ku confirm wanachokitaka hivyo walifumbia macho uozo wote waliouona na kurudi kuishauri serikali kuanzisha mfumo huo. Japo si suala jema kulizungumzia kwa sasa ila Slaa na kamati yake walitumia pesa za walipa kodi 'hovyo hovyo' na kushindwa kuishauri serikali vizuri. Na kwa kuwa serikali inalengo la kulidhoofisha bunge hasa baada ya mhimili huu kuanza kuonesha cheche zake ililikubali wazo hili harakaharaka. Pasi kufanya tafiti au kusikiliza ushauri kutoka pande nyingine serikali imedhamiria kulipeleka suala hili mbele kwa kujua iwapo wabunge watalipitisha litakuwa ni aibu kubwa kwao kwa sababu mosi kutokusikiliza wananchi ambao wao ni wawakilishi wao na pili ni kushirikiana nao(serikali) kuvunja katiba hivyo mara zote wataendelea kuoneana aibu.
 
Mkuu,
Yaani umemaliza yote yote kabisa ktk hili.
Mimi wala sitaki kabisa kusikia hii kitu. Yaani bunge limeshindwa kuisimamia na kuidhibiti serikali yenyewe inataka ipewe fedha iende yenyewe! Independence itakuwa wapi??? Nani atauliza kama fedha za mfuko zitatumiwa vibaya??? Who is going to question that?? Upuuzi upuuzi kabisa.

Yaani ukitazama jinsi baadhi ya majimbo ya wapinzani yanvyosahauliwa wakati wa utekelezaji wa ilani ya chama tawala utashukuru kwa wao kuanzishiwa mfuko huu. Swala lililo tatizo ni namna ya kuhakikisha fedha haipotei.

Anagalieni wenzetu wakenya, waganda na wajamaica wamefanya nini katika mfuko wa aina hii and they are more corrupt than us.

Wanaharakati lazima wataupinga kwa kuwa hii kazi inayofanywa na wanasiasa ndiyo wanayopaswa kufanya wao.
 
Mkuu Pasco hapa sijakuelewa vizuri, unaunga mkono kuanzishwa kwa mfuko huu na unawashangaa wanaharakati kuupinga japo unaamini kuwa lengo lake ni kutengeneza ulaji na kuhodhi majimbo.
Msimamo wa Dr. Slaa katika hili ni vyema ukatazamwa kwa kuangalia role yake katika kuanzishwa kwa muswada huu. Picha yenyewe ilianzia kwake, yeye na kamati anayoiongoza walianza kufanya utafiti juu ya mifuko kama hii huko Kenya, Malawi na India.Kwa bahati mbaya Slaa na wenzake hawakwenda kujifunza bali walitaka ku confirm wanachokitaka hivyo walifumbia macho uozo wote waliouona na kurudi kuishauri serikali kuanzisha mfumo huo. Japo si suala jema kulizungumzia kwa sasa ila Slaa na kamati yake walitumia pesa za walipa kodi 'hovyo hovyo' na kushindwa kuishauri serikali vizuri. Na kwa kuwa serikali inalengo la kulidhoofisha bunge hasa baada ya mhimili huu kuanza kuonesha cheche zake ililikubali wazo hili harakaharaka. Pasi kufanya tafiti au kusikiliza ushauri kutoka pande nyingine serikali imedhamiria kulipeleka suala hili mbele kwa kujua iwapo wabunge watalipitisha litakuwa ni aibu kubwa kwao kwa sababu mosi kutokusikiliza wananchi ambao wao ni wawakilishi wao na pili ni kushirikiana nao(serikali) kuvunja katiba hivyo mara zote wataendelea kuoneana aibu.

Pasco anatambua kwamba huumfuko ni ulaji kwa namna nilivyomuelewa, lakini anaonekana kukubaliana na hali hiyo kwa vile wanaoupinga wanapata vijisenti vya wafadhili na kwamba anaona bora wabunge nao wapate vijisenti vya kuwapa wananchi takrima wakati wa uchaguzi wa mwakani.
 
Tatizo letu watanzania ni kupenda kupinga kila kitu. I for one support this. Wekeni huu muswada hapa halafu tuujadili.
 
Hivi ukiwaacha wanaharakati ambao wapo katika NGO amabzo nyingi zinakuwa funded na wafadhili kutoka nje, haiwezekani -----sisi wanaharakati wengine/au wasomi kuandaa forum na wabunge.....hata wakigoma kuja (lakini ukishawaambia kuwa kuna posho huwa hawagomi!!) tukaongea na kuweka hoja wazi kwa watanzania wote??!

Vyuo vikuu mpo???? SUA, UDOM, UDSM, Mzumbe wapi jamani??

Inaudhi......uzembe wa kutimiza majukumu isiwe kisingizio cha kubadilisha majukumu.
 
Cha umbeya kwanza unatakiwa ujue wanaharakati wanapinga kuanzishwa kwa CDCF na si muswada wa sheria ya CDCF, hapo kama hujanipata hivyo ni vitu viwili tofauti. Japo hilo la pili linategemea la kwanza ila si lazima sana kuwepo kwa mfuko huu sambamba na sheria ndio maana malawi wanaendesha mfuko huu bila kuwepo kwa sheria.Wanaharakati madai yao ni makubwa zaidi ya sheria, wanachosema hatuwezi kuwa na sheria nzuri inayopingana na katiba kwa hiyo hata ukipata mazuri kiasi gani ambayo nina doubt kama yapo alimradi yanakinzana na katiba yote ni uozo tu. Nakushauri anza kwanza kupitia kifungu cha 63(2) cha katiba kabla haujautafuta muswada huu.
 
Pasco anatambua kwamba huumfuko ni ulaji kwa namna nilivyomuelewa, lakini anaonekana kukubaliana na hali hiyo kwa vile wanaoupinga wanapata vijisenti vya wafadhili na kwamba anaona bora wabunge nao wapate vijisenti vya kuwapa wananchi takrima wakati wa uchaguzi wa mwakani.
Asante Mwita Maranya kwa kunielewa, mimi ni realist, hata kama siupendi huu mfuko, ni ulaji kwa wabunge, hata upingwe vipi leo unapitishwa. Kama realist ni lazima kukubali matokeo ya ambayo lazima yatatokea.
Niliwahi kusema naipenda demokrasia ya kweli na siupendi udikteta wa chama dola CCM, lakini wapinzani wanatudisapoint sana kwa kutoweza kuweka mgombea mmoja kwenye urais kupambana na JK, hivyo hakuna ubishi JK atashinda kwa kishindo, hivyo kuliko kuipoteza kura yangu, you play with the winning team, 'if you can't beat them, join them and fight from within'.
Niko hapa Dodoma na kesho natia timu mjengoni kushuhudia kwa macho yangu mwenyewe na kusikia kwa masikio yangu mwenyewe jinsi waheshimiwa wabunge wetu wakijipatia ulaji wa kuwajengea uwezo wa kutoa 'takrima maendeleo';
 
Tatizo letu watanzania ni kupenda kupinga kila kitu. I for one support this. Wekeni huu muswada hapa halafu tuujadili.
Ninao na nimeuscan ila unagoma kujiatach sijui tatizo nini, kesho nitamtupia invi aubindike ila fainali ndio leo, jamaa wanaupitisha.
 
Mfuko huu ni mbinu ya Wabunge kutafuta fedha za kampeni 2010,hii ni aina nyingine ya Takrima,fedha za walipa kodi zinachezewa na wawakilishi tuliowaamini.
 
Mkuu Mwanakijiji, umesahau mfuko mwingine, huu utaitwa mfuko wa maendeleo ya Kata unajua tena kuna Waheshimiwa wengine hapa wanaitwa madiwani, nao watataka ka mfuko kao kakutesea huko kwenye kata zao!

Ama kama vipi tukubaliane tu hatuna mhimili wa Bunge kama wawakilishi wenyewe ndio hawa wameshindwa kuelewa wajibu na majukumu yao! wameishia kuwa ni wazee wa ahadi na wanafikiri dawa ni kuanzisha mifuko! mbona vitu kama harusi Watanzania huwa tunaweza kuhamasishana! tunashindwa nini kuhamasishana katika masuala ya kujitafutia maendeleo yetu wenyewe mpaka tumesahau misingi tuliyoachiwa na wahenga wetu? Mwalimu alisema, pesa ni matokeo na sio msingi wa maendeleo au ndiyo yale yale ya penye udhia penyeza njuruku?
NAPINGA HOJA KWA ASILIMIA MIA MOJA 100%
 
Naona wakati tunaendelea kuchambua hoja za wabunge na fuko lao hilo la Jimbo pamoja na kwamba serikali ya CCM iliuzika rasmi ukweli na busara, hekima vilivyokuwamo ndani ya AZIMIO LA ARUSHA kupitia Azimio batili na la kihaini la Zanzibar ukweli unabakia pale pale! Tuendelee kukumbushana na hapa naomba kuwashushieni kipande kimoja toka katika AZIMIO LETU TUKUFU LA ARUSHA

Mnyonge hapigani kwa Fedha:

Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua
silaha; kwani silaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa
unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo
sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na
vitendo vyetu ni kama tumekata shauri kwamba bila fedha mapinduzi
yetu hayawezekani. Ni kama tumesema, "Fedha ndiyo msingi wa
maendeleo. Bila fedha hakuna maendeleo"!

Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao ni
kwenye fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi,
mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha. Viongozi wa
wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA, Bunge, UWT.,
Vyama vya Ushirika, TAPA na makundi mengine ya wananchi,
mawazo yao na maombi yao na matumaini yao ni FEDHA. Ni kama
wote tumekubaliana na tunasema kwa sauti moja, "Tukipata fedha
tutaendelea, bila fedha hatutaendea"!
Mpango wetu wa maendeleo ya miaka mitano shabaha zake
kwa kifupi ni shibe zaidi, elimu zaidi na afya zaidi. Na silaha yetu
tuliyotilia mkazo sana ni fedha. Ni kama tumesema, "Katika miaka
mitano ifuatayo tunakusudia kujiongezea shibe, elimu na afya, na ili
kutimiza shabaha hizo tunatumia $ 250,000,000". Kama tumetaja na
tunapotaja vyombo vingine vya kututimizia shabaha hizo tunavitaja
kama nyongeza tu; lakini chombo kikubwa katika akili zetu, silaha
kubwa katika mawazo yetu, ni FEDHA.
Mheshimiwa Mbunge anaposema kuwa wananchi wa sehemu
yake wana shida ya maji, je Serikali ina mpango gani wa kuondoa
shida hiyo? Jibu analotaka ni kwamba: Serikali inao mpango wa
kuwapa maji wananchi wa sehemu hiyo – KWA FEDHA.
Mbunge mwingine anaposema kuwa sehemu yake haina
barabara au shule au hospitali au vyote, je, Serikali ina mpango gani?

Naye pia jibu ambalo angependa kupewa ni kuwa Serikali inao
mpango safi kabisa wa kutengeneza barabara au kujenga shule au
hospitali au vyote kwa wananchi wa sehemu ya Mbunge Mheshimiwa
huyo - kwa FEDHA.
Kiongozi wa NUTA anapoikumbusha Serikali kuwa mishahara ya
chini kwa wafanyakazi wengi bado ni midogo mno na nyumba
wanazolala si nzuri, je, Serikali inao mpango gani? Jibu apendalo
kusikia ni kuwa Serikali inao mpango maalum wa kuongeza
mishahara na kujenga majumba bora - KWA FEDHA.
Kiongozi wa TAPA anaposema kuwa wanazo shule nyingi sana
ambazo hazipati msaada wa Serikali. Je Serikali ina mpango gani wa
kuzisaidia shule hizo, jibu analopenda kusikia ni kuwa Serikali iko
tayari kabisa kesho asubuhi kuzipa shule hizo msaada unaotakiwa -
wa FEDHA!
Kiongozi wa Chama cha Ushirika akitaja shida yo yote ya
mkulima jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali itaondoa shida hizo za
mkulima – kwa FEDHA. Mradi kila shida inayolikabili Taifa letu
wananchi tunawaza Fedha, Fedha, Fedha!
Mwaka hata mwaka kila Wizara na kila Waziri hufanya
makadirio yake ya matumizi – yaani fedha wanazohitaji mwaka huo
kwa kazi za kawaida na mipango ya maendeleo. Waziri mmoja tu na
12
Wizara moja tu hushughulikia pia kufanya makadirio ya mapato. Ni
Waziri wa Fedha. Kila Wizara ina mipango mizuri sana ya
maendeleo. Wizara zinapoleta makaidirio yao ya matumizi huwa
zinaamini kwamba fedha zipo ila mkorofi ni Waziri wa Fedha na
Wizara yake. Na kila mwaka lazima Waziri wa Fedha na Wizara yake
awaambie Mawaziri wenzake na Wizara zao kwamba hakuna fedha.
Na kila mwaka Wizara zote huinung'unikia Wizara ya Fedha kwa
kupunguza Makadirio yao ya matumizi.
Kadhalika Wabunge na Viongozi wengine wanapodai Serikali
itimize mipango mbali mbali huwa nao wakiamini kwamba fedha zipo
ila mkorofi ni Serikali. Lakini kukataa huku kwa Wizara, na Wabunge
na Viongozi wengine hakuwezi kuondoa ukweli; nao ni kwamba
Serikali haina fedha.
Na kusema kuwa Serikali haina fedha maana yake ni nini?
Maana yake ni kuwa Wananchi wa Tanzania hawana fedha. Kiasi
walichonacho hutozwa kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha
shughuli za Serikali hivi sasa na maendeleo mengine ya nchi.
Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa fedha
tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama Serikali haina fedha
zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi.
Ukidai Serikali itumie fedha zaidi unataka izipate; na njia ya
kuzipata ni kodi. Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi
13
zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi
bila kutaka Ng'ombe akamuliwe tena. Lakini kukataa huku kukiri
kwamba tunapodai Serikali itumie fedha zaidi nia yetu ni kutaka
Serikali iongeze kodi kunaonyesha kuwa tunatambua ugumu wa
kuongeza kodi. Tunatambua kuwa ng'ombe hana maziwa zaidi;
kwamba hata ng'ombe mwenyewe angependa ayanywe maziwa hayo
au yanywewe na ndama wake au yauzwe yamfae yeye na jamaa
yake; utashi huo hauwezi kuondoa ukweli kwamba hana maziwa
zaidi.

AZIMIO LA ARUSHA 1967
 
Kwa taarifa tu sheria ya mfuko wa jimbo imepita tayari na mswada umesomwa kwa mara ya tatu inasubiri hatua ya rais
 
Mimi nina wasi wasi na huu mfuko wa jimbo kama CAG hatakuwa anafuatilia kuhakikisha gharama kuhusiana na mfuko huo za Waheshimiwa zimetumia kwa manufaa ya majimbo yao, vinginevyo itakuwa ni ufisadi mwingine ambao waheshimiwa wanaweza kabisa kuutumia kwa ufisadi wa aina mbali ikiwemo kutoa rushwa ili kununua kura wakati wa uchaguzi.
 
Hatimaye ule muswada tata wa Mfuko wa Maendelea ya Jimbo, CDCF, umepita kwa kishindo kikubwa cha kihistoria ambapo ndoa rasmi ya wabunge wa CCM na Wapinzani imezaliwa kwa wote kuunga mkono hoja kwa asilimia 100 bila pingamizi lolote wala any reservation huku vijimambo vikijiri kwenye upitishaji wa mswada huo.
1. Kuna wabunge walisema wangepinga
2. Jana usiku baada ya kuahirishwa bunge, kilifanyika kikao cha siri cha wabunge wote.
3.Leo baada ya kuwasilishwa, wachangiaji wote waliunga mkono hoja kwa asilimia 100.
4. Waziri Membe akachangia kwa sauti ya ukali na kutoa karipio kali kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao humu nchini kwa kuingilia mambo ya ndani..(he who pays the piper may call the tunes)
4.Bunge likakaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu, vyote viliafikiwa bila reservation yoyote!
5.Muswada uliposomwa kwa mara ya tatu, Speaker Sita alighafilika na kuupitisha moja kwa moja bila kuwauliza wabunge, akakumbushwa ndipo akawauliza na wote wakaafiki, muswada huo, ukapita kiulaini.

Haya sasa mfuko wa maendeleo ya majimbo umepita, tusubiri maendeleo ya majimbo yatakayo tupeleka kwenye maisha bora kwa kila Mtanzania.
-Waheshimiwa Wabunge hongereni sana!.
-Wanaharakati poleni sana!.
-Nchi wafadhili asanteni sana kwa kutumwagia mahela na endeleeni kutufadhili kwa mahela ila msituingilie jinsi tunavyo taka kutumia, haya ni mambo yetu ya ndani.
Mungu Ibariki Tanzania!.
 
Back
Top Bottom